Wassira: Dk. Slaa ni kama Dereva Learner Kujaribu Ku-Drive Basi la Abiria! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wassira: Dk. Slaa ni kama Dereva Learner Kujaribu Ku-Drive Basi la Abiria!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngurudoto, Oct 8, 2010.

 1. N

  Ngurudoto JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Bunda mkoani Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amewaomba wapiga kura jimboni humo kutompigia kura mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa kwa madai kuwa hana uzoefu wa uongozi.

  Wasira amesema, kama wakimpigia kura Dk. Slaa ni sawa na kumkabidhi dereva anayejifunza gari, usukani wa basi la abiria.

  Badala yake Wasira ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, (Nec) amewataka wapiga kura hao kumpatia kura nyingi za ushindi mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete kwa kuwa ni dereva makini aliyehitimu mafunzo yote aliyeiendesha nchi kwa usalama katika miaka mitano iliyopita.

  Akihutubia mkutano wa kampeni za CCM juzi kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Bukama na
  Nyabehu, Wasira alisema tofauti na Kikwete, Dk. Slaa hajawahi kushika nyadhifa zozote za kiutendaji ambazo zinaweza kutumika kushawishi watanzania wamchague kushika mamlaka makubwa ya kiutendaji.

  “Slaa huyu hajawahi kushika wadhifa wowote ule wa kiutendaji, hata uofisa utendaji wa kijiji ili tumwone anavyoamua mashauri mbalimbali yanayomfikia. Leo tumpe kura za urais?

  Tumechanganyikiwa yaani tumpe ‘learner’ gari la abiria! Akiwaangusha nani alaumiwe? Mnyimeni kura,” alisema Wasira.

  Wasira ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika alisema nafasi ya urais ipo ya juu zaidi katika muundo wa serikali na inahitaji mtu makini.

  Alisema licha ya umakini wa mtu, pia anatakiwa atoke chama makini na awe amepimwa na kuonekana anafaa kwa kazi hiyo na kamwe siyo ya kutolewa kwa kila aiombaye kama majaribio.

  Kuhusu hoja kwamba mgombea huyo wa Chadema ameshika nyadhifa kadhaa ikiwemo ya ubunge wa Karatu, Wasira alisema mbunge hakumaanishi kuwa unafaa kuwa rais kwani ubunge ni uwakilishi na wala siyo utendaji.

  “Ndugu wananchi ubunge siyo utendaji, ni uwakilishi tu. Unazidiwa na utendaji wa kijiji na kata ndio maana hawa wanaamua kesi mbalimbali tofauti na mbunge, na unaweza kukaa bungeni muda wote wewe ni kusinzia tu,” alisema Wasira.

  Akimwelezea Kikwete, Wasira alisema mgombea huyo amejaribiwa kupitia nyadhifa mbalimbali za kiutendaji ndani na nje ya chama ukiwamo uwaziri katika wizara za Maji, Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na pia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Alisema, katika miaka mitano ya Rais Kikwete madarakani, ameiwezesha nchi kung’ara katika medani za kimataifa huku akihifadhi amani, utulivu na mshikamano ndani ya nchi.

  “Huyu ndiye rais anayefaa. Amejaribiwa kwa nyadhifa mbalimbali na zote alifanya vizuri. Hata tulipomkabidhi nchi mwaka 2005 ameiwezesha kubakia katika hali yake ya amani na utulivu. Tumpe kura zetu,” alisema.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,290
  Likes Received: 19,438
  Trophy Points: 280
  Huyu naye inabidi achambuliwe ili afunge mdomo.jk amani aliikuta kwa hiyo hakuna kitu cha kujivunia hapa.
   
 3. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni metaphor nzuri!
   
 4. M

  Mtuwamungu Senior Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watu wengine Bwana, wanabwabwaja tu! Hili jamaa nikiliangalia sura natamani kukimbia. Jitu kubwa hovyoooo!
   
 5. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Mwalimu aliposhika nchi 1961 alikuwa na uzoefu wa kutosha, na Slaa ana uzoefu zaidi ya huo.

  Poor CCM logic. Wamekosa talking points kabisa?
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Asante mwalimu mwenzangu. Nashangaa sana kuona Tanzania tunajifanya kuwa na metric ya uraisi ilhali kila kukicha nchi inarudi nyuma. Viongozi wengi wazuri wamekuwa ni wale ambao hawakuwa na rekodi za uongozi kabla ya kukabidhiwa madaraka. Watu wengi wakisha kaa madarakani muda mrefu, huwa akili zao zinaharbika.
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Mimi ninamfahamu Mzee wasira vizuri sana. Pamoja na ujasiri wake kisiasa, vile vile ni opportunist mzuri sana. Kelele hizi ni kutaka Kikwete ashinde kusudi amfikirie tena nafasi ya uwaziri.
   
 8. N

  Ngurudoto JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tafadhali, habari ya Mwaka Sitini na Moja dunia hii ya leo jamani..Dr. Slaa ni mlipua mabomu, Hana Track Record Tujue atatupeleka Wapi TZ.. MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI...TYSON NI SAHIHI HAPA: CV YA UTENDAJI WA SLAA NI MUHIMU SANA TZ..USHABIKI ASIDE!
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mwambieni aeleze sera si kulenga mtu, kwao ambao wanajifanya wanaweza uongozi nchi hii wameisaidiaje kama si kuitafuna tu!
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kwani kikwete alikuwa na cv gani?sio mnaongea tu Kama mmelewa komoni...urais unataka rekodi ya nini? Kabila alikuwa rais Kongo mpaka Leo anaongoza Kwani Ana rekodi gani?
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Alichokifanya akiwa mbunge hujakiona? poor you umefumbwa macho na mafisadi. Wanaojiita wazoefu wameisaidiaje nchi kama si kujinufaisha?
   
 12. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Kama alivyosema Mwalimu Kichuguu, viongozi wengi waliotokea kuwa bora sana duniani ni wale ambao wameingia madarakani kabla ya kukaa sana serikalini. Kwani Barack Obama si alikuwa tu Seneta kwa muda mfupi kabla ya kuwa Rais? Mbona amekuwa Rais mzuri tu?

  Dr. Slaa amekuwa Mbunge kwa miaka 15. Na uwezo wake umeonekana nchi nzima. Ndio maana wote wanampenda na watampa kura zao.
   
 13. N

  Ngurudoto JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kipi..Kafanya nini akiwa Mbunge Bwana? Utendaji wa Serikali Kuu au Serikali za Mitaa, SLAA NI STRANGER--HATA WEWE HUJUI..Hisia Hizi!!
   
 14. N

  Ngurudoto JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  uwezo ndio bado tunauliza, kupendwa anapendwa sababu anaendesha populism kwa hisia za watu masikini, unajaribu kuongea hisia bila kutaka kusema uzoefu wangu katika kutatua ni huu..the question is fair and square..

  Nafasi ya slaa kushindwa bado ipo....na kuhusu obama? Cheki kukubalika kwa mhe. Barack obama marekani kabla hujasema ni rais mzuri...check your facts jack!!!
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nimependa kigezo cha amani na utulivu kutumika kama kigezo cha uongozi na achievement ya ccm.
  Amani na utulivu vikiambatana na umaskini wa kutisha ni nothing. kama ccm walishindwa kutumia amani na utulivu kuipeleka nchi kwenye mawanda mazuri inabidi sisi wenye nchu tuikabidhi kwa CHADEMA kwa amani na utulivu kwani wana malengo chanya kwa nchi hii.
  Wanasiasa wachumia TUMBO kama wassira ni wa kupuuzwa milele.

  Mnaposema Dr. Slaa ni learner na kikwete ameshajaribiwa anafaa, kwa hiyo tulikabidhi nchi miaka mitano iliyopita kwa learner kikwete ambaye ametufikisha kwenye korongo hata rivasi haiwezi kufua dafu. dawa ni kuruhusu katapila (CHADEMA) kuinasua nchi korongoni na kuiweka kwenye njia nzuri na ya kupitika bila vikwazo
   
 16. N

  Ngurudoto JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe ni MSANII KAMA SLAA..SIJAONA POINT YA KUTUKATAZA KUOMBA EXPERIENCE (CV) YA HUYU MHE. SLAA..UCHA USANII KUPATA RAIS
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Nshasema umeamua kufumba macho usione na mi sina uwezo wa kukufumbua, baki tu na hitikadi yako but one day yes!
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,097
  Trophy Points: 280
  Mbona Barack Obama marekani ilimpa Uraisi na hakuwa anauzoefu wa kiutendaji? Hata JFK historia ni hiyo hiyo ya Obama na sasa hivi JK na CCM yake ndiyo wanamtegema Obama awanusuru kwa misaada kemkem. JK amediriki kutamka ya kuwa ahadi bila ya Obama hazitekelezeki sasa kulikoni?

  Kauli hii ya Wasira itachangia kumwongezea Dr. Slaa kura na wala siyo kuzipunguza hata punje moja......


   
 19. N

  Ngurudoto JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hisia, Hisia, Hisia Tanzania..Tuna Watu wawili, watatu Kupewa nafasi ya Urais 2010, Kupima ndio Usaili Tutumia Demokrasia..Ukitaka Kusema Nyerere na Kikwete nani Bora Kiuongozi, rekodi ya Nyerere iko viwango (sio mjadala)..

  Mfumo wetu TZ umetupa Jakaya Kikwete, Dr. Wilbroad Slaa, Prof. Lipumba...Atapewa Mtu mmoja hapo Urais, ukienda CV wise, Slaa Haitwi kwenye Usaili sababu BACKGROUND "NOT FOUND", sio kashfa, Hatujui tu..Prof. Lipumba kaomba Hii kazi ya Urais mara nne, ila ataitwa kwenye Usaili aliwahi kuwa Mshauri wa Rais wa Uchumi. nae atashindwa.

  Uzoefu sio swala la Watanzania tu, Dunia Nzima huuliza Experience!! The End of the day: Busara itashinda Hisia
   
 20. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  walewalele, upupu mtupu! Ushindweeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...