nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Mwandishi Wetu Raia Mwema | 21 Sep 2011 | Toleo na 204
Imejitokeza hali ya kugawa kura za Upinzani katika uchaguzi mdogo wa Igunga, kati ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), huku hali ya mambo ikiwa si shwari ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Raia Mwema ikielezwa kuwa mikakati ya hujuma imeshamiri ndani ya chama hicho.
Taarifa za ndani ya CCM zinabainisha kuwa mikakati hiyo inafadhiliwa na mmoja wa wanasiasa ndani ya chama hicho ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu na aliyepata kuwa mbunge. Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kuwa kwa sasa kuna kambi ya chama kwa upande mmoja, na kambi ya mwanasiasa huyo kwa upande mwingine.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa kuwapo kwa katibu mkuu mstaafu wa CCM, Philip Mangula, kumesaidia kuanza kuvuruga mikakati ya hujuma ambayo inatajwa kuwa ilianza kushindwa kudhibitiwa na Katibu Mkuu wa sasa, Wilson Mukama.
Mbali na Mangula, kiongozi mwingine mstaafu wa CCM ambaye amekwisha kufika na kufanya kampeni Igunga ni rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye wakati yeye akiwa Mwenyekiti, Mangula alikuwa Katibu Mkuu, na wao ndio waliokabidhi mikoba ya chama hicho kwa Mwenyekiti Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Yusuf Makamba.
"Tangu amefika Mangula, hali kidogo imeanza kuleta matumaini ndani ya chama. Kambi ya chama na ile ya huyu jamaa zimeanza kuelekeza imani kwa Mangula kwa sababu yeye hayumo kwenye kundi lolote ndani ya siasa za chama kwa sasa...si unajua huyu mzee alistaafu na kwenda kulima kijijini kwake Njombe?," kilieleza chanzo chetu cha habari ndani ya CCM, Igunga.
Mangula anatajwa kubadili masuala mbalimbali yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho akitajwa kulenga kuboresha zaidi kasi ya kampeni za chama hicho.
Mangula abomoa mkakati
Inaelezwa kuwa Mangula amebomoa mkakati wa awali wa kampeni uliokuwa umesukwa na timu ya kampeni kabla ya kuwasili kwake huko. Awali, inaelezwa kuwa vituo vya uratibu wa kampeni ya CCM vilikuwa katika ngazi ya tarafa, lakini Mangula amebadili na kuviweka katika ngazi ya kata.
"Ametueleza kuwa kwenye tarafa si mahali muafaka kwa sababu unakuwa mbali na watu, kwa hiyo tumesogea sasa tuko kwenye kata. Mashambulizi ni katika kata. Nguvu kubwa sasa inabaki kwenye kata," kinaeleza chanzo chetu cha habari.
Mbali na uamuzi huo, inaelezwa kuwa nidhamu imeanza kurejea kati ya makundi yaliyokuwa yakihasimiana, kwa sababu Mangula anatajwa kuwa na uwezo wa kumkaripia yeyote katika makundi hayo.
"Kuna watu mwanzo walionekana hawakosei mbele ya Katibu Mkuu Mukama, lakini Mangula amekuwa mkweli, anakosoa na kumkaripia yeyote anapokosea. Kuna watu walikuwa wanawasilisha ripoti za hovyo na Mukama alikuwa akizikubali, lakini wengine wenye ripoti zenye ukweli walipuuzwa si kwa kigezo cha ubora wa ripoti zao bali masuala mengine binafsi.
"Kwa hiyo, Mzee Mangula ameleta nidhamu. Kuna watu wamekuwa wakirudishwa na ripoti zao za ubabaishaji....inawezekana walikuwa wanatumika kufanya hujuma. Huyu Mangula amekuwa na uwezo mkubwa wa kuchambua ripoti, na kama umefanya ubabaishaji au kupachika uongo atakung'amua."
CCM na kampeni za kuvizia
Inaelezwa kuwa mgawanyo wa majukumu ya kampeni sasa umebadilika. Wakati wengine wakifanya kampeni za jukwaani, makada wengine wa chama hicho watakuwa wakifanya siasa za kufuata makundi ya watu, kama wazee, wanawake na vijana.
Taarifa za ndani ya CCM zinaeleza kuwa Mangula ndiye mwenye jukumu la kukabiliana na makundi ya wazee na anatarajiwa kuongezewa nguvu na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro sasa mstaafu, Stephen Masishanga, anayetajwa kuwa na heshima kubwa kwa watu wa kabila la Wasukuma, wilayani Igunga.
Katika orodha hiyo, wamo pia baadhi ya wakuu wa wilaya wastaafu wa Igunga, wanaotajwa kuwa na nguvu ya ushawishi wilayani humo, ambao pia jukumu lao litakuwa ni kampeni za chini kwa chini na si za jukwaani.
Miongoni mwao ni pamoja na aliyepata kuwa DC wa Igunga, Andrew Masanje, ambaye pia amewahi kuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM, na DC mwingine wa zamani wa Igunga, Deogratius Mtambalike.
Viongozi hao wanatajwa kama wanaokubalika na wazee wa Igunga, kwa sababu wakati wa uongozi wao kama wakuu wa wilaya walikuwa karibu mno na jamii hiyo ya wana-Igunga.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa tayari Mangula amefanikiwa kubadili misimamo ya baadhi ya koo za kikabila, ukiwamo ule wa Wataturu, wanaotajwa kuwa awali walishawashiwa na wakajiunga na CHADEMA.
Taarifa zinaeleza kuwa ujio wa Mangula Igunga ni kama umeanika udhaifu wa Mukama. Sasa Mukama anazungumzwa na wana-CCM wanaoshiriki kampeni za Igunga kama kiongozi aliyekuwa hayapi uzito unaostahili masuala mazito yaliyokuwa yakijitokeza wakati wa kampeni.
"Wengi hawakuridhishwa na Mukama, wanasema alikuwa anachukulia mambo kirahisi mno, hakuwa makini. Alikuwa akipuuza taarifa nyingine nyeti.
Mikakati ya hujuma ndani ya CCM
Hata hivyo, inaelezwa kuwa ingawa CCM imekuwa na timu maalumu ya kampeni ya wanachama wake kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwamo Dar es Salaam, wapo baadhi ya wanachama, hasa vijana, wenye makazi Dar es Salaam na maeneo mengine nje ya Igunga, ambao wako Igunga kwa ufadhili maalumu.
Inadaiwa kuwa baadhi yao ni vijana ambao kuwapo kwao mjini Igunga, hakuna uhusiano wa moja kwa moja na chama na badala yake wamekuwa wakigharimiwa nje ya chama.
Inaelezwa kuwa kundi hilo linafadhiliwa liendelee kuwapo hapo kwa ajili ya kuratibu mikakati ya hujuma, ambayo ni pamoja na kushambulia au kuzomea baadhi ya viongozi wa chama hicho wasio na maslahi nao.
Hata hivyo, mipango hiyo imekuwa ikifanyika kwa siri kubwa, ingawa taarifa za ndani ya CCM zinaeleza kuwa wahusika wamekwisha kubainika na tayari wamekwisha kumhujumu mmoja wa viongozi wa kampeni hizo, kwa kumtengenezea tukio la kumdhalilisha, akidaiwa ‘kutembea' na mke wa mwanachama mwenzake.
Mgawo wa kura CUF, CHADEMA
Chama cha Wananchi (CUF) ambacho katika Uchaguzi Mkuu uliopita kilishinda nafasi ya pili kwa kupata kura 11,000 za ubunge, kwa mgombea wake, Leopard Mahona, kimekuwa kikikituhumu CHADEMA, kukihujumu kwa kulenga kugawa kura za upinzani.
Kwa mujibu wa CUF, CHADEMA ilipaswa kuiunga mkono kwa kuwa tayari CUF ina mtaji wa kura 11,000 za mwaka jana. Hata hivyo, CHADEMA kwa upande wake imekuwa ikiishambulia CUF kwa kudai ni CCM-B, na hivyo ina utata kuwapo katika kambi ya upinzani.
Mvutano kama huo umewahi kujitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana katika uchaguzi wa ubunge, Jimbo la Tarime, ambako mgombea wa CCM, Nyambari Chacha Nyangwine alishinda dhidi ya mgombea wa CHADEMA, Mwita Mwikabe na yule wa CUF, Charles Mwera.
CHADEMA yajizatiti kuweka mtandao
Kwa upande mwingine, taarifa kutoka ndani ya CHADEMA zinaeleza kuwa chama hicho kimejipanga ngazi ya kata ambako kila kata kumewekwa timu maalumu.
Timu hiyo katika kila kata inatajwa kuhusisha mbunge, vijana wanne kutoka vyuo vikuu na ofisa mmoja kutoka makao makuu ya chama hicho, ambao ndio wamekuwa waratibu wa ujio wa mgombea ubunge wao, Joseph Kashindye, kila anapofika huko kwa ajili ya mikutano ya hadhara.
Hata hivyo, pamoja na mkakati huo bado inaelezwa kuwa CUF imekuwa na nguvu kubwa katika baadhi ya maeneo kuliko CHADEMA ambayo pia katika baadhi ya maeneo imefanikiwa kuyadhibiti na ikitarajiwa yanaweza kuendelea kubaki kuwa ngome yake hadi wakati wa upigaji kura, Oktoba 2, mwaka huu.
Uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, unafanyika baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Rostam Aziz, kujiuzulu baada ya kutakiwa "ajivue gamba" ndani ya chama hicho kwa kujiuzulu nyadhifa zake za kisiasa, naye akajivua zote hadi ubunge.
- Mangula aongezewa RC Masishanga, ma- DC wastaafu
- CHADEMA, CUF sasa waonekana watagawa kura za ushindi