Wassira: Nasisitiza Vincent Nyerere sio Ukoo Wa Nyerere

Kwa kauli hizi nina kuhakikishieni kuwa hii ni hujuma dhidi ya Siyoi na CCM kwa ujumla. Naona kinachofanyika kuhakikisha wana mkomoa yule aliyempa tafu Siyoi mpaka akapitishwa kuwa mgombea ubunge.

Kwa namna yoyote hile Wapiga kura wa Arumeru hawawezi kushawishika kwa kauli hizi zisizo na mashiko kumpa kura zao Siyoi. Wanaarumeru wanazoshida nyingi sana zinazokwamisha maendeleo yao.Hizi polojo wanazozitoa hawa akina 'Mh'. Wassira na wenzake ni dhahiri wanamuhujumu Siyoi na CCM kwa ujumla.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Usukumani kuna simulizi tuliikuta kuwa mtu anayelala lala sana kama afanyavyo Wasira au yule wa game resrve ya Gombe kule kigoma basi ujue wazazi walikuwa wanawa chanjia dawa inayochanganywa na mnyama mmoja anaitwa kwa kisukuma FUNGO, tabia ya mnyama huyu ni mbili kuu ya kwanza ni kujisaida sehemu moja kila siku,yeye akibanwa haja hata kama alikuwa arusha mjini basi atakwenda kujisaidia USA river, kila siku hufanya hivyo na tabia yake ya pili ni kulala lala kila wakati tena usingizi wa pono.

Hata kama akikurupushwa na mbwa au basi yeye huwa anakimbia muda mfupi tu na kisha analala,anaweza akakimbia hatua kumi tu kisha analala,basi nadhani kwa ulalaji wa Tyson huenda wazazi wake walimchanjia hiyo dawa baada ya kumuona ni mtoto aliekuwa anawasumbua kwa kulia sana, na hivyo ku-adapt tabia za huyo mnyama, na ndio maana yeye akikurupuka kutoka usingizini anadandia hoja na kuropoka,kama ni mjengoni akiamka anapiga makofi kwa kugonga meza. Hii ndio maana amerudia tabia mipasho ya kung'ang'ania kuwa Vicent sio wa ukoo wa Nyerere, na kwa jinsi ninavyomjua Mh Vicent kwa jukwaani ndio maana wamepanic naye sana.

CCM- magamba tupambaneni kwa hoja sio kuingilia mambo ya ukoo wa fulani hayatawasaidia wananchi wa arumeru
 
Uwongo, Kijiji kinachotajwa ndiko aliposemea Wasira hata Wasirra mwenyewe hajafika, Tena hasemi chochote kuhusu Vicent Nyerere. Wasira anamjua Vicent anamfahamu baba yake mama yake.hata baba yake Josephat Kiboko Nyerere alipofariki yeye binafsi alihudhulia mazishi. Sasa kutumia Jf kusema uongo kunasaidia nini?
 
...............Miaka mingi ya kazi alioifanya Mwalimu Nyerere kwa ufanisi mkubwa kuondoa migawanyiko ya kikabila leo hii kule Arumeru Mashariki tena kwa hisani ya CCM watu tumeanza kusikia vifungu vya maneno kama vile 'Sisi Wamasai', 'Wao wa Musoma', wengine 'Wabunda' -.....

Bahati mbaya sana mlezi wa vyama vya Siasa John Tendwa hawezi kulikemea hili.
 
Baada ya siasa za UDINI kugoma, CCM sasa yaanza rasmi na siasa za KIKABILA kwa mara ya kwanza Tanzania; na hili sasa tukaliweke vizuri kwenye kumbukumbu kunakoelekea uchaguzi mkuu 2015.

Miaka mingi ya kazi alioifanya Mwalimu Nyerere kwa ufanisi mkubwa kuondoa migawanyiko ya kikabila leo hii kule Arumeru Mashariki tena kwa hisani ya CCM watu tumeanza kusikia vifungu vya maneno kama vile 'Sisi Wamasai', 'Wao wa Musoma', wengine 'Wabunda' - ama kweli chama kikifilisika kisiasa kumbe ne hatari mwisho hivi!!!

Jamani kuna HATARI kubwa sana inatusubiri kama taifa huko tuendako kwa mtindo huu wa CCM endapo hatua za haraka kudhibiti mambo haitochukuliwa kwa wakati.

JK Nyerere aliwahi sema MTU ALIYEFILISIKA KISIASA dalili yake kubwa ni kwamba" asipojihalalisha KIKABILA atajihalalisha KIDINI au KIKANDA. Mara muonapo mambo hayo yakitokea hususani kwa Chama kilicho ongoza nchi miaka karibu hamsini mjue kimezeeka na ule mwisho wake unakaribia
 
Kwa kauli hizi nina kuhakikishieni kuwa hii ni hujuma dhidi ya Siyoi na CCM kwa ujumla. Naona kinachofanyika kuhakikisha wana mkomoa yule aliyempa tafu Siyoi mpaka akapitishwa kuwa mgombea ubunge. kwa namna yoyote hile Wapiga kura wa Arumeru hawawezi kushawishika kwa kauli hizi zisizo na mashiko kumpa kura zao Siyoi. Wanaarumeru wanazoshida nyingi sana zinazokwamisha maendeleo yao.Hizi polojo wanazozitoa hawa akina 'Mh'.Wassira na wenzake ni dhahiri wanamuhujumu Siyoi na CCM kwa ujumla.


Na mimi niliwaza hivyo hivyo. Huu mtandao wa Wassira una mkakati wa kummaliza Sioi.
 
uu upumbavu mwengine wa ajabu sana,
Eti mtu achaguliwe ubunge kisa baba yake kafariki, hizi ndizo sera gani sasa??
Wangapi katika hao wanaohutubiwa hawana Baba??
Tushageuka Korea sasa!!
 
Uwongo. Kijiji kinachotajwa ndiko aliposemea Wasira hata Wasirra mwenyewe hajafika, Tena hasemi chochote kuhusu Vicent Nyerere. Wasira anamjua Vicent anamfahamu baba yake mama yake.hata baba yake Josephat Kiboko Nyerere alipofariki yeye binafsi alihudhulia mazishi. Sasa kutumia Jf kusema uongo kunasaidia nini?

Ehee ! ebu tueleze muda huo anaodaiwa/unaodaiwa alikuwa/ulikuwa maeneo hayo, je alikuwa/ulikuwa wapi na anafanya/unafanya nini?

Uje na udhibitisho halisi hapa vinginevyo nitakushikia bango mpaka ulimwe 'BAN' kwa kumuita muanzisha thread muongo.
 
CCM KUSHUKA VIWANGO VYA SIASA KIASI HIKI WATANZANIA TUTARAJIE KUSIKIA MAAJABU MAZITO ZAIDI KULIKO YALE YALIOIBULIWA NA KAMPENI ZA ARUMERU MASHARIKI

Ukiona CCM sasa inainamia silaha mpya kama vile:

(1) 'VURUGU ZA GREENGUARD-Mwigulu', (2) 'Ukabila-Ole Sendeka' na sasa (3) 'Oparesheni Kimbiza Kivuli cha Mwalimu Nyerere kila kona ya Nchi' inayoongozwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akisaidiana kwa karibu sana na Mzee wa Usingizi wa Pono Mzee Wasira a.k.a. Mzee Tyson, ni wazi kwamba hali si shwari hata kidogo ndani ya CCM

Si miezi mingi sana Watanzania tutashuhudia maajabu ya dunia zaidi ya yale yanyoendelea kuibuliwa kwa CCM kwenye kampeni kule Arumeru Mashariki; watch this space.
 
tunaweza kuwalaumu lusinde na wasira bila kufanya tafakuri ndogo. kwa upande wangu naona kauli hizi kama za makusudi ili kumuharibia mgombea wao mana ccm inayomnadi sioi inawezekana siyo ccm iliyokuwa unamtaka sioi kuwakilisha chama cho. hivyo hizo ni hujuma ili isiweze kuwa mbunge!
 
Nilikuwa namuheshimu sana mzee sendeka kumbe ni ovyo kabisa,kwenye ukabila watu tulishatoka kitambo ila sasa ndo inaonekana ajenda kuu kwa mujibu wa sendeka! Mwigulu nchemba ni mmeru? Yeye mwenyewe ni mmeru? Wassira je? Na huyo wassira si ndo alikuwa anampinga sioyi kwenye vikao vya ndani vya magamba? Sasa anafanya nini huko Meru?
 
Isiwe taabu; Vicent waachie hilo jina bana! Steven Wassira anapenda naye kujiita Steven Nyerere, sasa tuna Benjamin Nyerere, Jakaya Nyerere, Siyoi Nyerere, hata Ole Sendeka nae awe Ole Nyerere. Mimi nilidhani mmekwenda kushindana na mgombea kumbe mnashindana na meneja wa kampeni!
 
Uwongo. Kijiji kinachotajwa ndiko aliposemea Wasira hata Wasirra mwenyewe hajafika, Tena hasemi chochote kuhusu Vicent Nyerere. Wasira anamjua Vicent anamfahamu baba yake mama yake.hata baba yake Josephat Kiboko Nyerere alipofariki yeye binafsi alihudhulia mazishi. Sasa kutumia Jf kusema uongo kunasaidia nini?
Kakojoe ulale.
 
Ni jambo la busara kabisa
Isiwe taabu; Vicent waachie hilo jina bana! Steven Wassira anapenda naye kujiita Steven Nyerere, sasa tuna Benjamin Nyerere, Jakaya Nyerere, Siyoi Nyerere, hata Ole Sendeka nae awe Ole Nyerere. Mimi nilidhani mmekwenda kushindana na mgombea kumbe mnashindana na meneja wa kampeni!
 
Mh. Wassira ni mtu wa CCM na pia ni mbunge wa Bunda ambayo iko mkoa wa Mara ambayo makao makuu yake ni Musoma..
Ole Sendeka akimpinga Mh. Nyerere pia anapaswa kumpinga Mh. Wassira kwa kuwa wote wanatoka Musoma.

ndugu yangu sometimes it very difficult to follow the logic out of confused people.
 
Mimi sina tatizo na wagombea ubunge, kinachonishangaza ni pale watu wenye busara zao kwenda jukwaani na kuwambia wananchi eti "mbunge achaguliwe hili apate pesa za kusaidia familia yake kwa kuwa mhusika mkuu kesha tangulia mbele ya HAKI!" Jamani hii ni kampeini ya aina gani - kweli Watanzania tumekwisha fikia hatua ya kukosa hoja za msingi na kutafuta public sympathy kwa mtindo huu, sielewi mimi.
 
Ni jambo la busara kabisa
Isiwe taabu; Vicent waachie hilo jina bana! Steven Wassira anapenda naye kujiita Steven Nyerere, sasa tuna Benjamin Nyerere, Jakaya Nyerere, Siyoi Nyerere, hata Ole Sendeka nae awe Ole Nyerere. Mimi nilidhani mmekwenda kushindana na mgombea kumbe mnashindana na meneja wa kampeni!
 
Vicent Nyerere anapata wapi nguvu ya kuwaamulia wana arumeru?
Hofu hii inatoka wapi kwa wasira? au Vicent atapiga kura kwa niaba ya wana arumeru?
Sielewi kama Sendeka anajua sheria ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom