Waswisi ni Mabingwa wa Hospitality huku Wakiwakamua Wateja Wao Kiuchumi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waswisi ni Mabingwa wa Hospitality huku Wakiwakamua Wateja Wao Kiuchumi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Oct 27, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,543
  Likes Received: 18,175
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Inasemekana Waswiss ndio mabingwa wa hospitality katika huduma za mahoteli, ila kusema la ukweli, ubingwa huo wa hospitality unakwenda sambamba na kuwakamua kisawasawa wateja wao pasipo sababu za msingi!.

  Kabla sijaja, nilishamtuma mwenyeji wangu aniangalizie hoteli ya gharama ya wastani, ili nitakaporejea nyumbani angalau niweze kununua japo kimfuko kidogo cha chokolate za Uswisi (ndio wanaoongoza kwa kutengeneza Chokolate Duniani, huko hawana Cacao hata moja!).

  Mwenyeji wangu akanitajia kiwango nikaona poa nikampa go ahead anibukie. Siku nafika, nakuta bei imepandishwa kwa asilimia mia (mara mbili)!. Nikataka kugoma kuwa bei niliyopewa sio hiyo, ndipo nikaelezwa, hizi ni bei za mkutano, eti kwa vile kulikuwa na mkutano mkubwa hapo Geneva, kwa hiyo hoteli zote zimajaa, kitendo cha kureserve chumba kwa bei za kawaida kunawapotezea fursa za kutengeneza faida maradufu!.Hivyo unakuwa huna jinsi, wala hili na lile, ni kulipa tuu!.

  Wakasisitiza kutokana na wingi wa watu, ukilipia hoteli, unakuwa umelipia na usafiri wa public transport hivyo unasafiri bure!

  Ndipo nikagundua kumbe hospitality ya wenzetu Waswisi, wako makini zaidi katika sio tuu, kukuhudumia ipasavyo, bali pia kuvuna mapesa kadri wawezavyo, na haswa kunapotokea firsa za mikutano, tena wajameni, ile mikutano ya kimataifa inayofanyikaga Geneva, inafanyika Geneva miaka nenda miaka rudi ili kuendeleza mavuno hayo!, haihamishiwi pengine popote!.

  Hivi wenzetu hawa, walipokuja nchini kwetu kwenye ile mikutano ya Sullivan na World Economic Forum, sisi pia tulitumia fursa za mikutano hiyo kuwakamua?. Kule Arusha nilishuhudia jinsi wakinamama wajasilia mali walivyolizwa!.

  Swali, hivi ofisi zetu za kibalozi, zilizotapakaa sehemu mbalimbali, pia wanafanya inteligensia ya kiuchumi ili tuige mazuri ya maendeleo ya wenzetu, au maofisa wetu kazi yao ni kuissue viza na balozi kumpokea mkuu?!.

  Pasco,
  Geneva.
   
 2. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  wenye hiyo funny wanakuja subiri nadhani bado wamelala..
   
Loading...