Wastaafu - Je ni halali wananchi wabebe mzigo wa kutunza viongozi wabadhirifu?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wastaafu - Je ni halali wananchi wabebe mzigo wa kutunza viongozi wabadhirifu??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Morani75, Feb 19, 2008.

 1. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima kwa wanaJambo wenzangu. Nimekuwa nikifuatilia hili swala la serikali (through jasho la wananchi) kuendelea kuwatunza viongozi waliostaafu. Sina shida na wale waliostaafu sababu hata jeshini hawa wanatunzwa pia. Lakini nina hoja ambayo ningeomba kama wanaJambo watu wenye uchungu wa nchi na jasho la wananchi (ambao ndio sisi) tuijadili,

  Hoja yenyewe ni:

  "Je kiongozi aliyejiuzulu kutokana na kashfa inayohusishwa na rushwa, ni halali kuendelea kulipwa mafao na kupata huduma zote yeye na familia yake kwa maisha yao yote kwa gharama za wananchi ambao walidhulimiwa mali zao na kiongozi husika??"

  Tukiwa katika hilo pia tunagalie pande zote, upande wa kwanza ni uraiani (ambapo sheria ya matunzo haiongelei kuhusu wale viongozi waliojuiuzulu kutokana na ubadhirifu) na upande wa pili ni kwenye jeshi ambapo ingaw viongozi wastaafu wanatunzwa na jeshi lakini wale waliokuwa "Dishonourably discharged" sidhani kama wanapata maslahi na matunzo kama wenzao!

  Ka ajili ya kujua gharama za matunzo hayo, naomba tuangalie kwenye hii ThisDay ya leo kwa kubofya hapa chini:
  http://www.thisday.co.tz/News/3511.html

  Naomba kuwakilisha.......
   
Loading...