Wassira amtaka Dr. Slaa aache kuita wake za watu chumbani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wassira amtaka Dr. Slaa aache kuita wake za watu chumbani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by masopakyindi, Oct 1, 2012.

 1. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,905
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  Katika kile sasa kinachoonekana kuwa bifu kali kati ya hawa wanasiasa waili wa umri mkubwa, Waziri Wassira amemtaka Dr Slaa awe mwangalifu katka kutoa kadi za chama chake chumbani bila wadau wengine kuwapo!!

  Kulingana na gazeti la Majira leo tarehe 1/10/2012, Wassira alikuwa akijibu mapigo kwa jina lake kutumiwa na Dr Slaa katika kuwapa kadi wanachama waili wenye jina la Wassira.
  Hata hivyo Nd Wassira alisema ndugu zake hao ambao ni watoto wa kaka yake,Lilian na Ester Wassira wana haki ya kujiunga na chama chochote cha kisiasa.

  Ni kinukuu gazeti la Majira la leo, lina sema:

  " Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Bunda,mkoani Mara, Bw Wassira alimshukia Dr Slaana kumtaka awe makini kuwaita wake za watu chumbanina kuwapa kadi bila maofisa wengine wa chama hicho kushuhudia tukio hilo."

  Wassira aliendelea,

  "Namtahadharisha Dkt Slaa kwani alichokifanya kinaweza kuleta mtafaruku katika ndoa za watu"

  Wana bodi hili bifu sasa ni kali, lakini namii niliona lile jicho alilolikata yule binti mdogo mdogo kwenye TV, lilikaa kimahabuba, sijui pengine macho yangu.
  [​IMG]
  Nawapongeza CDM kwa kupata wanchama wazuri hivyo.
   
 2. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii ni kali aisee.
   
 3. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Laana ya mzee Ndege itamtafuna milele!:A S 39:
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ofisini ni Chumbani? na alitaka awakabizie kwenye ukimbi wa Idala ya habari maelezo?
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa YEYE alikuwa anakatiwa BIMA chumbani basi anadhani watu wote kama YEYE?
   
 6. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  picha tulizoziona katika vyombo vya habari zilipigwa na nani? Wassira bhana ana pumba yaani mpaka anakera sijui huko serikalini anafanya kazi gani!!!
   
 7. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  I dont think there's a way more personal it can get rhan this!
   
 8. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  wasira anatapatapa..........kama anaweza basi awakane hadharani!!..kashasema kwamba hao ni watu wazima wana uhuru wa kuchagua chama chochote akasahau kuwa wana uhuru pia wa kuichukulia iyo kadi popote..iwe gest au Maelezo that is non of wasira's business!!
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Wassira amechanganyikiwa rasmi na wala siwezi kumlahumu ana hitaji huangalizi wa karibu!

  Kama ofisi yeye ana iona ni chumba kwa hiyo ni ushahidi tosha kuwa wassira amechanganywa na wale watoto wake!

  Yan mtu mzima ana wakana watoto wa kaka yake wa damu alaf tutegemee kuwa haumwi!

  Haiitaji kuwa Dr kujua tatizo la wassira
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  hahahhahaha
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Umeleta mada vizuri lakini mwisho na wewe umevaa tabia za wassira!

  Hakuna kulala mpaka kieleweke!


   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Haaaahaaaa! nani alifanya mapinduzi kumrudi mwenzake? Gati?
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Mimi naona ni ofisini.........sijui ''chumbani'' anakokuongelea ''PET'' WASSIRA ni wapi?

  [​IMG]
   
 14. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,905
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha
  Mkuu Ruta, TV wote tuliona, sio uongo ,hata kama ni mke wa mtu yule mdogo wallah, nampa zote marks.
   
 15. A

  Ankara Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  At least the old man should show some respect to his daughters. Its typical non-African to utter such remarks concerning his daughters, a fact he cannot deny.
   
 16. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,682
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Huyu mpuuzi nini, Kwani Dr adindishi?!


   
 17. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Na Mwandishi Wetu, Bunda na Dar

  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Bw. Stephen Wassira, amesema

  kitendo cha Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibrod Slaa kutumia jina na cheo chake wakati akiwapa kadi wanachama hao ni upotoshaji unaofanywa na CHADEMA ili kujipatia umaarufu.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Bunda, mkoani Mara, Bw. Wassira alimshukia Dkt. Slaa na kumtaka awe makini kuwaita wake za watu chumbani na kuwapa kadi bila maofisa wengine wa chama hicho kushuhudia tukio hilo.


  "Namhadharisha Dkt. Slaa kwani alichokifanya kinaweza kuleta mtafaruku katika ndoa za watu, Lilian na Esther ni watoto wa kaka yangu George Wassira si mimi, hawa ni watu wazima na wote wana haki ya kuchagua chama wanachokitaka," alisema.


  Aliongeza kuwa, Dkt, Slaa anaishi kwa kutafuta matukio bila kutumia akili ambapo mume wa Bi. Lilian ni mwanachama wa CHADEMA hivyo uamuzi aliochukua mkewe hauna uhusiano wowote na ukoo wao.


  "Hata Makongoro Nyerere awliwahi kujiunga NCCR-Magezui wakati hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (baba yake), akiwa hai, je, tatizo lilikuwa wapi na yeye ni mtu mzima," alisema.


  Alisema siku zote Dkt. Slaa na viongozi wengine wa CHADEMA wamekuwa wakichukizwa na jinsi anavyojibu hoja zao hivyo wanachokifanya ni kumtafutia tuhuma lakini wameshindwa kufanikiwa hivyo wamezna kuwachonganisha katika ukoo.


  "Wanachukizwa ninavyojibu mambo yao hasa wanayosema katika majukwaa na kuhatarisha amani, mimi ni mzalendo wa kweli ambaye nalitumikia Taifa lengu kikamilifu na sina tuhuma za ufisadi ambao Dkt. Slaa ameufanya kuwa wimbo," alisema.


  Hata hivyo, aliwataka Watanzania waelewe kuwa ukoo wao msingi wake si vyama vya siasa bali kila mtu ana haki ya kuingia na kutoka katika chama chochote.


  Alisema kitendo cha Dkt. Slaa kuhusisha ukoo huo na tukio la watoto hao kujiunga CHADEMA ni kuwadanganya Watanzania kuwa ukoo huo umegawanyika jambo ambalo si kweli.


  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP) Taifa, Bw. Fahmi Dovutwa, naye amemshukia Dkt. Slaa kutokana na kauli yake kuwa CCM kinakufa.


  Bw. Dovutwa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.


  Alisema hivi karibuni, gazeti moja (si Majira), lilimnukuu Dkt. Slaa akisema CCM kimeonesha kila dalili ya kufa baada ya kushindwa kuwaengua wagombea wawili (aliowaita watuhumiwa wa ufisadi), katika nafasi walizowania ndani ya chama hicho.


  Wagombea hao ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge ambaye amepitishwa kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.


  Mwingine ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa, ambaye chama chake kimempitisha kuwania ujumbe wa NEC, Wilaya ya Monduli, mkoani Manyara.


  "Kauli ya Dkt. Slaa imenishangaza na imevitia doa vyama vya upinzani, yeye hakupaswa kuihadarisha CCM ili isianguke katika Uchaguzi Mkuu 2015, nilitegemea afurahie chama tawala kianguke ili CHADEMA kiingie Ikulu.


  "Kutokana na kauli yake, inaonesha CHADEMA kinamuogopa Bw. Lowassa ambaye kama ataamua kugombea Urais 2015, Dkt. Slaa anaamini chama chake hakitafurukuta," alisema.


  Alisema Dkt. Slaa aliamua kuondoka CCM mwaka 1995 na kuhamia CHADEMA ili akajifariji baada ya jina lake kuenguliwa katika kura za maoni mwaka hivyo bado ana mapenzi na chama tawala ndio maana anawajibika kukipa ushauri.


  "Ni wazi kuwa Dkt. Slaa hajui chochote kuhusu haki za binadamu kwani katiba ya nchi ya mwaka 1977 ibara ya 13 (6) (b), inasema ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hadi itakapothititika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo," alisema Bw. Dovutwa.


  Alisema kwa mujibu wa kifungo hicho pamoja na Dkt. Slaa kuwataja mafisadi katika Viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam, hapaswi kuendeleza tuhuma dhidi yao kwani yeye si polisi, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), wala mahakama.


  Bw. Dovutwa alisema inaonesha baada Dkt. Slaa kutoa tuhuma hizo, yeye ndie aliyefanya uchunguzi, kuandaa kesi na kuwatia hatiani.


  "Madai ya Dkt. Slaa kuwa kabla hajaondoka bungeni alimwambia Bw. Lowassa kwamba kwa vile amejiuzulu Uwaziri Mkuu kwa madai ya kuwajibika, ina maana alikuwa anamjua aliyesababisha achukue uamuzi huo hivyo alimtaja amtaje ili wamsafishe na kushindwa kumtaja ni siasa za kutishiana ambazo hazina tija.


  "Kwa kauli hiyo, baada ya Bw. Lowessa kukataa kumtaja, anachokifanya Dkt. Slaa ni siasa za chuki ambazo haziwezi kukubalika hata kidogo kwa masilahi yake," alisema.


  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu ili kujibu madai hayo, Dkt. Slaa aliangua na kusema kuwa " Mimi sitaki kujibu, waulize waliokuwepo wakueleza kama tulikuwepo peke yetu".


  "Wewe ulikuwepo? alihoji Dkt. Slaa akimuuliza mwandishi wa wetu na baada ya kujibiwa hakuwepo, alisema atafutwe aliyekuwepo ili azungumzie ukweli wa madai hayo.


  Akizungumzia madai ya Bw. Duvutwa, alisema kiongozi huyo wa UPDP si saizi yake. "Siwezi kujibizana na mtu ambaye hana hata Mwenyekiti mmoja wa mtaa...nijibizane naye nini? kibinadamu sina sababu ya kumjibu," alisema Dkt. Slaa.

  chanzo:Gazeti la Majira
  http://majira-hall.blogspot.com/2012/10/wassira-sasa-amlipua-slaa-amtaka-aache.html#more
  Leo Tar.01/10/2012
  Nawasilisha

   
 18. m

  mamajack JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wasira hajui tofauti ya chumbani na ofisini maana kila sehemu yeye ni kusinzia tu,kwahiyo tusimlaumu ndivyo ajuavyo.
   
 19. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Kuna watu labda hamumfahamu vizuri Wassira, ni kwamba Wassira alipigika na maisha ile kisawasawa, sasa wakati JK ankwenda kuomba baraka kwa mama Maria Nyerere, Maria Nyerere alimwambia nakubali mwanangu uwe Rais ila usimuache Wassira anaadhirika.

  Wengi hili hawalijui ila kwakuwa JF ni mkusanyiko wa watu wengi najuwa wapo watakaothibisha maneno haya, Wassira mpaka leo nina uhakika hawezi kukosa sugu kwenye bega lake la kulia maana baada ya kupigigika na maisha ilibidi awe mbeba mabegi ya mawakili ili na yeye apate pesa ya kula. kwahiyo sishangazwi na lolote kutoka kwa Wassira.
   
 20. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wassira alimtenda akajitwali mutoto! Halafu mkuu itabidi tuongee fresh mbona ID yako inafanana na
  Jina la babu yangu
   
Loading...