Wastaafu kuendelea na kazi kwa mkataba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wastaafu kuendelea na kazi kwa mkataba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Justine Kilasara, Aug 19, 2011.

 1. J

  Justine Kilasara Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hodi jamvini
  Kwangu mimi hili jambo linanikera sana. hasa kwa wastaafu wa serikali na mashirika ya umma. wengi wanaopata mikataba hii ni wale wenye vyeo vikubwa. kwa hiyo wanazuia ajira mpya kwani ili kulinda haki yao ya kuendelea na mikataba hii mibovu. wana jamvi naomba hivi, mtu akishastaafu aongoke ili apishe vijana waajiriwe na kupata uzoefu, vinginevyo waking'ang'ania kazini mpaka wafe, vijana watapata uzoefu lini? naomba maoni yenu
   
 2. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Justin, sio wote wanaong'ang'ania bali wanaombwa na ni kwasababu ya ujuzi wao. Kumbuka hili limeanza kutokea sana kipindi cha JK na Mkapa kama sikosei. Sababu ziko nyingi; lakini ambazo ninazifahamu na nimezishuhudia ni kwamba wastaafu wengi e.g. idara ya Mahakama ni wale wenye ujuzi wa uhakika. Hawa watu wapya wapya wengi wamepandishwa vyeo/ajiriwa bila sifa za kutosha/ujuzi. Mambo yamefanyika kiundugu-ndugu au tuseme kishkaji-shkaji, na wakiondoka hawa wazee wajuzi wazamani ndio utumbo utaanza kuonekana. Sasa serikali inawaomba iendelee na wao wanajua ndio tegemeo pekee . Kuna mmoja aliniambia wazi akasema; hiki kizazi cha wasomi wa awamu ya kwanzan na kidogo ya pili wakiondoka itakuwa janga la taifa. Yaani wengine tangu wameapishwa kuwa majaji for 2 years hawajawahi kuandika hukumu hata moja, wanapiga piga chenga then kesi inapangiwa majaji wengine. Ndio ushangae why JK anaapisha majaji kila siku lakini bado kunaucheleweshaji wakesi kutokana na ufinyu wa majaji? The answer is; wachache sana ndio watendaji wengine ni wasindikizaji. Sasa subirini mshuhudie hayo madudu yanayokuja huko mbele. God Bless Tz.
   
 3. M

  Mkomandaa Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kulikuwa na shiniskizo la kutoajiri kati ya 1992 - 2006 toka majuui. Japo kuwa watumishi walikuwa wanastaafu, wanaacha kazi wanabadilisha kazi, wanatorokea nchi zingine kukimbia mishahara midogo, Wanakimbilia ubunge n.k. Matokea yake watumishi serikalini wameisha. ilitabiriwa kuwa 2013, 70% ya watumishi watastaafu. Nani atafanya kazi?ij Ajira ya wastaafu ni mpango kabambe unaenda sambamba nakuajiri vijana wengi watakaofunzwa kazi na wastaafu hawa ili baada ya muda hali ya utumishi iwe shwari. Kamawewe ni kijana soma magazeti utapata kazi ya fani yako na utafunzwa utakuwa mtendakazi mzuri. Siyo kwamba wazee hawa wanazuia kazi hizo hadi wafe la hasha. Ni kuokoa jahazi tu miaka miwili mitatu.
   
 4. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Soma sheria ya utumishi wa umma 2002, kanuni zake za 2003. hapo utapata sababu kwani si kila jambo lifanyalwo na serikali ni kosa na usikerwe bali jishughulishe kujua na upande wa pili wa shilling ili uweze kubalance mambo kwa maslahi ya nchi yako.
   
 5. hengo

  hengo JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bila shaka mnao tetea wazee wa 60yrs waendelee kufanya kazi nanyi ni wastaafu ama wazee wenu.Binafsi siridhishwi na mfumo huo hasa ukizingati wimbi kubwa la vijana hawana ajira na wenye ajira hawapandishwi vyeo mbaya zaidi mfumo wa kufanya kazi kwa mikataba umeshamili hadi kwenye Idara nyeti kama Ikuru,mahakama na majeshini hasa Polisi na hivyo kudhorotesha mipango na maendeleo ya nchi, mbaya zaidi ni pale wastafu hao wanapopewa mamlaka makubwa na nyeti ya kutoa maamuzi makubwa ya kitaifa.Hii ni hatari sana kwa ustawi wa taifa letu.Kama muasisi wa Taifa hili aliamua kung'atuka hao wanaojifanya wanaujuzi wa kipekee wa nanii au ndo wemeiweka serikali viganjani mwao? Wizara za utumishi wa uma na Wizara ya kazi na Maendeleo ya vijana ziko wapi?
   
 6. N

  Nguto JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,652
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  Ni kweli vijana wengi hawana ajira lakini hawaajiriki!! Utamwajiri wapi kijana wa darasa la saba? Tatizo la vijana wa siku hizi shule hawataki. Wanataka maisha ya haraka haraka badala ya kusubiri wasome kwanza. Solution ya ajira anayo kijana mwenyewe kwanza ajitoe pale alipo e.g asome apate vyeti halafu atafite kazi au ajiajiri.kwa kutumia utaalamu atakaosomea.
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  mzee wangu kastaafu mwezi wa 3.......juzi ameombwa arudi kazini kwa mkataba
   
 8. T

  Tata JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Wazee ni taifa la leo, Vijana ni taifa la kesho na Watoto ni taifa la kesho kutwa. Kwa hiyo nyie vijana na watoto kwa sasa bado mpo mpo tu mnasubiri mataifa yenu. In the mean time ni kutesa kwa zamu tu kunaendelea.
   
 9. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  huwa siwapendi lakini wengi huwa hawajajiandaa na maisha ya uraini.
   
Loading...