Wataalam wa Benki na Mikopo naombeni msaada kwa hili

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
5,066
2,000
Wale wataalamu wa kukopa na wenye ujuzi wa Bank na Mikopo, habari zenu?

Hivi nikikopa Benki na kila baada ya muda natop up!! Nitakuwa nafaidika au Benki itaninyonya zaidi Mimi?

Je, nikikopa mkopo wa miaka mitano na kusubiri hadi mkopo wote uishe ndiyo nikope nitakuwa na hasara?

Natanguliza shukurani zangu kwenu nyote mtakaotoa ushauri na maoni jenzi?
 
Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
636
1,000
Mikopo yote ya benki inaanza na riba kubwa na mtaji kidogo. Mfano: Makato yako ni 200,000/= kwa mwezi.

Mgao wake utakuwa hivi.

Riba 150,000/=

Mkopo 50,000/=

Hivyo wao huanza kuchukua faida mapema hata ukitop up baadae au ukiuza deni wanakuwa wamekupiga tayari
 
Kim wa TZ

New Member
Feb 8, 2021
1
45
Inategemea na benki wametumia njia gani ya kutafuta riba.

1: Reducing method- benki watapata faida sababu utaanza kulipa riba kubwa na principal ndogo
2: Straight line: Huna hasara
Note
Reducing 18% ni kama 10% staright line ..kuwa mwangalifu kwa kuwa ukipewa straight line kubwa utajuta
 
Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
11,588
2,000
Yaelekea wengi humu hawajui hata mambo ya mikopo inaendaje.

Unapokopa mf 10 000 000 na banki ikakwambia itakukopesha kwa riba ya 21% maana yake fedha hiyo utairudisha 12 100 000 kama mkopo utakuwa ni wa mwaka mmoja basi utagawanya kwa miezi 12 hivyo kwa kila mwezi utatakiwa kulipa 1 008 333.
 
Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
5,066
2,000
Yaelekea wengi humu hawajui hata mambo ya mikopo inaendaje
Unapokopa mf 10 000 000 na banki ikakwambia itakukopesha kwa riba ya 21% maana yake fedha hiyo utairudisha 12 100 000 kama mkopo utakuwa ni wa mwaka mmoja basi utagawanya kwa miezi 12 hivyo kwa kila mwezi utatakiwa kulipa 1 008 333.
Kwa hiyo ni muhimu umalize ili ukope tena?
 
Lukonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
248
500
Wale wataalamu wa kukopa na wenye ujuzi wa Bank na Mikopo, habari zenu?...

Ingawa mimi si mtaalamu wa mambo ya mikopo.
Common sense inaniambia kuwa suala la msingi ni unakopa kwa sababu gani?

1: Kama utakopa pesa ambayo unawekeza na ku-service mkopo husika vyovyote itakuwa sawa.

2: Kama unakopa na kwenda kuweka heshima baa, mifumo yote haitakufaa.
 
Ze last Born

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
1,623
2,000
Katika maisha yetu ya utumishi wa kitanzania suala la mikopo haliepukiki.

Kimsingi huwa sishauri mtu akope bank mkopo wa zaidi ya miaka miwili. Mkopo wa kuanzia miaka mitano na kuendelea ni mateso kuliko unavyodhani maana riba huwa inaji-double kila mwaka hivyo Kama mkopaji utajikuta unarejesha pesa nyingi za bure bure na kuifaidisha bank.

Mkopaji asiye na elimu sahihi ya mikopo huwa anafurahia mikopo ya muda mrefu kwa kuwa anakatwa / anarejesha kiasi kidogo kwa mwezi lakini anasahau kadri maturity time ya mkopo inavyoongezeka ndivyo riba inavyoongezeka.

Kwa kuwa mikopo haiepukiki katika maisha ya utumishi basi kopa bank lakini uwe mkopo wa muda mfupi (at least miaka 2). Hii itakusaidia pia kufanya wise investment ya mkopo uliochukua kutokana na "intense pressure" ya marejesho kuwa ipo karibu kuliko ukichukua mkopo wa muda mrefu sana unakua "reluctant" sana kuhusu marejesho and most of the time kutokuwa huko under pressure kunaweza kukufanya ufanye unwise investment or mis-allocation of loan hivyo majuto wakati wote wa marejesho.
 
Mkuu vp top up na kusubiri hadi mkopo wote uishe? Ipi bora?
 
Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
636
1,000
Yaelekea wengi humu hawajui hata mambo ya mikopo inaendaje.

Unapokopa mf 10 000 000 na banki ikakwambia itakukopesha kwa riba ya 21% maana yake fedha hiyo utairudisha 12 100 000 kama mkopo utakuwa ni wa mwaka mmoja basi utagawanya kwa miezi 12 hivyo kwa kila mwezi utatakiwa kulipa 1 008 333.
Angalia form yako ya mkopo, kuna vitu viwili PRINCIPAL & INTEREST. Sasa kwenye hilo rejesho unalosema wewe la 1008333 kila mwezi kuna kiasi kinalipa principal na kiasi kingine interest. Kwa miezi ya mwanzoni mwa mkopo kiasi kinacholipa interest ni kikubwa kuliko kinachopelekwa kwenye interest hasa mkopo ukiwa wa miaka mingi
 
Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
11,588
2,000
Angalia form yako ya mkopo, kuna vitu viwili PRINCIPAL & INTEREST. Sasa kwenye hilo rejesho unalosema wewe la 1008333 kila mwezi kuna kiasi kinalipa principal na kiasi kingine interest. Kwa miezi ya mwanzoni mwa mkopo kiasi kinacholipa interest ni kikubwa kuliko kinachopelekwa kwenye interest hasa mkopo ukiwa wa miaka mingi
mikopo mizuri ni ile mifupi mifupi not exceeding 2 years sasa unapokopa mkopo wa muda mrefu huku wafanyakazi wa benki wakihitaji mishahara kila mwezi unadhani hapo wangefanyaje ? ndio maana unaweza kukopa kwa muda mrefu amount ya kulipa ikawa ni ndogo sana monthly lakini ukaweza kulipa pengine mara mbili ya fedha ulizokopa
 
Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
5,066
2,000
mikopo mizuri ni ile mifupi mifupi not exceeding 2 years sasa unapokopa mkopo wa muda mrefu huku wafanyakazi wa benki wakihitaji mishahara kila mwezi unadhani hapo wangefanyaje ? ndio maana unaweza kukopa kwa muda mrefu amount ya kulipa ikawa ni ndogo sana monthly lakini ukaweza kulipa pengine mara mbili ya fedha ulizokopa
Twende Kwenye kiini Cha mada.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom