Wassira, Tendwa waipiga mkwara Chadema - Chatishiwa kufutwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wassira, Tendwa waipiga mkwara Chadema - Chatishiwa kufutwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Smartboy, Mar 3, 2011.

 1. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kuna mwana ccm hapa mlimani tv anasifu Jk na kulaumu cdm. Yaani huyu jamaa sijui wamemtoa wapi. Jaribuni kuangalia
   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Yupo mtu anaitwa Lisasi Mwaulanga, ni mnafiki hakuna mfano, nimepoteza appetite ya kuangalia.
   
 3. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa anasema cdm wametembelea kaburi la Jk Nyerere mara 5, ila hawajawahi kutembelea la mzee Karume, inaoneka ana kaudini kwa mbali
   
 4. h

  hamenya Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata mimi naona Mlimani TV imekosa watu wa kuzungumzia hali ya siasa nchini. Wanapokosa watu wasirushe matangazo. Upuuuziiiii.
   
 5. markach

  markach Senior Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hawawezi kuifuta CDM. Kama uliangalia maojiano ya Wasira na TBC juzi, alishindwa hata kutoa Tamko la kuzuia maandamano japo alilazimishwa sanaaaa na Gabriel Zakaria, sembuse kuifuta? Mi nafikiri ni ngumu kama kupiga ngumi ncha ya mkuki au kumpiga Ng'e busu
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kuifuta cdm hawawezi wafa maji tu hao..hawaachi kutapa tapa....na jinsi mkwere anavyoendesha chama mwaka 2015 atawaachia kazi mzito wenzake
   
 7. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  CHADEMA kwa sasa sio chama cha siasa tu bali ni harakati zilizopo ndani ya mioyo ya watu.Kukifuta ni sawa na kukibadilishia tu jina.mimi na wewe tutabaki walewale.serikali isipotimiza wajibu wake madai yetu yatabaki yaleyale.CHADEMA kikinyamaza mawe yataongea.
   
 8. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  gazeti la mwananchi la leo limemkariri Mbowe akisema Wassira hana ubavu wa kuzuia maandamano ya CHADEMA
   
 9. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Waziri wasira amenukuliwa akisema eti serikali ikifika mwisho na uvumilivu wake,itawashughulikia viongozi wa chadema,kwa kosa la kuchochea chuki dhidi ya serikali,,ni bahati mbaya kuwa leo bado tuna waziri na mbuge Kilango ambao hawana hata uwezo wa kusoma alama za nyakati,,ndugu wasira suluhisho pekee la haya ni kuboresha maisha ya mtanzania,na kamwe serikali na vyombo vyake vya dola haviwezi kuzuia maandamano ya umma wa watanzania uliochoka na kupigika katika lindi la umasikini.
  Boresheni maisha ya mtanzania na chadema wakose ajenda,huwezi kumtisha mtu mzima nyau,,Kudhubutu kuwaweka viongozi wa chadema kizuizini mtakuwa mmejiandalia anguko lenu wenyewe....
  Peoples power forever..
   
 10. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jamani,

  Hizi propaganda za kutaka kuzima nguvu ya wananchi kutaka kuona viongozi wao wanawajibika kwao na kuanza kuuita uhaini imekaa vipi hii wadau!

  Mimi siyo mtaalamu wa sheria na kwa bahati mbaya sijaiona sheria ya uhaini ina-define vite neno "uhaini" lakini kwa uelewa wangu wa ki-layman nadhani uhaini ni kufanya kosa linalohatarisha uhai na utengamano wa jamii unayoishi.
  Ukichukua definition yangu hii matendo ambayo ningeyaingiza kwenye uhaini yangekuwa ni kama ifuatavyo: kuchochea udini (Kikwete amefanya hivyo kwa kuanza kuuhubiri kwenye majukwaa ya siasa bila kuwachukulia hatua aliosema wanachochea udini huku akiwa ndiye amiri jeshi mkuu wa majeshi yetu) au kutochukua hatua ukiwa na mamlaka ya kuwachukulia wale wote wanaochochea udini (wapo wengi lakini miongoni mwao yapo majarida ya Al hulda,n.k), kuhujumu uchumi wa nchi au kutowachukulia hatua yoyote wanaotenda kosa hili ukiwa wewe umepewa dhamana ya kusimamia sheria na kuhatarisha maisha ya raia wa nchi hiyo kwa kuwakosesha huduma za msingi kama afya, elimu, chakula, n.k (Wafisadi, CCM na serikali yao wanafanya hivi).
  Kwa mtazamo wangu Chadema wanahamasisha wananchi kuwawajibisha watawala wao pale ambapo watawala watashindwa kusimamia sheria na kutetea masilahi ya nchi kama walivyoapa wakati wanakubali majukumu hayo.
  Propaganda za kutaka wananchi wawachukie Chadema zinafanikiwa kuwaongezea umaarufu Chadema na viongozi wao kuliko kuwaonya wananchi wasiwasikili. Ninaamini wanachi wa Tanzania siyo wehu wa kufuata mambo ya kipumbavu kama ambavyo Kikwete na serikali yake wanataka tuamini, ninaamini watu hawa wanakwenda kuwasikiliza Chadema kwa hiari yao na wanaamua kwa hiari yao kuwaunga mkono, kama CCM na serikali yake watataka kuwalazimisha wananchi wasiwapende Chadema watakuwa wanavunja katiba waliyoahidi kuilinda.
  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika... ALUTA KONTINUA!
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Mrema, Wassira waivaa CHADEMA


  Na Waandishi Wetu

  VYAMA vya upinzani vimetakiwa kuangalia njia wanazotumia katika kupata madaraka kwa kuwa baadhi yake hasa malumbano zinaitumbukiza nchi kwenye
  maafa na maangamizi kama ilivyowahi kutokea kwenye nchi nyingine duniani.

  Akizunguma na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbunge wa Vunjo, Bw. Agustino Mrema alisema malumbano yanayojumuisha maandamano pamoja na mikutano ya hadhara inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupinga ufisadi serikalini ni hatari kwa usalama wa nchi.

  Kwa mujibu wa CHADEMA maandamano hayo ni kupinga hali ngumu ya maisha, iliyosababishwa na kupanda kwa bei ya vyakula, bei ya umeme na kupinga malipo kwa kampuni ya Dowans.

  Bw. Mrema alisema serikali iondolewe kwa kutumia njia ya katiba na si njia za mkato, kama maandamano kwa kuwa njia hizo zinaleta matatizo makubwa zaidi na kusababisha maasi na uvunjaji wa amani nchini na kuliangamiza taifa kama Somalia ilivyoangamia.

  "Wapinzani wamepewa kazi ya kupambana na ufisadi kwa kutumia bunge na kama wakishindwa ni udhaifu wao wenyewe na sio serikali. Ufisadi hauwezi kumalizwa kwa maandamano bali ni kubuni sera mbadala na mikakati endelevu ya kuleta maendeleo," alisema Bw. Mrema.

  Kauli ya Bw. Mrema inashabihiana na ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Bw. Stephen Wassira aliyoitoa kwenye Kipindi Maalumu kilichorushwa juzi usiku na Televiesheni ya Taifa na krudiwa jana mchana, akisema chama hicho kimekuwa kikiwachochea wananchi kuindoa serikali kwa maandamano, jambo ambalo ni kinyume cha katiba.

  Hata hivyo, alisema CHADEMA haina uwezo wa kuiondoa serikali madarakani kwa njia hiyo, lakini kwa kutamshi yake tayari wamevunja katiba na sheria za vyama vya siasa na ile ya usalama wa taifa.

  Katika hatua nyingine, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi, Bw. John Cheyo alionya hali yoyote ya kuhatarisha amani nchini akisema hata CHADEMA wanafanya maandamano yao na mikutano kwa sababu Tanzania kuna amani, hivyo hawana budi kutoa hotuba ambazo zinalenga kuhimiza amani.

  "Wanasiasa tuache hisia za ushabiki na kupenda kuzungumzia vitu ambavyo ni hatari kwa taifa, alisema Bw. Cheyo.

  Aliongeza matatizo ya wananchi yasichukuliwe kama njia ya kukaa na kuanzisha mijadala isiyo ya msingi isipokuwa jibu lake ni kufanya kazi kwa bidii na kama mijadala ikiendelea inaweza kutokea hali mbaya ya siasa kama ilinayoendelea nchini Libya.

  Mbali na hilo, Bw. Cheyo alitaka Rais Kikwete kutimiza ahadi yake ya kuchukua maamuzi magumu kwa mambo yanayolalamikiwa katika serikali yake bila kujali kama yatawaudhi wanasiasa marafiki waliomo katika serikali yake.

  Alimtaka Rais Kikwete kuwahakikishia Watanzania amani, kuwaondoa katika hofu inayojitokeza na hali ngumu ya maisha ikiwemo gharama za kupanda kwa maisha.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Cheyo alisema Serikali ya Rais Kikwete imepoteza matumaini na kuleta hofu kwa wananchi na ikiwa ataendelea kukaa kimya bila kuwahakikishia amani nchi inaweza kuelekea kubaya.

  "Rais Kikwete anatakiwa kufanya maamuzi ambayo yatawaridhisha Watanzania, anatakiwa kufanya maamuzi, hata yasipowapendeza marafiki zake, ili kulihakikishia taifa amani," alisema.

  Alisema amani Tanzania imeanza kutoweka na ikiwa Rais Kikwete ataendelea kukaa kimya bila kuchukua uamuzi wananchi watatakiwa kufanya maandamano kudai amani kwa sababu ni haki yao.

  Katika hatua nyingine Cheyo alisema kuhusu suala la umeme la mkataba kati ya Shirika la Umeme Tanzania TANESCO na kampuni ya DOWANS wanasiasa wanatakiwa kuiunga mkono mahakama na kuiacha ilishugulikie kisheria kuliepusha taifa katika malumbano yasiyokuwa ya msingi.

  Bw. Cheyo pia amemtaka Mbunge wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora Rostam Aziz kuchagua moja la kufanya kati ya biashara au siasa kumsaidia rais na serikali yake kufanya kazi.

  "Rais anatakiwa kujua hali ya hewa ni chafu, hali ya hewa kwa Rostam sio nzuri, achague moja la kufanya kwani kwa kufanya hivyo atakuwa ameisaidia serikali na taifa na kama angekuwa kwenye chama changu ningeshamtimua," alisema Cheyo.

  Imeandikwa na Nassra Abdulla, Amina Athumani na Addolph Bruno

  [​IMG]


  11 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... Cheyo na Mrema waache kujipendekeza kwa chama tawawla, wameona wamezeeka ndiyo maana wanaona wajipendekeze ili serikali iwafikirie baaadae.Kweli CHADEMA wanaweza kutumia bunge lakini ni wachache na hoja yao haiwezi kusikilizwa sana watazomewa na wana CCM pamoja na CUF. Tusiogope yanayotokea LIBYA kwani kwetu hapa hayawezi kutokea kulingana na misingi ya taifa letu iliyoundwa na Mwl. kama yakitokea si sasa hivi, iaweza kutokea labda baada ya miaka mingi ijayo kama kuna wasiwasi basi CCM na CHADEMA wakae pamoja wajadiliane ili kutafuta namna gani kero hizi za CHADEMA zinzvyoweza kutatuliwa kwa masilahi ya taifa.
  March 3, 2011 11:02 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Cmm acheni kutesa wananchi, sera zenu mbovu hamna cha kujitetea. Hao akina Mrema ni wachovu tu nao wanaangalia maslahi yao.
  March 3, 2011 11:38 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Wasira ni rafiki wa mafisadi.Watanzania tumechoshwa na ukandamizaji unaofanywa na CCM.CCM sasa hatuitaki.Serikali ikianzisha vurugu au kuwakamata viongozi wa CHADEMA huo ndio utakuwa mwanzo wa vita.Wananchi tutatumia marungu na mapanga na mikuki kama Mkwawa, nyie CCM mtumie mabomu yenu hayo ya Mbagala na Gongolamboto. Tuko tayari kufa kwa kuondoa ufisadi walau kizazi kijacho kiishi vema kwenye nchi yenye asali na maziwa tuliyojaaliwa.Hahaaaaaa!
  March 3, 2011 11:44 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... CCM acheni kupeana uongozi katika ngazi mbalimbali kirafiki.Sasa wananchi wamefungua macho hata mkiwatisha hamuwezi,mbona mabomu sasa tumeyazoea.Hatuogopi hivyo vibomu vyenu mlivyonunua kwa pesa nyingi wakati watu hawana dawa hospitalini.Ushauri wa bure,Rostam ajihuzuru ubunge,Lowasa ajihuzuru ubunge,Ngeleja ajihuzuru uwaziri.Mkifanya hilo tu umma wa watanzania watarudisha imani kwa CCM kwa asilimia fulani.Vinginevyo acheni CHADEMA wachape kazi.
  March 3, 2011 11:50 PM [​IMG] [​IMG]
  mallya said... Maandamano ya CHADEMA kuandamana kulalamikia hali ngumu ya maisha hayako specific,kwa sababu hali ya maisha kuwa ngumu ni tatizo la miaka mingi.And it is not something that is gonna change tommorrow. Tatizo hapa ni sera ziboreshwe hasa zinazolenga watu wenye maisha ya chini kabisa ambao ndio wengi.
  Rais Kikwete katoka na "Kilimo kwanza".Jengeni hoja kwenye hili kwa sababu ndio hapa pekee tutakapomaliza tatizo la mfumuko wa bei ya vyakula.Jengeni hoja bungeni kwenye bajeti,na vikao vingine vya bunge,badala ya maandamano nchi nzima.
  Isitoshe,baada ya maandamano haya,hali ngumu ya maisha ndio itaisha?Na je isipoisha,kwa muda mfupi kama CHADEMA wanavyotaka,then what,ndio wataiondoa serikali madarakani kama wanavyosema "mpaka kieleweke"??.
  CHADEMA kuweni realistic,you folk should put forward the targets which are achievable.!!

  March 3, 2011 11:54 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Hawa wanalipa fadhila. Kupewa uenyekiti wa kamati za bunge ingewezekanaje kwa vyama vyenye mbunge mmoja? Hii inawezekana? Walipewa support na CCM, lazima waitetee CCM.
  March 4, 2011 12:09 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Wewe Mallya Saidi,unajua pesa wanazoiba viongozi walioko madarakani zingesaidia kupunguza makali ya maisha kwa kutoa ruzuku kwenye vitu kama vile: gharama za umeme,vyakula toka nje,viwanda vidogovidogo,kilimo n.k. Kwa kuwa CCM inagawa madaraka kiurafiki basi kila kiongozi anaiba kwa kwenda mbele.Hivyo wananchi wakielimishwa watasimamia haki zao.Mishahara inakatwa kodi kubwa lakini inaishia kwa wachache.Naomba Mallya Saidi ubadilike.Hapa hatuna ushabiki wa chama bali ukweli.
  March 4, 2011 12:12 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... kaka Mallya said,hongera kwa kuwa na upevu wa mawazo.japo sikufahamu naamini ww ni mmoja wa watanzania wenye busara.ugumu wa maisha ya watanzania usitumiwe na wanasiasa kujitafutia umaarufu then tuushabikie ila tuchape kazi ili tuutokomeze umaskini huu wa kutisa.lakini kama amani na mshikamano vikitoweka pia hatutakuwa na nafasi ya kuutokomeza bali tutauzidisha zaidi ,maana pengine tutakuwa wakimbizi ktkt nchi jirani.tukemee mabaya kwa busara na tuikosoe serikali kwa hekima bila kutukana viongozi wetu au kuwalaani.maana wapo wazuri na wabaya,wale mafisadi tutumie sheria zaidi kuwahukumu,maana sheria ipo kwa ajili ya wahalifu.pia tujue siasa ni propaganda jamani tusiishabikie kupindukia.
  March 4, 2011 12:24 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Hivi huyu jamaa Rostam anahusishwa vipi na ugumu wa maisha ya watanzania? ina maana Rostam ndiye aliyeshika akili za viongozi ,watendaji na wanachi wa tanzania yote kiasi cha kushindwa kufikiri jinsi ya kujindoa katika matatizo tuliyonayo? tatizo siyo Rostam bali ni sisi wananchi na viongozi tulio nao. hivi Rostam ndiye anayepanga na kupitisha matumizi makubwa ya kifahari kwa viongozi na watendaji wetu katika serikali, posho kubwa,magari ya kifahari wakati wananchi wa kawaida hata mlo mmoja shida,tofauti kubwa ya kipato,huduma za jamii wakati nchi ni yetu sote, ni lazima tubadilike na kukubari kuwa hawa wenzetu pia watu na wanastaili kupata huduma bora, hakuna mwananchi atakaye kubari kuandamana na kuiondoa serikali madarakani kama atakuwa anapata huduma bora za jamii kama shule,tiba usafiri na mlo wake wa kila siku.lakini kwa stahili hii ya kufanyana wajinga hakutakuwa na amani ya kudumu, maana itafika wakati inakubidi mwananchi uchague kufa kwa njaa na kwa kukosa huduma muhimu au kufa kwa kudai haki yake.tusimgeuze Rostam mbuzi wa kafala wakati hata nyinyi wanasiasa wengine mnasababisha nchi hii kwenda pabaya kwa kujari zaidi maslahi yenu,
  March 4, 2011 12:30 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... maisha magumu ya Watanzania yasiwe mtaji wa wanasiasa,kaeni bungeni mjadili namna ya kuboresha huduma za jamii. chadema, CCM na vyama vingine vya upinzani zungumzeni mstakabali wa taifa letu wanaotaka kuchochea maandamano kuing'oa serikali madarakani wanadanganyika hiyo vita wanaisikia tu kwa majirani, haijawapigia hodi haya endeleeni, mtoto akililia wembe hupewa! ujinga wetu ulituongoza kuichagua CCM licha ya sera nzuri zilizosemwa na chadema wakati wa kampeni, mbona kwenye masanduku ya kura hatukujitokeza kama kwenye mikutano ya chadema, halafu tunasingizia eti kura zilichakachuliwa na sasa tumechoka na ufisadi tuwaondoe kwa maandamano wakati ni miezi michache tu imepita tangu uchaguzi umalizike? nani aniambie ni kipi kipya sasa ambacho chadema hakikusema wakati wa kampeni? kwa nini hamkutumia nguvu hiyo kuindoa CCM kwa kura, mbona maeneo waliofanya hivyo chadema ilishinda? acheni kutudanganya subirini uchaguzi 2015, watu wafanye kazi kwa sasa.acheni kuchochea vita ikitokea hata huo mlo mmoja ya watoto wako hautaupata na utajenga visasi visivyoisha ndani ya nchi hii kwa vizazi vyote.'akili ya kuambiwa changanya na yako'tusiwe remote control watanzania wenzangu.
  March 4, 2011 1:16 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Mrema na Cheyo ni makuadi wa CCM kwa sasa. Mrema anasahau alipokuwa NCCR jinsi wananchi wa kawaida walivyosumbuliwa wakati akipinga ufisadi? Sasa amejumuika nao!
  CUF, CHADEMA, NCCCR na wengine msikubali 'mihadhara' kutoka kwa viongozi wa CCM kana kwamba wao ndiyo wana akili zaidi ya wengine!
  Wasio wana-CCM ni Watanzania /Wazalendo vile vile ni wapembuzi yakinifu pia, kwa hiyo wasikilizwe.

  March 4, 2011 1:29 AM
   
 12. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Teh teh............uwwwwwwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

  Haya mkuu naanza week end
   
 13. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  tendwa ailima barua cdm ya uhaini , kimesera asema atoe ushahidi vinginevyo hawakubali onyo
   
 14. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ni sheria gani waliyoivunja, maandamano ni haki ya kila mtu, mikutano ni haki ya kila chama cha siasa, Hayo mambo ambayo CDM wanayazungumza ni uongo? kwani wamemtukana mtu? Wao wanagomba ugumu wa maisha, kutoilipa DOWANS na kupanda kwa bei ya umeme, sasa wao kama wapinzani wana kazi ya kucritisize serikali, sasa serikali inataka wawacritisize kistaarabu?

  Serikali inasema CDM wanao uwanja wa bungeni kupeleka hoja zao, lakini tumeshuhudia jinsi bunge lilivyoanza uendeshaji ulikuwa ni wazi wa kuwabana CDM, wamewakejeli wakawambia poor politicians, na mambo mengi. Walifikiri chadema wananjia ya bunge tu kumbe wamenoa. Sasa wanashitaki kwa wananchi, na kuwaonesha kuwa pamoja na wabunge wa CCM na vyama vingine kujaribu kuwapaka matope wabunge wa CDM kuwa hawafai na wananchi wasiwachague tena, lakini bado CDM wanapata wafuasi wengi na wanaongezeka umaarufu tofauti na walivyotarajia.

  Ni jambo lisilowezekana kukifuta CDM eti kwa sababu wanzungumzia ugumu wa maisha.
   
 15. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Kutokana na harakati za CDM kuwakomboa wananchi kushika kasi nchi nzima, Msajili wa vyama vya siasa amekurupuka kuwaandikia CDM barua ya onyo akidai kuwa inachochea wananchi kuvunja sheria za nchi. Pia cha kushangaza zaidi wakati anahojiwa na mwandishi wa TBC1 Tendwa anajigamba kuwa ana uwezo wa kuifuta chadema na kwa sasa mkono wa DPP unawasha kuandika hati ya mashtaka kwa chadema.
   
 16. P

  PakavuNateleza JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 957
  Likes Received: 513
  Trophy Points: 180
  Eleweka mkuu ni barua ya uhaini au onyo? And either of the above kwanini?
   
 17. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao ndio wanataka nchi hii isitawalike, ngoja tusubiri tu
   
 18. T

  TULIBAHA Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ccm waache uongo na unafiki na hayo ndio matokeo ya kuiba kura. Nasema watatukoma hebu wajaribu kuwa na fikra chanzo cha yote ni nini. Kwa staili hii naona na tendwa yupo biased jamaa nae kumbe ni ccm hebu afute chama tuone
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Mar 4, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,736
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..vijana wana maoni gani kuhusu maandamano ya CDM?

  ..wazee sasa hivi hawawakilishi mawazo ya walio wengi.
   
 20. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  john Tendwa ametoa onyo ila kiongozi wa chadema kasema ilo onyo its just a vague so hawana la kujibu. na kama wanaona wamekosea waende kokote.
   
Loading...