Wastaafu wa Polisi na wajeshi ni mafukara/maskini wa kutupa: Ndo maana kuna wezi wengi ktk majeshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wastaafu wa Polisi na wajeshi ni mafukara/maskini wa kutupa: Ndo maana kuna wezi wengi ktk majeshi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mabadilikosasa, Jun 8, 2011.

 1. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani kati ya wafanyakazi wanaostafuu na kuwa na maisha ya kifukara na ombaomba ni wanajeshi na polisi. Usimwone kagonja anavimbisha mashavu, na anaongea kwa kukejeli wapinzani waofanya kazi ya kuleta maisha bora, akistaafu ndo wale wanaopita maofisini kuomba msaada wa matibabu na chakula. Ndo maana kina mahita waliiba sana jeshi la polisi wakajenga magorofa. Majeshi yetu yamejaa tuu wezi watupu. Jamaa mmoja amestaafu juzi mwenye cheo cha major sasa analala kwenye banda la kuku na kutembelea ndala.

  hawa jamaa wajinga kweli kweli. Badala ya kusaidia wapinzani ili wawasaidie wao wanaleta kiburi then wanaisha kuwa ombaomba. wengine hata mavazi ya ziada hawana zaidi ya hizo uniform. Ndugu yangu mmoja polisi akaja ananiomba hela za kupeleka mtoto shule, anasema mshahara wake ni mdogo. Nikamwambia mbona unawapiga wapinzani mabomu wakati wanataka kuleta mabadiliko. Nikamwambia sisi wenyewe mishahara yetu imepanda maana tuligoma. akadai wale FFU wanavuta bangi, eti wakilipwa laki moja ya operation wanaua mtu. Nikasema duu, hawa jamaa, wanadanganywa tuu kwa laki moja au mbili wanakosa maisha yote??

  Jeshi na polisi ungeni mkono mabadiliko, nanyi mpate nafuu, hamuoni wanasiasa wanakula nchi, mfano wabunge?
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Polisi hawawezi kuchagua chama hili ni jeshi la wananchi na tunatakiwa kuwasaidia wafuate sheria badala ya kuwalalamikia. Ni kweli viongozi wa juu wanachukua rushwa kwasababu wanatelekezwa wakistaafu. Serikali inabidi iangalie upya hili kwani hawa jamaa inabidi waweke urafiki na mafisadi kwasababu wakistaafu wawe na vibiashara vya kuuishi.
   
Loading...