Muda usiopungua miaka kumi na hadi sasa wapo wastaafu wa Air Tanzania Company Limited wanadai mafao ya PPF sasa PSSSF hawajalipwa. Wastaafu wa ATCL wanadai haki yao kwa kuwa walikatwa kutoka katika mishahara lakini haikupelekwa PSSSF (PPF) hivyo kuwafanya waambulie mafao kidogo wakati wa kustaafu na pensheni ya kila mwezi kuwa ndogo sana.
Suala hili Rais Samia Suluhu Hassani analifahamu, bunge wanalifahamu, Katibu mkuu kiongozi marehemu Kijazi alikwisha agiza wizara Ujenzi na Uchukuzi kutekeleza malipo na apate mrejesho. Mahakama Kuu ilisha pitisha hukumu wazee hawa wastaafu wa ATCL walipwe lakini hadi leo hawajalipwa.
Waziri mkuu ana nadi serikali kutoa pesa kulipa wastaafu kauli ambayo wastaafu wanaiona kama ni siasa kwa kuwa PSSSF wanasema pesa inayolipwa na serikali ni kupunguza deni serikali ilikopa na sio ya wastaafu moja kwa moja hivyo hela hiyo hutumika kuendeshea taasisi au mfuko huo wa PSSSF.
Tunaomba Raisi Samia simamia suala hili ili wazee hawa walipwe maana hata huko wizara ya Fedha na wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuna watendaji hawataki haya madai ya wastaafu wa ATCL yalipwe. Bila ya Raisi kuwa imara vizazi na vizazi vya wastaafu na jamaa zao watakosa upendo na imani kwa serikali kitu ambacho wewe ndio SULUHU.