Wassira awakana 'watoto wake' waliojiunga na CHADEMA...

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,260
7,195
Huku mzee akikuna kichwa kwa style ya kushindwa pata majibu kirahisi katika suala gumu, kapanda jukwaani kujitetea kuwa waliojiunga na CDM si wanae ni wa kaka yake.

Mzee akionekana kuchoka hakuwa na majibu ya kujiamini. Naye kaingia ktk game kama ya Mkapa.

Tusubiri kama kweli si watoto wa kuzaa, atamjibu vipi kakake kama kaona watoto wa kakake si wake.

Chanzo: TBC Habari

1st October 2012



WassiraKilimo%281%29.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, amekana kuwa watoto walijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) juzi si watoto wake wa kuzaa, bali ni watoto wa ndugu yake ambao wana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa.

Wasira amesema kwamba kutumia jina na cheo chake ni upotoshwaji mkubwa ambao umefanywa na Chadema kwa lengo la kupata umaarufu.

Wasira, alitoa kauli hiyo jana mjini Bunda katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao aliutumia kumshambulia Katibu Mkuu wa Chedema, Dk Wilibrod Slaa, kwa kumtaka awe makini.

"Wale watoto ni wa George Wasira siyo wa Stephen Wasira, hivyo kusema ni watoto wa wWziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) na mwanasiasa mkongwe katika ukoo wetu walilenga kunisema mimi. Hawa si watoto wangu wa kuzaa, bali ni watoto wa kaka angu na ni watu wazima wana haki ya kuchagua wawe katika chama gani,"alisema na kuongeza:

"Mimi sina mtoto wa kuzaa anaitwa Lilian, lakini nawajua wale Lilian namjua na Esther ni watoto wa kaka angu anaitwa George Bukore Wasira na mama yayo Wanzita, sasa habari ilitangazwa inasema ni watoto wa Stephen Wasira hii si kweli."

S
ource: Nipashe
 
daaha wakuu wassira anafunguka now anasema hao mabinti wa jana waliojiunga cdm si wake wa kuzaa, bali ni wa kaka yake.. daaha naona limemtachi sana... kwa jinsi anavyoongea source ITV
 
Asema si watoto wake ni ndungu wa ukoo wake,na kusena anawatambua kama watoto wa kaka yake

ITV HABARI
 
Amesema ni watoto wa kaka yake na wala si wake kama vyombo vya habari vilivyoripoti.SOURCE ITV HABARI
 
kwani watoto wa kaka yake si wake? AU WATOTO MAANA YAKE NI NINI?
MAANA ANASEMA KUWA SI WAKE BAALI WA KAKA YAKE NA WALA HAIKUWA HOJA KUWATANGAZA...
 
watoto ni watoto tu hana lolote, mbona makongoro hajawahi kumkana mbunge wa musoma mjini kuwa sio ndugu yake. ni vizuri wanasisa hasa WASIRA akakubali ukweli. siasa zisitengenishe undugu. watoto wa kaka ni wako, anatakiwa kuwa muungwana. hakua cha ajabu mbona yeye mwaka 1995 alijiunga na NCCR mageuzi na kuwa Mbunge wa Bunda baada ya kumshinda Warioba na alipoenguliwa na mahakama kwa madai ya kutoa rushwa aliunda chama chake ambacho kilikufa na yeye kurudi CCM.
 
siasa inapotaka kuvunja undugu!
Leo hii huyo george wassira akifariki kina ester watakimbilia kwa nani kama baba 'wassira' anawakana?
 
mbona wasira mwenyewe alikacha ccm akajiunga na nccr baadae akaanzisha chama chake. sasa kapata shavu ccm anasahau alikotoka.
Mzee mnafiki kweli huyu! Aaghaaaaaaa!
 
Back
Top Bottom