WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Nakubaliana nawe kabisa lakini hawa Wasaudi bado wako nyuma sana katika freedom of religion na katika nyanja nyingi nyinginezo. Kama marafiki zao wakubwa US na jumuiya ya kimataifa wakiamua kuwashinikiza ili nao waruhusu freedom of religion na katika nyanja nyingine basi watakuwa hawana jinsi bali kukubali shinikizo hilo na kuleta mabadiliko makubwa katika nchi hiyo na nchi nyingine za kiarabu.
BAK
Mchango wako umetulia sana.Inashangaza sana kuwa inapotokea nchi fulani wakataka kutunza utamaduni wao basi watalaaniwa kwa nguvu zote.Hapo hapo kuna nchi zinasifika sana kwa kukandamiza uhuru wa religion tena to the extreme, wale wenye kulilia freedom of religion huoni wakipiga kelele kwa nguvu ile ile.Ni kwanini kuwe na double standards?Mimi bado silalamiki kwanini SAUDIA wanachukia dini za wengine namna ile maana naamini ni ile hali ya kudumisha utamaduni wao ikiwa ni pamoja na dini yao.Nchi nyingine nazo ziheshimiwe kwa kutaka kudumisha tamaduni zao.Binafsi naheshimu kila dini na sipendi ukandamizwaji wa dini yoyote... ila napenda pia hali ya kuwa na tolerance kwa kuheshimu matakwa ya wenye nchi zao.