Wastaafu walipwe pensheni yote kwa mkupuo ndani ya mwaka mmoja baada ya kustaafu

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,856
2,000
Kile wafanyakazi wanachochangia kwenye hiyo mifuko huwa kinawekezwa na kuzalisha kingi zaidi kwa takribani miaka 30. Huenda kungekwa na mifuko binafsi ya pensheni yenye ushindani wangelipwa kingi zaidi.
Mtoa mada unajua kwamba mafao TZ yanatolewa kama bima (kwa kutumia kikokotoo) na siyo kama akiba (ulichoweka ndicho unachopewa)? Unajua kikokotoo kinatema pesa nyingi kuliko mtu angalipewa kile tu alichochangia (hata ungijumlisha na kiasi kidogo cha riba)?

Ukisema "apewe zote" --- zipi? Michango yake (midogo kuliko jumla kuu ya kikokotoo). Dhana ya pensheni kama bima ni kitu muhimu.

Cha msingi kile kiinua-mgongo kisichelewe, na pensheni ya kila mwezi halikadhalika.

 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,856
2,000
Hiyo pensheni ya kila mwezi ichanganywe yote kwa pamoja na kiinua mgongo mstaafu alipwe kwa mkupuo.

Serikali iuze hisa kwa wafanyakazi wastaafu kwa mashirika kama NHC, bwawa la Umeme la Nyerere na mengineyo hizo pesa zao zizungushwe zizalishe zaidi badala ya kuchota tu kodi za wananchi muda wote kugawia hao wazee.
Kuna Pension ya kila mwezi na Kiinua Mgongo ambacho anapewa kwa mkupuo

Naam hio ndio maana ya pension.., kuganga njaa ili mtu huyu aliyezeeka na sasa hana nguvu kama zamani asiwe mzigo kwa jamii..., unataka afanye mambo makubwa ya maendeleo yapi ambayo hakufanya maisha yake yote...., hapa ni kulia kivulini kile alichochumia juani enzi za ujana wake

Hapana hao ndio kazi zao kuhakikisha wanakusanya pesa za wachangiaji na kuwapa wale wazee waliostaafu mpaka siku wakifa

Iwape pesa zao kwa mkupuo alafu siku zikiisha waanze kuwa omba omba mitaani ambapo jamii iingie tena mfukoni kuwalea, au unataka wawe omba omba uzeeni ?
 

Shakir

JF-Expert Member
Jul 31, 2012
1,039
2,000
Kwanini wastaafu huwa wanendelea kulipwa kila mwezi pesa kidogo kidogo baada kupewa kwa mkupuo kiasi kikubwa pindi wanapostaafu badala ya kupewa pesa zao zote ndani ya muda mfupi wa kustaafu kwao?

Hizi pesa za pensheni wanazopewa kila mwezi ni za kuganga njaa tu na huwa hawewezi kudunduliza kufanyia nazo mambo makubwa ya maendeleo pia ni kupoteza muda na kuingezea serikali mzigo usiokuwa wa lazima wa kusimamia na kufuatilia kila siku mafao ya hawa wazee wastaafu.

Ni vyema serikali ikawa inawapa pesa zao zote angalau ndani ya mwaka mmoja baada ya kustaafu ili huyo mstaafu mwenyewe akajue pa kuzipeleka ua jinsi ya kuzitumia.
Kwani Infantry Soldier anasemaje kwenye hii issue?
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,338
2,000
Hiyo pensheni ya kila mwezi ichanganywe yote kwa pamoja na kiinua mgongo mstaafu alipwe kwa mkupuo.
Akilipwa kwa mkupuo akizila zote na kuwa omba omba uzeeni ni mzigo kwa jamii
Serikali iuze hisa kwa wafanyakazi wastaafu kwa mashirika kama NHC, bwawa la Umeme la Nyerere na mengineyo hizo pesa zao zizungushwe zizalishe zaidi badala ya kuchota tu kodi za wananchi muda wote kugawia hao wazee.
Pension funds ndio inachokifanya theoretically..., inachukua pesa za wachangiaji (sio kodi) mwajiriwa anakatwa na mwajiri anamuongezea mwajiriwa na pesa kupelekwa kwenye pension funds ambazo inazizungusha ili mfuko usifilisike..., kwahio practically wanaowaweka wazee mjini ni wachangiaji wa sasa..., tatizo kama hili ndio liliwapata Japan kutokana na kwamba wazee ni wengi hence wachangiaji wanapungua kuliko wachangiwaji (old people population increasing)
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,686
2,000
Wakishapewa hizo hela waje mtaani tuwafundishe siri ya utajiri iliyopo kwenye forexi na biashara za kimtandao kama Q-neti ili tuwe na wastaafu wengi mabilionea🤣🤸🐒
Munazisubiri kuzifanyia utapeli, na hayo ndiyo yanayowafika wazee wengi huku kwetu, hasa kwa vile hawajawahi kupata fedha nyingi kwa mkupuo kwa hivyo zinawachanganya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom