Wastaafu wa JWTZ Mkoani Kagera wataka wapewe kazi, kuliko kufanywa na watu au kampuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wastaafu wa JWTZ Mkoani Kagera wataka wapewe kazi, kuliko kufanywa na watu au kampuni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Mar 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wastaafu JWTZ wataka wapewe kazi Thursday, 17 March 2011 19:48

  ASKARI wastaafu wa JWTZ mkoani Kagera, wamemuomba Mkuu wa mkoa huo, Mohamed Babu, awaopatie kazi mbalimbali kulingana na taaluma zao, zikiwamo za ujenzi wa vyumba vya madarasa, madaraja, barabara na utengenezaji wa samani za shule, ili waweze kupata fedha za kujikimu kimaisha.
  Wastaafu, walitoa rai hiyo jana katika risala yao iliyosomwa kwa niaba yao na Kaimu Mwenyekiti wa Muungano wa wanajeshi wastaafu Tanzania (Muwawata) mkoani Kagera, Luteni Richard Kashombo, katika mkutano wa kutambulisha muungano huo.

  Pia walimwomba mkuu wa mkoa, kuwapatia shughuli zote zinazohusu usafi na kutunza mazingira, ili wazifanye na kupata vipato.Walisema kuwa nchi nyingi duniani, zimeingia katika matatizo baada ya wanajeshi wastaafu kukaa bila kazi na hatimaye kuchoshwa na hali ya maisha, tofauti na walivyokuwa wamezoea.

  Walisema ni jambo la ajabu kuona kwamba serikali bado inaendelea kuwatunza kwa kuwapatia viwango vidogo cha fedha kulingana na cheo cha kila mtu.Walisema kuwa pamoja na kwamba kiasi hicho hakitoshelezi mahitaji kulingana na hali ya maisha ya sasa, bado wanapatiwa kiasi hicho kila baada ya miezi sita, hali inayosababisha kuangaika na baadhi yao kujiingiza katika bishara ndogo ndogo kwa ili kujipatia vipato.

  Mwenyekiti wa Muungano wa Wanajeshi wastaafu Tanzania, Assedy Mayuggi, alisema kuwa serikali inapoteza nguvu kazi nyingi kutokana na kutotambua umuhimu wa wanajeshi baada ya kustaafu, ambapo huachwa na kwenda kuishi uraiani, huku wakiwa na taaluma mbalimbali.

  Mayuggi alisema kuwa katika nchi nyingine wanajeshi wanapostaafu wanawekwa kwenye jeshi la akiba, ili serikali iendelee kuwatumia katika shughuli mbalimbali za uzalishaji.

  Alisema Tanzania zipo kazi muhimu ambazo wanajeshi wanaostaafu wangekuwa wakizifanya, kuliko kufanywa na watu au kampuni binafsi.
   
 2. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni jambo jema maana kuna uwezekano mkubwa sana wa wanajeshi wastaafu kujihusisha kwenye vitendo vya uhalifu kama watakaa idle bila kazi. Ikumbukwe kwamba watu hawa wamepitia mafunzo mbalimbali ya maigano.
   
 3. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  serikali yetu haiwez kuwa makin kwa kweli mtu kaitumikia nch amelinda nchi kastaafu et akajenge nyumba au kuwa security guard kweli? hakuna njia ya kuwatunza kwa kaz yao nzuri walioifanya kwa kumlinda mkwere na serikali yake mpk wakajenge huu ni utani wanashindwa hata kuwa wanawapa posho na je kwani walishindwa kuwekeza ujanani mwao au nao hawana elim ya kujiajiri kama wahitim wa bongo wanavyoambiwa. mi nahisi serikali ina mpango wa kuibua majambazi wenye utaalam wa wa hali ya juu
   
Loading...