Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,897
- 1,334
Wastaafu Kufuata Huduma ya NHIF Dodoma Sasa Limekwisha
"Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita Aliandika Barua Kwenda Wizara Ya Afya Kuomba Wazee "Wanatakiwa Wasije Hapa Dodoma Ama Kwenda Ofisi Za Mikoa Kwenda Kuhudumiwa Kule Na, Tumeiona Barua Yako na Mimi Nikwambie Sasa Wale Wazee wastaafu Wa Kiteto Wakusanye Na Wataalam Watawafuata Huko Kiteto Na Itakuwa Hivyo Kwa Wabunge Wote Sasa Watu Watashuka Kuwafuata Kule Waliko" Naibu Waziri Wa Afya Dkt. Godwin Mollel.
Mbunge Wa Jimbo La Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita Aliuliza Swali Februari 7, 2025, Kupitia Wizara Ya Afya Kuhusiana Na Wazee Wastaafu Kufuata Huduma Za Afya Dodoma Na Badala Yake Wafuatwe Maeneo Waliko Ili Kuhakikiwa Kupata Huduma Ya NHIF, Kwani Wamekua Wakipata Taabu Sana Kufuatilia Suala Hili.