Wataalam: Mababu wanaongezeka wajukuu wanapungua kupita kiasi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,550
44,700
WATAFITI duniani hivi sasa wana hoja ya kitaalamu kwamba, idadi ya watoto wanaozaliwa, imepungua duniani kote kwa kiwango kikubwa na kinyume chake wazee wanaongezeka kwa kiwango kikubwa.

Kada hiyo ya umri inaelezwa idadi yao inapungua duniani. PICHA ZOTE: MTANDAO.

Imebainika kwamba, idadi ya watoto wanaozaliwa imeshuka na wengine wanatoweka kutokana na mimba kuharibika, jambo ambalo linawaingiza katika mshangao wasomi.

Takwimu hadi sasa inaonyesha kwamba, sehemu kubwa ya jamii duniani imetawaliwa na wazee wengi zaidi ya wajukuu, uwiano ambao hauko sahihi.

Utafiti uliochapishwa na jarida la Lancet, ambalo ni maarufu kwa ajili ya taarifa za kitabibu, inayoshughulika mwenendo wa kitabibu wa nchi duniani, ikifuatilia kilichokuwepo katika mwaka 1950 mpaka 2017.

Wastani wa kitakwimu unaonyesha kwamba, hapo zamani katika mwaka 1950, kila mwanake alikuwa na takribani watoto watano na hadi kufika mwaka jana, wastani huo umeshuka hadi watoto wawili.

Hata hivyo, tofauti hiyo inaelezwa inatofautiana kati ya nchi moja na nyingine. Mathalan, kiwango cha watoto wanaozaliwa nchini Niger ni saba kwa kila mwanamke, huku wanaozaliwa ukanda wa Mediterranean, wako katika wastani wa mtoto mmoja kwa kila mama.

Mabadiliko hayo ya kupungua idadi ya watoto wanaozaliwa, yanaathiri hadi idadi ya watu waliopo duniani kwa sasa na siku zijazo.
Takwimu ya watoto wanaoharibika pamoja na vifo vya watoto wachanga vimeongezeka.

Profesa Christopher Murray, Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Tathmini cha jijini Washington, Marekani, anasema: "Tumefikia mahali nusu ya mataifa yana upungufu wa watoto wanaozaliwa dhidi ya waliopo".

Hoja yake ni kwamba, iwapo hakuna hatua itakayochukuliwa, basi idadi ya watu itapungua katika hayo mataifa, akiongeza amebakiwa na mshangao katika mabadiliko hayo
.
"Idadi ya watoto wanaozaliwa imepungua nusu ya mataifa yote duniani, kiwango hicho ni kikubwa na kinastaajabisha," Profesa Murray anaeleza.

Anazitaja nchi zilizopiga hatua kiuchumi, zinajumuisha za bara za Ulaya, Marekani, Korea Kusini na Australia, zikiwa na kiwango kidogo cha watoto wanaozaliwa, ingawaje haimaanishi idadi ya wakazi wake imepungua.

Kwa sasa inaelezwa, idadi ya watu imechanganyika katika sura pana ya mtazamo wa wanaozaliwa, kufa pamoja na wahamiaji, ambayo inachangia mabadiliko katika idadi ya watu wanaozaliwa na kufa.

Profesa Murray anasema, ni hali inayofikisha dunia katika hatua kwamba wakazi wake wanaanza kuathirika kwa kupungua idadi ya watu.

Mtaaluma huyo anasema, hivi sasa kinamama katika nusu ya mataifa duniani wanazaa watoto wanaotosha kulingana na kiwango cha uchumi wao, lakini kadri kunavyokuwepo mabadiliko ya uchumi wa dunia unavyoongezeka, wastani wa idadi ya wanaozaliwa inashuka kukidhi matakwa ya uchumi huo.

Nini sababu?

Kupungua kiwango cha watoto wanaozaliwa, wataalamu wanasema kunachangiwa na mambo makuu kadhaa ambayo ni: Idadi ndogo ya watoto wanaokufa; wanawake kujifungua watoto wachache; upatikanaji wa dawa za uzazi wa mpango; wanawake zaidi kuwa na elimu na kazi.

Pasipokuwapo kasi kubwa ya nyendo za Uhamiaji kati ya nchi moja na nyingine, inaelezwa wataalamu hao kuwa mataifa yatahangaika sana na suala la umri na kupungua kwa kiwango cha watu.

Dk. George Leeson, Mkurugenzi katika Taasisi ya Idadi na Umri wa Watu, katika Chuo Kikuu cha Oxford, nchini Uingereza, ana maoni ya kitaalamu kwamba, hakuna ubaya kutokana na ongezeko la wastani wa idadi watu, ili mradi hawaathiriki nayo kwa kiasi kikubwa.

Anasema, kiwango na idadi ya watu inategemea maisha ya kila mmoja. Kwa kuangalia hali ya maisha mitaani, kwenye makazi na foleni za barabarani, matumizi yao yanategemea kiwango cha watu kilichopo.

Dk. Leeson anasema, kila kitu ambacho jamii inapanga duniani, inategemea kiwango cha watu kilichopo, vilevile umri wao.

Mtaalamu huyo anasema kwamba, maeneo yao ya kazi yanaweza kubadilika na hata masharti ikiwemo hata umri wa juu wa ajira, kulingana na mazingira ya kuchumi, yakioanishwa na mahitaji ya jamii

Maoni ya kitaalamu kutoka kwa mtaaluma huyo, yakioaniswa na mahitaji ya nchi, yanasema katika nchi ambazo zimeathirika, zitahitajika kuongeza idadi ya wahamiaji.

Pia, anasema nchi hizo zitahitaji sera mpya za kuwahamasisha wanawake kuzaa watoto zaidi, jambo ambalo limekuwa tatizo kwa jamii.

Murray anaeleza ripoti ilivyo ni kwamba, katika kipindi kijacho kunatarajiwa kuwapo mustakabali mgumu kulingana na wastani tata wa watoto watakaokuwapo wachache katika siku zijazo na wengi watakaokuwapo ni wenye umri zaidi ya miaka 65.

Msomi huyo anasema, hilo linawafanya wawe katika mazingira magumu kukabiliana na mabadiliko ya idadi ya watu duniani.

Nchi ya mfano Japan, ni kwamba ina upungufu mkubwa wa idadi ya watu wanaozaliwa na katika nchi za Kaskazini mwa dunia, hazijaathirika kama ilivyo Japan, kwa sababu wanafidiwa na idadi ya wahamiaji wengi.

Wakati kuna sura moja ya jamii kuathirika, pia kuna mafanikio ya kimazingira, yenye manufaa katika jamii yetu.

Nchini China, kuna kiwango kikubwa cha ongezeko la watu tangu mwaka 1950 na ilikadiriwa kuwa na hisa kubwa katika idadi ya watu duniani.

Hivi sasa, bado wanakumbana na changamoto ya kiwango cha watu wanaozaliwa kuwa kubwa, hali inayofanya katika nchi hiyo kuwapo sera ya kila mtu kuwa na mtoto mmoja.
 
Kumbe duniani! Nilidhani Tz nilitaka kushangaa!! Maana huku ni mwendo wa kufyatua tu. Na hivi mkuu wa kaya ameunga mkono juhudi, ni full burudani
 
Yes resources lazima ziendane na idadi ya watu la si hivyo mbelen kutakuwa na vita vikubwa vya kugombea resources baina ya nchi na jamii mbali mbali
 
Back
Top Bottom