Waswahili walisema "usiige kunya kwa tembo!" Kinachonikuta Sasa!

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,213
56,849
Si ulishasikia ile kauli ya jino kwa jino..? Sasa nikajaribu kuifata! Kumbe sikujua mwenzangu anameno mimi namapengo!

Aliponiblock nami si tu ya kwamba nikamblock bali nilimubuloku!.. haikuisha hapo aliacha kunitafuta nami si tu nikaacha kumtafuta bali nilimfuta kabisa!.. mambo ya jino kwa jino hayo!

Nae wala hakuisha visanga akafanya kimbwanga nami nikafanya tena huku nikijipa moyo kwani yeye nani?

Sahivi nimeshajua yeye ni nani na Mimi ni nani!.. yeye ni nyonga mkalia ini wangu nami ni komamanga tu!! Hii jino kwa jino sahivi inanitesa! Kumbe nilisahau nilikuwa na mapengo 😭

Mkimuona mwambieni moyo wangu unamfikiria yeye!, yeye ndo kimwana cha jahazi kilichobeba ukopakopa wote unaonisibu!..
Waswahili si kila kitu mtu atakachokikoroga anatakiwa anywe mengine tunayaoga kabisa! Kama ni dimbwi Basi nilitumbukia dubwiii.. sahivi nahangaika na mapengo yangu! Kweli kiberenge ni kiberenge tu..😭
 
Ni bora usepe mazima ukirudi utakufa nakwambia. You meant nothing in her life ...
 
Unafikiri ipo hivyo! Tatizo she's waving..
Unajipa moyo. Yani kila anayeachwa au kupuuziwa uwa anapenda kujipa moyo oh no body will treat her like I do... Oh atanikumbuka nimemtndea mengi ... Oh anajifanya tu ila ananiwaza.
Kumbe mwenzako ashasahau anakumbuka tu lako jina.
Just move on mtu kama anakupenda hawezi vumilia hata siku 3.
 
Mkuu yaelekea yalishakukuta mengi..😂
Hawa ndo watu wenye experience..
 
Mkuu yaelekea yalishakukuta mengi..😂
Hawa ndo watu wenye experience..
Nyani mzee nimeshakwepa mishale yakutosha mpaka nakaribia kufika msitu wa ahadi wenye matunda na misosi ya kila aina kama katikati ya msitu wa congo ambapo hakuna binadamu wa zama zetu amewahi fika.
 
Nyani mzee nimeshakwepa mishale yakutosha mpaka nakaribia kufika msitu wa ahadi wenye matunda na misosi ya kila aina kama katikati ya msitu wa congo ambapo hakuna binadamu wa zama zetu amewahi fika.
Pole sana
 
Aisee nilisahau kama niliahidi kutolitamka tena hilo jina.

Je itakua poa nikikuita komamanga?
Vyovyote utakavyoita ila usisahau kujiita wewe mwenyewe Mrs komamanga au Mrs huyohuyo..😅
 
Back
Top Bottom