falcon mombasa
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 9,186
- 9,288
Wastaafu wengi mitaani na sehem mbali mbali za tanzania wamekuwa na vilio vyao vya kutolipwa mafao yao na mifuko ya hifadhi ya jamii, suala hili limekuwa likijirudia rudia mara kwa mara .hivi hawa wanaosoma huko vyuoni mnategemea watakuja kufanya kazi serikali na wakawa waaminifu?ilhali wanajua kabisa wakija kustaafu hawatalipwa mafao yao. Sasa wiki jana nilipost taarifa juu ya baadhi ya wastaafu mkoa wa dar kuandamana kwa amani kuelekea ofisi ya waziri mkuu kudai madai yao,tayari weekend iliyopita wazee hawa waliotumikia taifa lao wameanza kupokea vitisho endapo wataandamana.inasikitisha sana.nafikiri pia iko siku moja kila mtu ataitwa mzee na utajisikiaje ikiwa utapuuzwa na jamii hata katika haki yako.sasa kwa upendo kabisa tunaomba serikali ikae na hii mifuko ya hifadhi za jamii kisha waangalie ni namna gani wastaafu waliotumikia taifa lao kwa upendo watalipwa. My take yawezekana huu ni mpango wa watu wachache either kwenye chama au serikali