EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Wassira juzi alianza mchakato wa vikao vinavyowashirikisha viongozi na baadhi ya makada wa chama hicho wa wilaya na mkoa wa Arusha, kwa kuonya kuwa "ni uhaini kuzungumzia urais wakati huu ambao Rais Jakaya Kikwete hajamaliza muda hata mwaka mmoja kati ya mitano ya awamu yake ya pili na ya mwisho ya uongozi".
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho zilisema, licha ya kuelezwa kuwa ni uhaini kuzungumzia nafasi hiyo kwa sasa, pia vijana hao waliambiwa kwamba hoja hiyo inatumiwa na watu wenye malengo binafsi kwa nia ya kuwagawa wana CCM.
Hata hivyo, inasemekana baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vijana wilayani humo wanadaiwa kufurumusha makombora mazito ndani ya kikao cha juzi wakituhumu viongozi wao kwamba ndio chanzo ya mgogoro mkoani hapa.
Mmoja wa vijana hao alinukuliwa akitoa kauli nzito mbele ya Wassira katika kikao cha juzi, akiwatuhumu baadhi ya viongozi kwamba wao ndio chanzo cha mgogoro unaofukuta huku akisisistiza kuwa wanaendeleza sera ya kutaka nchi na CCM visitawalike kwa maslahi yao binafsi.