Wastaafu wa EAC: Mahakama ya Rufaa yamwondoa jaji Mtamwa........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,635
2,000
Mahakama ya Rufaa leo imemwondoa jaji Mtamwa kulisikiliza suala la madai ya wastaafu wa Afrika mashariki kwa kile ambacho kiliitwa ni kukosea katika maamuzi ya kukubalina na hoja za serikali katika suala hilo na hivyo kuwakatalia wastaafu hao kusikilizwa shauri lao.

Sasa shauri hilo litapangiwa jaji mwingine ambaye atalisikiliza na kulitolea uamuzi juu ya hoja za kimsingi za wastaafu hao walilipwa nini na walipunjwa nini?

Uamuzi huo ulisomwa na Jaij Mkuu Agustine Ramadhan.................Mahakama ya Rufaa inastahili pongezi kwa kuingilia kwa hiari yake yenyewe danadana zilizokuwa zinaendela hapo Mahakama kuu dhidi ya haki za wazi za wastaafu hao......................

SOURCE: ITV
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,635
2,000
Mahakama ya Rufani yatoa ahueni wazee Afrika Mashariki
Wednesday, 15 December 2010 20:29

Hussein Kauli na James Magai
JOPO la Majaji watano wa Mahakama ya Rufani likiongozwa na Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan, limetengua uamuzi wa Mahakama Kuu uliotupilia mbali na kufuta maombi ya wazee wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaodai mafao yao.
Sambamba na kutengua uamuzi huo, uliotolewa na Jaji John Utamwa Novemba 9, mwaka huu, pia jopo hilo limemuondoa Jaji Utamwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Kabla ya kutupa maombi ya wastaafu hao kupitia kwa mawakili wao, Jotham Lukwaro na Charles Semgalawe, waliwasilisha mchanganuo wa madai yao, wakieleza kuwa wanaidai serikali Sh2, 149,076,684, 275.80.
Wastaafu hao waliwasilisha maombi hayo baada ya Jaji Utamwa kuwataka wawasilishe mahakamani hapo taarifa kamili zinazohusu takwimu sahihi za fedha wanazodai wafanyakazi hao wapatao 31,700, na kiwango ambacho tayari wamelipwa na serikali.

Hata hivyo, madai hayo yalipingwa na wakili wa serikali, Gabriel Malata, kwamba sio kweli na kudai kuwa kwa mujibu wa hukumu ya makubaliano ya Mahakama Kuu ya mwaka 2005, wastaafu hao wanadai Sh117 bilioni.
Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa alikubaliana na hoja za pingamizi la serikali na kufuta kabisa maombi hayo, huku akisema hayakubaliki kwa sababu hayapo kwenye kumbukumbu za awali za kesi hiyo.
Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa alisisitiza kuwa, mahakama haiwezi kutoa hati ya malipo ya Sh2 trilioni kwa wastaafu hao kwa kuwa, madai hayo yako nje na uamuzi wa mahakama hiyo wa mwaka 2005 uliotolewa na Jaji Catherine Urio.

Jopo la majaji hao jana, likiongozwa na Jaji Ramadhan lilitengua uamuzi wa Jaji Utamwa baada ya kufanya marejeo ya uamuzi huo na kubaini kuwapo kwa kasoro za kisheria.
Kabla ya kutoa uamuzi huo, Jaji Ramadhan alitoa fursa kwa upande wa mawakali wa wastafu hao, kueleza kilio chao kutokana na uamuzi ya Jaji Utamwa na kwamba, kila upande kwenye kesi hiyo ungependa kuona inamalizika.
"Mlikuwa na malalamiko mengi kwenye magazeti, kila siku ni kilio, sasa mahakama ingependa kusikia kilio chenu ni nini ili tufikie hitimisho," alisema Jaji Ramadhan.

Baada ya kupewa fursa hiyo, Lukwaro alieleza malalamiko kuhusu uamuzi wa Jaji Utamwa, ambaye alidai alikiuka baadhi ya mambo.
Alidai alishindwa kusikiliza baadhi ya mambo ambayo upande wake uliwasilisha baada ya kukubaliana na pingamizi la awali lilitolewa na serikali.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Malata alipingana na maelezo hayo kwa madai kuwa, Jaji Utamwa alisikiliza hoja zote zilizotolewa na wastaafu hao na kuzijumuisha kwenye maamuzi.

Baada ya mjadala huo, Jaji Ramadhan alitangaza uamuzi na kutamka: "Baada ya kusikiliza pande zote mbili, hakuna ubishi kwamba Jaji Utamwa baada ya kutoa maamuzi ya pingamizi la upande wa wastaafu, angetakiwa kusikiliza madai yaliyotolewa na upande wa walalamikaji."

Jaji Ramadhan alisema Jaji Utamwa alifanya kosa na uamuzi wake umeondolewa na kesi hiyo itachukuliwa na jaji mwingine na kwamba, sababu za kufanya hivyo zitatolewa baadaye.


 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom