Mung Chris
JF-Expert Member
- Sep 12, 2017
- 3,367
- 3,778
Niwasaidie tu wanao tegemea kustaafu kuanzia mwezi huu wa 9 na kuendelea, natumai ma tamko ya Mawaziri na Marais wawili aliyepita na aliyeko madarakani mlisikia kabisa wakisema na kusisitiza watu walipwe mapema akiwemo Waziri ambaye ni mbunge wa Jimbo la Peramiho. Hakuna utekelezwaji hadi leo hii mnavyo sikia OMBI LANGU KWENU NI KWAMBA:
Mjipange muwe na akiba ya pesa ya kula na kutumia kama miezi 12 hivi kwa kusubiria pensheni na mafao. Mkicheza, mkifanya yenu, mtatafuta pa kukimbilia kumbukeni kwa sasa hamuwezi kulelewa na wazazi wenu tena na wao kuwalisha na familia zenu. Wenzenu tumesota haswa haswa. Hakuna cha mafao wala pensheni, wao PSSSF wanategemea eti kulipa malimbikizo ya pensheni siku watakulipa mafao sasa waulize ni lini hata wao hawajui.
Kaeni vizuri nawasaidia mtakuja kunishukuuru badae na ka zawadi mtanipa. Mimi ni muhanga wa hili najua maumivu ya mtu mwenye familia kukaa bila bila aibu mpaka kwenye familia na ndugu.
Jiulize kwanini hawaleti vipindi kwenye TV kama NSSF ili watoe na wajinadi watu wawe na maswali kwao. kuna maswali hawataki kusikia