Wastarabu wengi wanapatikana mikoa hii Tanzania

Mtwara
Lindi
Tanga
Kigoma
Kilimanjaro-upareni.
Mikoa yote ya Zanzibar
Tabora
Morogoro
Pwani
Dodoma-kondoa

NB: ustarabu kote upo ila hiyo mikoa level yao iko juu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, kwa mujibu wa "Swahili Oxford Living Dictionaries", Ustaarabu ni "Hali ya mtu kuwa na vitendo, tabia namwenendo unaolingana na maadili ya jamii inayohusika". Kwa bandiko hili unataka kusemaje? Ni ustaarabu gani unaoongelea? Kilangila.
 
huyu jamaa hujamuelewa vizuri...! Alivyo fala kataja yale maeneo yenye waislamu wengi, kuwa ndipo kuna ustaarabu.... ni wa kumpuuza tu
 
Wema hauna kwao na ubaya hauna kwao. Ustaarabu sio registered trade mark ya watu fulani. Mtu yeyote anaweza kuamua kuwa mstaarabu au kinyume chake ingawa mazingira nayo huweza changia
Nimeishi Znz nimesoma kule, nimemsoma mtu kama Ghassani na kwa kweli ukiisoma historia ya kule na mambo waliofanyiana hata chakula huwezi kula.
Watu unaweza kuwakuta ustaarabu kwenye jambo hili ukawakuta washenzi kwenye jambo lingine. Kwa mfano nilienda wakati fulani Chake Chake Pemba pale nikaenda sehemu kunywa Kahawa wakati huo adhana ikawa inaita yule Muuzaji wa Kahawa akanambia kunywa ukimaliza weka pesa mezani uende zako. Si hivyo siku nyingine nilikuwa kwenye daladala Wete nikashuhudia kuna mtu kaja kwenye lile daladala akauliza nani anaenda Chakechake kuna jamaa wakajibu akamteua mmoja akamkabidhi laki akamwambia akifika pale Chakechake Nmb amuulizie mtu anaitwa Amir amkabidhi. Matukio hayo mawili yalinipiga bumbuwazi juu ya uaminifu wa watu wale, hata hivyo mwenyeji wangu alivyonihadithia kuhusu mambo yao mengine meusi ya usiku nilijisikia vibaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo meusi ndo ninayo yasubiri niyajuwe.

]Kupata hakuna kudogo
 
Write your reply...
nafikiri wagogo ndo wa mwisho kwa ustaarabu,kama unabisha weka kwako mpangaji mgogo,au jaribu kupita pale machinjioni vingunguti


waha nao kwa ustaarabu,sifuri kabisa
Waha nimeishi nao ni wastaarab sema wanajiharibia kwa ubishi wa kijinga tu.

]Kupata hakuna kudogo
 
Uzi wako Una dhamira iliyojificha.mikoa yenye wastaarabu, zanzibar mikoa yote,kilimanjaro_upareni,dodoma_kondoa.duh.jf huezi leta ujinga ukabaki salama.hapa ndipo nakubaliana na Jay z aliposema "dini zimeletwa ili tubaguane".
 
Labda ustaarabu wa kufuga ndevu na kuvaa vipedo

Miji kama Iringa na Moshi, ambayo ilitajwa kuongoza kwa usafi Tanzania hujaitaja.
Umetaja eti sijui Lindi, Tanga, sehemu ambazo hadi karne hii Serikali inawalazimisha wajenge vyoo la sivyo watawatoza faini ama watawafunga..

Nyie watwana wa kiarabu bana
Haha ha haa --- ustaarabu ni mfumo unaogosa Mazingira yote au mfumo wote wa maisha "...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipoona kigoma nimecheka sana aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
Haha " Mpaka kigoma nadhani mtoa mada anadhani neno Ustaarabu lina bebwa na neno ukarimu pekee " yaani kama akienda sehemu akakaribishwa vizuri tu halafu akapatiwa malazi au chakula basi kwake huo unakuwa tayari ni ustaarabu "

Kustaarabika ni mfumo Unaochukua maisha yote ya mwandamu " mfumo huo huwa unaanzia kwenye elimu .. kwa sababu ukishaelimika utakuwa unaishi katika ustaarabu ''

Utatambua umuhimu wa kuvaa mavazi nadhifu yanayo kutofautisha na wahuni " utakuwa na maneno yenye busara " utaitumia taaluma yako vyema ' na kuihudumia jamii ili iweze kutoka kwenye changamoto iliyonazo," utautambua umuhimu wa afya " hauwezi kuacha kunawa mikono ukiwa umetoka toilet au ukiwa umeshika kitu kichafu " utawaheshimu watu wote bila ya kujali dini rangi na makabila yao "utakuwa ni muumini wa haki na usawa ", Jamii ambayo inaishi katika mazingira hatarishi na haba ki huduma hiyo haipaswi kuonekana kuwa ni jamii ya watu waliostaarabika ", kwa sababu neno ustaarabu ndio mzizi wa elimu " endapo Jamii hiyo ikielimishwa basi ni wazi kwamba ndio watakuwa ndani ya ustaarabu. Na kuanza kuishi kistaarabu "

Mtoa mada anapaswa kufahamu kwamba ustaarabu umebeba maana pana haswaa"... hauwezi kutofautisha ustaarabu na Elimu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom