Wassira: Dk. Slaa ni kama Dereva Learner Kujaribu Ku-Drive Basi la Abiria!

Ndio Hisia + Pumba...Dr. Slaa hasemi atafanyaje mfuko wa Cement uwe Tsh. 5,000/=.. Show us experience aliwahi kufanikisha hilo wapi, lini?

Perform a task so we can know your capable of achieving..Otherwise, Mageuzi Tanzania bado kama Dr. Slaa is one of TZ best..more info please
 
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Bunda mkoani Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amewaomba wapiga kura jimboni humo kutompigia kura mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa kwa madai kuwa hana uzoefu wa uongozi.

Wasira amesema, kama wakimpigia kura Dk. Slaa ni sawa na kumkabidhi dereva anayejifunza gari, usukani wa basi la abiria.

Badala yake Wasira ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, (Nec) amewataka wapiga kura hao kumpatia kura nyingi za ushindi mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete kwa kuwa ni dereva makini aliyehitimu mafunzo yote aliyeiendesha nchi kwa usalama katika miaka mitano iliyopita.

Akihutubia mkutano wa kampeni za CCM juzi kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Bukama na
Nyabehu, Wasira alisema tofauti na Kikwete, Dk. Slaa hajawahi kushika nyadhifa zozote za kiutendaji ambazo zinaweza kutumika kushawishi watanzania wamchague kushika mamlaka makubwa ya kiutendaji.

“Slaa huyu hajawahi kushika wadhifa wowote ule wa kiutendaji, hata uofisa utendaji wa kijiji ili tumwone anavyoamua mashauri mbalimbali yanayomfikia. Leo tumpe kura za urais?

Tumechanganyikiwa yaani tumpe ‘learner’ gari la abiria! Akiwaangusha nani alaumiwe? Mnyimeni kura,” alisema Wasira.

Wasira ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika alisema nafasi ya urais ipo ya juu zaidi katika muundo wa serikali na inahitaji mtu makini.

Alisema licha ya umakini wa mtu, pia anatakiwa atoke chama makini na awe amepimwa na kuonekana anafaa kwa kazi hiyo na kamwe siyo ya kutolewa kwa kila aiombaye kama majaribio.

Kuhusu hoja kwamba mgombea huyo wa Chadema ameshika nyadhifa kadhaa ikiwemo ya ubunge wa Karatu, Wasira alisema mbunge hakumaanishi kuwa unafaa kuwa rais kwani ubunge ni uwakilishi na wala siyo utendaji.

“Ndugu wananchi ubunge siyo utendaji, ni uwakilishi tu. Unazidiwa na utendaji wa kijiji na kata ndio maana hawa wanaamua kesi mbalimbali tofauti na mbunge, na unaweza kukaa bungeni muda wote wewe ni kusinzia tu,” alisema Wasira.

Akimwelezea Kikwete, Wasira alisema mgombea huyo amejaribiwa kupitia nyadhifa mbalimbali za kiutendaji ndani na nje ya chama ukiwamo uwaziri katika wizara za Maji, Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na pia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Alisema, katika miaka mitano ya Rais Kikwete madarakani, ameiwezesha nchi kung’ara katika medani za kimataifa huku akihifadhi amani, utulivu na mshikamano ndani ya nchi.

“Huyu ndiye rais anayefaa. Amejaribiwa kwa nyadhifa mbalimbali na zote alifanya vizuri. Hata tulipomkabidhi nchi mwaka 2005 ameiwezesha kubakia katika hali yake ya amani na utulivu. Tumpe kura zetu,” alisema.

Utitiri haumnyima Jogoo Usingizi wewe! Kwanza huyo unayemzungumzia ameshapitwa na wakati Mtu anasura kama Goti asituletee siasa zake za maji taka! Usidanganye watanzania Wasira Watanzania wa sasa hivi sio wale mliokua mnawadanganya subirini Tarehe 31 mtajua kati ya yai na kuku ni kipi kilianza!
 
Dr. Slaa is playing loose with the facts...playing loose with facts ndio njia ya kistaarabu kusema "mtu ni mwongo"

cement 5,000/=, alipita na helikopta musoma akasema bwawa kubwa la maji la mifugo, kasema hilo lingejengwa kwa sh. Mil 35 tu...unajuaje kutoka juu gharama ni ndogo, populism ya kupandisha hisia za watu masikini..akiulizwa cv, kujitetea tu..

Oh, mbona obama, oh mbona kabila hakuwa na experience, oh nyerere aliingia wakati wa uhuru.. Kuweka slaa is not equal to obama, nyerere, kabila...hakuna achievement ya kumpeleka katika medani hiyo..bado na ndio miaka 62 na mchumba wake anayempenda wataoana ikulu mwakani...tumchangie harusi ya Slaa, ila akishindwa kutueleza uwezo wake kindakindaki, sio lazima urais wa Nchi hii, mwaka huu..Bado hajajibu hoja Mhe. Slaa..Sisi ndio waajiri wake, sisi ni waTZ
 
Mzee huyu si anatakiwa apumzike alee wajukuu zake sivyo? miaka 75 una mawazo gani mapya na kutuambia sisi? - tunaomba unyamaze tafadhali.
 
Nlisikia mkulu akisema miaka-5 ilikuwa ya kujifunza..
Sasa "uzoefu" unasaidia nini kama huo muda alikuwa akijifunza... na umaskini wetu ndo unazidi shika chati..
 
mzee huyu si anatakiwa apumzike alee wajukuu zake sivyo? Miaka 75 una mawazo gani mapya na kutuambia sisi? - tunaomba unyamaze tafadhali.

miaka 75 ya babu yako...you my friend, are playing loose with the fact(mwongo wewe)!! Like dr. Slaa, angalia website ya bunge, stephen masatu wassira kazaliwa mwaka 1945, dr. Slaa 1948...kizazi hicho hicho tu!! Wasira mchumi, slaa paroko.

Sasa nani ana mawazo zaidi kitaaluma...sio kubwabwaja tu!!
 
Salutation Honourable
First Name: Dr. Wilbrod
Middle Name: Peter
Last Name: Slaa
Member Type: Constituency Member
Constituent: Karatu
Political Party: CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
Office Location: P.O. Box 119, Karatu - Arusha
Office Phone: +255 784 666995
Ext.:
Office Fax: +255 22 2668866
Office E-mail: wslaa@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Start Date: 28 December 2005
End Date: 30 August 2010
Date of Birth 29 October 1948

EDUCATIONS
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980 1981 ADV DIPLOMA
TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985 1985 CERTIFICATE
Kwermusl Primary School(Mbulu) Primary Education 1958 1960 PRIMARY
Daudi Primary School Primary Education 1961 1961 PRIMARY
Karatu Primary School Primary Education 1962 1965 PRIMARY
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966 1969 SECONDARY
Itaga Seminary School A-Level Education 1970 1971 HIGH SCHOOL
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972 1973 CERTIFICATE
St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977 1981 PHD
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974 1977 CERTIFICATE
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993 1993 CERTIFICATE



EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Tanzania Society for Blind Managing Director 1992 1998
Tanzania Episcopal Conference Secretary General 1985 1991
Diocese of Mbulu Development Director 1982 1985
Diocese of Mbulu Vicar General 1982 1985
Diocese of Mbulu Development Director 1977 1979
Diocese of Mbulu - Roman Catholic Church Padre 1977 1991
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
CHADEMA Secretary General 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu Constituency) 1995 Todate
CHADEMA Member of National Executive Committee 1995 -
Chama Cha Mapinduzi - CCM Secretary Foreign Branch(Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977
PUBLICATIONS
Description Published Date
No items on list

SPECIAL SKILLS
Skill Name or Description Years Experience Acquired Through Skill Level
No items on list

RECOGNITIONS
Recognition Type Recognition Date Reason Action Taken Issued by
No items on list


CV YA SLAA HIYO HAPO!!!!!
 
Salutation Honourable
First Name: Stephen
Middle Name: Masatu
Last Name: Wasira
Member Type: Constituency Member
Constituent: Bunda
Political Party: CHAMA CHA MAPINDUZI
Office Location: P.O.Box 9153, Dar es Salaam
Office Phone: +255 754 447064
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: swasira@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Start Date: 28 December 2005
End Date: 30 August 2010
Date of Birth 1st July 1945

EDUCATIONS
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Bariri Primary School Primary Education 1956 1959 PRIMARY
Nyambitilwa Middle School Primary Education 1960 1961 PRIMARY
Kisangwa Middle School Primary Education 1962 1963 PRIMARY
British Tutorial College O-Level Education 1964 1968 SECONDARY
American University Washington DC BA Economics & International Studies 1982 1986 GRADUATE
American University - Washington DC Masters of Public Administration (MPA) 1985 1986 MASTERS DEGREE
American University - Washington DC MA (Applied Economics) 1993 MASTERS DEGREE


EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Ministry of Agriculture, Food Security and Co-operatives Minister 5/12/2008
Parliament of Tanzania Member of Parliament - Bunda Constituency 2005 2010
Prime Minister's Office - Regional Administration & Local Govt. Minister 2/13/2008 5/12/2008
Siza Cold Storage Co. Ltd Managing Director 1996 2005
Parliament of Tanzania Member of Parliament - Bunda Constituency 1995 1996
Coast Region Regional Commissioner 1990 1992
Ministry of Agriculture and Livestock Development Minister 1989 1990
Ministry of Local Government Co-operatives and Marketing Deputy Minister 1987 1989
Plenpotential Embassy of Tanzania - Washington DC Minister 1982 1986
Mara Region Regional Commissioner 1975 1982
Ministry of Agriculture and Livestock Development Junior Minister 1973 1975
Parliament of Tanzania Member of Parliament - Mwibara Constituency 1970 1975
Community Development Assistant 1965 1967
Ministry of Agriculture, Food Security and Co-operatives Minister 10/17/2006 2/8/2008
Ministry of Water Minister 1/1/2006 10/16/2006
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Tanganyika African National Union - TANU District Executive Secretary 1967 1973

CV YA WASIRA HIYO HAPO!!! YEYE NA SLAA WOTE WALIKUWA TANU, CCM...NI KAZAZI HICHO HICHO..SASA MAWAZO MAPYA KUTOKA KWA SLAA KULIKO WASSIRA YANATOKA WAPI...CV YA MGOMBEA NI DINI, DINI, DINI TU AMBAYO SIDHANI NI SIFA KIUTENDAJI WA SERIKALI
 
Tatizo kubwa hapa ni uelewa mdogo wa watanzania, asingekuwa na sifa si wangemnyima hizo fomu za kugombea urais. Hii ina maana kuwa CV yake inamruhusu kuingia ikulu, anachohitaji hapa ni baraka za wananchi tu, unaye bwabwacha tu ni sawa na mfa maji/ au debe tupu ambalo mwisho wake unafahamika
 
Hata dereva wa basi la abiria aliye na uzoefu kuna siku ndio alikuwa anaanza, abiria wake wakamwamini na akawafikisha walipokuwa wanakwenda.
 
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Bunda mkoani Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amewaomba wapiga kura jimboni humo kutompigia kura mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa kwa madai kuwa hana uzoefu wa uongozi.

Wasira amesema, kama wakimpigia kura Dk. Slaa ni sawa na kumkabidhi dereva anayejifunza gari, usukani wa basi la abiria.

Badala yake Wasira ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, (Nec) amewataka wapiga kura hao kumpatia kura nyingi za ushindi mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete kwa kuwa ni dereva makini aliyehitimu mafunzo yote aliyeiendesha nchi kwa usalama katika miaka mitano iliyopita.

Akihutubia mkutano wa kampeni za CCM juzi kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Bukama na
Nyabehu, Wasira alisema tofauti na Kikwete, Dk. Slaa hajawahi kushika nyadhifa zozote za kiutendaji ambazo zinaweza kutumika kushawishi watanzania wamchague kushika mamlaka makubwa ya kiutendaji.

"Slaa huyu hajawahi kushika wadhifa wowote ule wa kiutendaji, hata uofisa utendaji wa kijiji ili tumwone anavyoamua mashauri mbalimbali yanayomfikia. Leo tumpe kura za urais?

Tumechanganyikiwa yaani tumpe ‘learner' gari la abiria! Akiwaangusha nani alaumiwe? Mnyimeni kura," alisema Wasira.

Wasira ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika alisema nafasi ya urais ipo ya juu zaidi katika muundo wa serikali na inahitaji mtu makini.

Alisema licha ya umakini wa mtu, pia anatakiwa atoke chama makini na awe amepimwa na kuonekana anafaa kwa kazi hiyo na kamwe siyo ya kutolewa kwa kila aiombaye kama majaribio.

Kuhusu hoja kwamba mgombea huyo wa Chadema ameshika nyadhifa kadhaa ikiwemo ya ubunge wa Karatu, Wasira alisema mbunge hakumaanishi kuwa unafaa kuwa rais kwani ubunge ni uwakilishi na wala siyo utendaji.

"Ndugu wananchi ubunge siyo utendaji, ni uwakilishi tu. Unazidiwa na utendaji wa kijiji na kata ndio maana hawa wanaamua kesi mbalimbali tofauti na mbunge, na unaweza kukaa bungeni muda wote wewe ni kusinzia tu," alisema Wasira.

Akimwelezea Kikwete, Wasira alisema mgombea huyo amejaribiwa kupitia nyadhifa mbalimbali za kiutendaji ndani na nje ya chama ukiwamo uwaziri katika wizara za Maji, Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na pia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Alisema, katika miaka mitano ya Rais Kikwete madarakani, ameiwezesha nchi kung'ara katika medani za kimataifa huku akihifadhi amani, utulivu na mshikamano ndani ya nchi.

"Huyu ndiye rais anayefaa. Amejaribiwa kwa nyadhifa mbalimbali na zote alifanya vizuri. Hata tulipomkabidhi nchi mwaka 2005 ameiwezesha kubakia katika hali yake ya amani na utulivu. Tumpe kura zetu," alisema.

Wasira haijui CV ya Dr. Slaa http://www.parliament.go.tz/bunge/mpcv.php?vpkey=254
 
Tafadhali, habari ya Mwaka Sitini na Moja dunia hii ya leo jamani..Dr. Slaa ni mlipua mabomu, Hana Track Record Tujue atatupeleka Wapi TZ.. MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI...TYSON NI SAHIHI HAPA: CV YA UTENDAJI WA SLAA NI MUHIMU SANA TZ..USHABIKI ASIDE!

Kwani Obama alikuwa na track record gani
 
Alikua anauza samaki pale siza cold,msasani njaa kali sasa anapiga debe la unafiki.kwani slaa hakua mbunge miaka 15?! nenda karatu kama utalinganisha na Bunda.huna maana wewe Wasira umeweka macho tu ovyo kabisa
 
Wote walianzia huko KWENYE ulearner hakuna mtu alizaliwa na post ya kuongoza!!!. learner mara nyingi ni makini na havunji sheria. ataendesha kwa makini kuwafikisha abiria salama.
 
Ndio Hisia + Pumba...Dr. Slaa hasemi atafanyaje mfuko wa Cement uwe Tsh. 5,000/=.. Show us experience aliwahi kufanikisha hilo wapi, lini?

Perform a task so we can know your capable of achieving..Otherwise, Mageuzi Tanzania bado kama Dr. Slaa is one of TZ best..more info please

WasiraSteve(1).jpg


Wasira anahitaji matibabu ya akili
 
Hakuna rais yeyote duniani aliyetoka chama cha Upinzani akaanza na Uzoefu anaotaka huyu Wasira - HAKUNA. Huo Uzoefu ataupata wapi ikiwa chama kimoja kimeshika madaraka muda wote ili hali viongozi pia wanatoka chama hicho.
Jamani msiwe na mawazo ya Kikumunist yale yanayolenga chama kimoja basi. Hadithi za bila CCM haiwezekani ni akili ya Kikomunist. Na ndio maana mnasita hata kumsifia Kagame kwa kazi nzuri alofanya kwa sababu ni aibu kwenu kuona mtu kaja majuzi tu kabadilisha kabisa uchumi wa Rwanda..

Udereva gani wa Kikwete unaosifika hali Watanzania wanajua fika kwamba sasa hivi gari letu limesha pinduka na tumewekwa kambi la msaada na vyombo vya Kimataifa. Leo hii IMF ni sawa na Red Cross kwetu hatuna hila, kila kukicha wanatupangia mikakati ya maendeleo ambayo haifanani na ahadi za Kikwete. Kikwete atawaahidi wananchi hili, kesho kinafanyika kitu kingine kabisa. Accomplishment zote za Kikwete ni kinyume cha sera na ahadi za chama kwa sababu tupo ktk kambi la misaada, bado tu mnasema JK ni dereva mzuri kutuweka bondeni tukisubiri misaada ya RedCross!
 
Back
Top Bottom