Wataalam nisaidieni: Umeme wa three phase vs umeme wa single phase

Dijovisonjn

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
466
125
Toka zamani tumekuwa tukiona umeme wa majumbani ukifungwa single phase na viwandani ukifungwa wa three phase. Lakini siku hizi hata majumbani watu wanafunga umeme wa three phase tofauti na zamani.

Naomba kufahamu tofauti ya matumizi ya huu nyumbani, na umeme wa three phase unaongeza nini katika nyumba ambacho single phase haina?!
 
Three phase hutumika kama matumizi makubwa ya umeme. Kwa hiyo katika zile live wires (yaani L1, L2, L3) zinagawana usambazaji wa umeme.

Hivyo kama una mashine za kufulia, viyoyozi, majiko ya umeme inamaanisha kuwa kila phase itapeleka umeme kwenye vifaa husika. Njia hii ni tofauti na inavyotumika katika kuendesha motor za mashine kwa sababu motor zinatumia phase zote tatu kuiendesha motor.
 
Ahsante sana. Kwa hiyo nini tofauti sasa ya kufunga three phase au single phase kwa matumizi ya vifaa hvyo?!
 
Endapo utafunga single phase kwenye mashine inayohitaji three phase basi mashine hiyo haitaweza kuwaka au kufanya kazi. Au kama utafunga kwenye nyumba ambayo inahitaji three phase baadhi ya vifaa havitaweza kufanya kazi, kwa mfano nyumba za ghorofa na baadhi ya nyumba zinahitaji umeme wa three phase kutokana na kuwa na vifaa nilivyovitaja hapo awali.
 
Je, kuna athari yoyote kufunga umeme wa three phase kwenye nyumba yenye vifaa vya single phase pekee?
 
Ikiwa unavifaa vingi ndani mwako yafaa kuwa na 3 phase. Kwasababu ukiwa na single phase meter itazidiwa mwisho kuungua sababu utakua na vitu vingi.
 
Endapo utafunga single phase kwenye mashine inayohitaji three phase basi mashine hiyo haitaweza kuwaka au kufanya kazi. Au kama utafunga kwenye nyumba ambayo inahitaji three phase baadhi ya vifaa havitaweza kufanya kazi, kwa mfano nyumba za ghorofa na baadhi ya nyumba zinahitaji umeme wa three phase kutokana na kuwa na vifaa nilivyovitaja hapo awali.
Kwahiyo ukijenga ghorofa lazima uweke 3 phase? Kuna mwingine anajenga nyumba ya chini ina vyumba 6,sebule 2 etc Mwingine ghorofa lakini ina vyumba vinne tu na sitting room 1.
 
Mtoa mada, huwa ipo hivi.
Kuna kitu kinaitwa Current ambapo unit yake ni Ampere. Na kuna kitu kinaitwa Power ambapo unit yake ni watts.

Sasa, Kwa hapa Tanzania kama load yako( kwa kiswahili kisicho rasmi sana ni kama tuseme uwezo wa vifaa vyako vyote vya kutumia umeme) haitazidi Ampere 60, (13,200 watts)wewe utabakia kuwa ni mteja wa single phase. Lea lugha nyi

Ikiwa load yako itazidi Amperes 60 Basi hapo moja kwa moja utakuwa ni mteja wa three phase. Kwa lugha nyingine ni idadi ya watts katika vifaa vyako vyote kama itazidi watts 13,200 wewe utakuwa ni mteja wa three phase.

Sasa hizo watts unazipataje? Katika kila kifaa cha umeme kina ratings zake. Lea mfano kwenye bulb utakuwa imeandikwa labda 9 W maana yake ni watts 9.

Sasa chukulia labda una pasi, feni, radio, TV, friji, birika la umeme, n.k kila kimoja hapo utajumlisha ili upate total load yako ujue ni kiasi gani.

Kwa summary tu, kama idadi ya watts kwa vifaa vyako vyote haitazidi watts 13,200 wewe utabakia kuwa ni mteja wa single phase.

Idadi ya watts kwa vifaa vyako vyote ikizidi watts 13200 wewe ni mteja wa three phase.

Nawasilisha.
 
Kwahiyo ukijenga ghorofa lazima uweke 3 phase? Kuna mwingine anajenga nyumba ya chini ina vyumba 6,sebule 2 etc Mwingine ghorofa lakini ina vyumba vinne tu na sitting room 1.
Ghorofa ni mfano au assumption tu, nyumba inaweza kuwa ndogo na ikawa na appliances nyingi hivyo ikahitaji umeme wa three phase
 
Je, kuna athari yoyote kufunga umeme wa three phase kwenye nyumba yenye vifaa vya single phase pekee?
Three phase ni mjumuisho wa Single phase lines tatu, hivyo mtumiaji anakua na uhuru mkubwa wa kutumia hizo single phase anavyotaka.
Kwa details zaidi angalia mchoro huo hapo chini utaona 240V zimetokea mara tatu.
(Line -Neutral)= Single phase

images.jpg
 
Endapo utafunga single phase kwenye mashine inayohitaji three phase basi mashine hiyo haitaweza kuwaka au kufanya kazi. Au kama utafunga kwenye nyumba ambayo inahitaji three phase baadhi ya vifaa havitaweza kufanya kazi, kwa mfano nyumba za ghorofa na baadhi ya nyumba zinahitaji umeme wa three phase kutokana na kuwa na vifaa nilivyovitaja hapo awali.
Mkuu mbona kama maelezo yako yana walakini, kwa hiyo gorofa linahitaji 3 phase?

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom