Wastaafu 51,000 walipwa trilioni 1.5/-

Ndenji five

JF-Expert Member
Nov 1, 2021
1,985
3,078
Mheshimiwa rais samia atoa trilion moja .
===
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umelipa mafao yenye thamani ya Sh. trilioni 1.15 kwa wanufaika, yaani wastaafu na wategemezi 51,079.

Vilevile, mfuko umelipa Sh. bilioni 692.38 za pensheni ya kila mwezi, sawa na wastani wa Sh. bilioni 57.7 kila mwezi kwa wastaafu 147,459.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, alibainisha hayo jana alipotoa taarifa ya mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

"Hii ni katika kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais yaliyotolewa katika sherehe za Mei Mosi, 2021, ambapo alielekeza madai ya mafao ya wastaafu yaliyocheleweshwa yaanze kulipwa kuanzia mwezi Mei, 2021 na kuendelea kulipwa hadi mrundikano utakapokwisha.

“Kiasi hiki cha fedha hulipwa kila ifikapo tarehe 25 ya mwezi husika bila kukosa. Hadi kufikia mwezi Februari 2022, mfuko umekamilisha kulipa madai yote ya muda mrefu," alisema.

Prof. Ndalichako alisema kuwa katika kuongeza kasi ya ulipaji mafao kwa wastaafu, serikali pia imelipa jumla ya Sh. trilioni 2.17 kupitia hati fungani.

“Fedha hiyo ni sehemu ya deni la Sh. trilioni 4.6 iliyotumika kufanya malipo kwa wanachama waliostaafu ambao hawakuchangia katika kipindi cha kabla ya mwaka 1999," alifafanua.

Waziri huyo pia alisema katika kipindi hicho, serikali imelipa Sh. bilioni 200 kati ya deni la Sh. bilioni 431 la mikopo ya uwekezaji lililokuwapo wakati serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani.

Vilevile, alisema katika kipindi cha mwaka mmoja, PSSSF imesajili wanachama wapya wapatao 21,461, sawa na asilimia 116.74 ya lengo la kusajili wanachama wapya 18,384 kwa kipindi husika.

“Wanachama hawa waliondikishwa kwa zaidi ya asilimia 60 wametokana na ajira mpya za kada za afya na walimu walioajiriwa na serikali katika awamu ya sita," alisema.

Waziri huyo alisema kuwa katika kuhakikisha wafanyakazi wanapata maslahi na haki zao za mafao, NSSF pia imeongeza kasi ya kusajili wanachama.

"Katika kipindi cha mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya sita, mfuko umeandikisha jumla ya wanachama wapya 185,288, sawa na ongezeko la asilimia 19 kulinganishwa na wanachama wapya 155,192 walioandikishwa katika kipindi cha mwaka mmoja ulioishia Februari, 2021," alisema.

Alibainisha kuwa kati ya wanachama hao, wanachama 153,119 waliandikishwa kutoka sekta rasmi na wanachama 32,169 waliandikishwa kutoka sekta isiyo rasmi.

Mfuko pia uliandikisha waajiri wapya 1,605, hivyo kufanya idadi ya waajiri kufikia 34,049 sawa na ongezeko la asilimia 4.9, kwa mujibu wa waziri huyo.

Alisema katika kipindi hicho, mfuko umekusanya michango ya Sh. bilioni 1,129.4 sawa na ongezeko la asilimia tano ya michango ya Sh. bilioni 1,075.3 iliyokusanya katika kipindi cha mwaka mmoja ulioishia Februari 2021.

“Aidha, mfuko umefanya mapitio ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari ili kuvutia wanachama wapya kutoka katika makundi mbalimbali ikiwamo vijana waendesha bodaboda na bajaji, kinamama, wanavyuo, wakulima na wavuvi.

“Ili kuongeza wigo wa wanachama na mafao yanayokidhi mahitaji ya makundi hayo, mpango wa uchangiaji wa hiari umeboreshwa na utazinduliwa rasmi hivi karibuni," alisema Prof. Ndalichako.

Aliongeza kuwa katika kuboresha mafao ya fidia kwa wafanyakazi, serikali imeongeza kiwango cha juu cha pensheni kutoka Sh. 3,685,852.69 na kufikia Sh. 8,400,000.00 kwa mwezi.

“Ongezeko hili limekuwa faraja kubwa kwa wafanyakazi na waajiri nchini na linachangia kupunguza umaskini kwa wategemezi wa wafanyakazi wanaofariki dunia kutokana na kazi," alisema.
 
Hii ni baada ya kuwasubirishaa weeh nje juani na nenda Rudi za kutosha na malalamiko mengi!

Walilipwa kweli wake hadharani wakiri!

Janjajanjaa nyingi Sana Kwa hawa wapenda kukaa front page!
 
Watu wanalipwa pungufu halafu zilizobaki wanazisotea utafikiri ni HISANI.

Hili nalo ni agizo tu kama yalivyo maagizo mengine mengi ya kisiasa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom