Wasovieti walitoa AK 47 nao Wamarekani wakatoa M16-bunduki hizi zinatofautiana vipi?

Sipo hapa kubishana Leta data alijiunga na jeshi mwaka gan na mwaka gan alianza harakat zake za kukamilisha AK 47 ninayo mahujiano yake yapata miaka michache tu tokea afarik ajafarik kitambo
Kuna movie inahusiana na hii story,inaonesha alikua nwanajeshi na kama aliumia mkono vitani,ndio akarudi na kupata muda wa kutengeneza hii kitu,sikuangalia movie yote.
 
Kwa msaada wa bbc
AK-47 na M16 ni bunduki mbili kati ya zinazotumika sana ulimwenguni.Mizozo mingi ya kivita hasa barani Afrika imehusisha matumizi ya bunduki hizi na hata sasa katika sehemu zinazoshuhudia machafuko kama vile nchini Msumbiji,Somalia na Jamhuri ya kati mwa Afrik bunduki hizi zipo mikononi mwa waasi,wanajeshi au polisi.
Mjadala wa ulinganishi wa bunduki hizi umefufuliwa maajuzi katika machafuko yaliyoshuhudiwa eneo la Laikipia nchini Kenya wakati maafisa wa utawala walipolalamika kwamba wavamizi walikuwa wamejihami kwa bunduki za kisasa kama M16 kuliko maafisa wa polisi waliokuwa wakitumia bunduki kama G3.
Silaha zote mbili zilipata umaarufu kwa kuwa bunduki za kawaida za kushambulia zilizotumiwa mtawaliwa na wanajeshi wa Soviet na Marekani wakati wa Vita Baridi.
Uwepo wa silaha hizo kila mahali leo hii, yaani kwa wanajeshi, polisi, vikosi vya usalama, wanamapinduzi, magaidi, wahalifu, na hata raia kunafanya silaha hizo kuwa gumzo na mara kwa mara kulinganishwa.

Wasovieti walitengeneza AK-47 muda mfupi baada ya Vita vya Pili vya Dunia.
Silaha hiyo iliundwa kwa msisitizo juu ya nguvu yake, matumizi rahisi, gharama za chini za utengenezaji na ya kutegemewa kulingana na mafundisho ya jeshi la Soviet.

Mwanzoni mwa miaka ya 1950, ilikuwa imeanza kutumika pakubwa katika Jeshi Jekundu la Urusi.
Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Jeshi la Marekani hapo awali lililenga utengenezaji wa silaha ambazo zinalenga ufyatuaji wa risasi moja kwa moja, na kupelekea kuundwa kwa M14.
Hadi kufikia Vita vya Vietnam, silaha za AK-47 na M14 zilikuwa zinashindana, upungufu katika udhibiti na ubora wa makali ya silaha hizo kulisababisha hitaji la mbadala wa M14 ambayo, kupitia safu ya maboresho, mwishowe kuliundwa bunduki aina ya M16.

Muundo​

AK-47 ni bunduki ya rashasha, inayotumia risasi za ukubwa wa 7.62x39mm.
Inategemea kupozwa joto na hewa na inatumia pistoni ndefu zinazotegemea skrubu inayozunguka.
Iliundwa kuwa bunduki rahisi na ya kuaminika ya kufyatua moja kwa moja ambayo ingeweza kutengenezwa haraka na kwa bei rahisi, ilitumia njia za uzalishaji kwa wingi ambazo zilijumuisha teknolojia ya kisasa wakati huo katika Umoja wa Kisovieti mwishoni mwa miaka ya 1940.
Kwa upande mwingine, M16 ni bunduki ya rashasha, inayotumiwa risasi za ukubwa wa 5.56x45mm.
Inatumiwa kupoza hewa na kuingiza gesi moja kwa moja, na skrubu inayozunguka na muundo wake unaegemea nguvu inayotoka moja kwa moja risasi inapofyatuliwa.
Iliundwa kimsingi kuwa bunduki nyepesi, na kufyatua risasi mpya ndogo nyepesi, yenye kasi kubwa ili kuwezesha watumiaji kubeba risasi zaidi.

Risasi​

Risasi za ukubwa wa 7.62x39mm zinaongeza uzani zaidi wa AK-47 na kupenya zaidi ikilinganishwa na M16.
Tofauti kati ya AK-47 zinazotumia vipokezi ambavyo hufyatuliwa kwa kukandamizwa au vipokezi ambavyo muundo wake umepinda vinasemekana kuwa na usahihi zaidi huku bunduki za AK-47 zenye vipokezi vinavyofyatuliwa ni kama mtu anapiga muhuri au stempu na zinaonekana kuhimili zaidi uchovu wa chuma.
Risasi ya ukubwa wa 5.56x45mm inaipa bunduki ya M16 umbali mzuri na shaba sahihi ikilinganishwa na AK-47. Nguvu yake, kasi yake na njia yake ya ufyatuaji wa bapa inaruhusu mpigaji risasi kuwa sahihi zaidi katika shaba zao kuliko AK-47.

Mtutu​

Mtutu wa AK-47 una urefu wa 415 mm, wakati M16 mtutu wake ni urefu wa wastani wa 508 mm.
AK-47 ni bunduki inayoendeshwa na gesi pamoja na skrubu inayozunguka kila upande
M16 inafyatuliwa haraka moja kwa moja au bunduki yenye skrubu inayozunguka.

Chombo cha kushikilia risasi​

Chombo hiki katika bunduki aina ya AK-47 kina umbo lililopinda na huwekewa risasi.
Ni kizito sana na cha chuma na kikowazi "kama midomo" kuifanya iwe sugu dhidi ya uharibifu.
Chombo cha kuweka risasi cha M16 kiliundwa kuwa chepesi zaidi na cha kudumu kwa muda tu. Kimetengenezwa kwa alumini iliyokandamizwa na sehemu yake iliyo "kama midomo" ni dhaifu ikilinganishwa na AK-47.

Uzito​

Ni kati ya kilogramu 3.26 na 4.0, huku M16 ikiwa nyepesi zaidi chini ya kilogramu 4.3.

Mazingira​

Usalama wa AK-47 imeundwa kufyatuliwa kwa urahisi na kidole cha shahada huku kidole cha kati kikibaki kwenye kichocheo.
Chombo cha kuwekea silaha kinaingizwa na kuondolewa kwa mwendo rahisi wa kutikisa.
AK-47 ni ya kupendeza sana na rafiki kwa watumiaji wa mkono wa kushoto katika suala la udhibiti na kuondolewa kwa risasi.
Kitufe cha kuhakikisha usalama wa bunduki aina ya M16 kinaweza kubadilishwa bila kupoteza mwelekeo wa unacholenga.
Lakini udogo wake unafanya iwe vigumu zaidi kutumia silaha hiyo ukiwa na mawazo. M16 sio rafiki kwa watumiaji wa mkono wa kushoto katika udhibiti na kutolewa kwa risasi.

Inaweza kutegemewa kwa kiasi gani?​

AK-47 inajulikana kwa ugumu wake na uthabiti. Ina kiwango cha utendakazi wa raundi moja kati ya 1000 iliyofyatuliwa na imeundwa kwa njia ambayo hata watu wasio na mafunzo wanaweza kuitumia. Pia imeundwa kwa namna ambayo inaweza kufanya kazi katika mazingira machafu na maboresho kidogo. Mbinu hii ina imarisha uthabiti wa AK kwa usahihi wake.
Na sifa ya mapema ya ukosefu wa kuaminika, M16 ina takriban mara mbili kiwango cha utendakazi ikilinganishwa na AK-47, kwa raundi mbili za ufyatuaji wa mara 2000.
Ubunifu wa M16 unahitaji matumizi mengi na ya mara kwa mara ya vilainishi vinavyoendana kwenye kipokezi chake, na ukosefu wa vilainishi ndio sababu ya kawaida ya silaha hiyo kuacha kufanya kazi au kuwa na matatizo ya hapa na pale kwenye utumiaji wake.
M16 imekuwa ikiboreshwa mara kwa mara ili kuongeza muda ambao inaweza kutumika.

Huduma inayotolewa​

Muungano wa Kisovieti haukudhibiti utengenezaji wa AK-47 na sheria ya hakimiliki au hati miliki.
Kwa hivyo, AK-47 imetengenezwa katika nchi nyingi, na wazalishaji wengi, kwa viwango tofauti vya ubora.
Kwasababu hii, huduma inayotolewa na AK-47 inaweza kuwa kati ya takriban raundi 6,000 hadi 15,000.
Imeundwa kama silaha rahisi, ya bei rahisi, na utengenezaji rahisi, mara nyingi ni rahisi kupata bunduki nyengine aina hii kuliko kuifanyia marekebisho kama imeleta matatizo katika utenda kazi wake au kuharibika.
M16, kwa upande mwingine, imetengenezwa kwa viwango vya juu ambavyo huruhusu kutumika kwa kuanzia raundi 20,000 hadi 50,000 kwa zilizoundwa na vipokezi vinavyotumika kwa kukandamizwa pale kwenye mtutu.
Tofauti na AK-47, M16 ilitengenezwa kutoa huduma na pia inaweza kufanyiwa marekebisho na maboresho.
Kwa AK-47 na M16, sehemu ndogo zinahitaji kubadilishwa katika kila raundi elfu kadhaa za ufyatuaji.

Bei ya AK-47 v M16​

Ingawa kuna aina nyingi zinazopatikana za bunduki zote mbili, wakati wa kulinganisha muundo, AK-47 ni ya bei rahisi kuliko M16.
Bei ya serikali ya AK-47 inaweza kuanzia $ 150 hadi $ 200, kulingana na mtengenezaji na mkataba.
Bei ya serikali ya M16 ilikuwa $ 673 kwa kila mpya kulingana na mkataba wa Jeshi la Marekani wa mwaka 2012.View attachment 1953568View attachment 1953569
Hii si ndio ile ya Hamza??
 
Mtoa mada una nafasi yako mlango wa jehanamu.

Unaielezea hii kitu kana kwamba una tenda ya kusaplai bana
 
Sahihi
Hiyo AK 47 imeua sana watu Duniani kama wangefanya tafiti na zimezagaa sana kwa Nchi zisizo na sheria kali kuhusu siraha hapo Somalia unakuta chalii tuu anazo mbili huku anaenda kufata tende zake sita dukani..
 
AK 47 haikuundwa na jeshi Bali iliundwa na jamaa flan Hiv mrussi kwakuwa kilikuwa kipind cha ujamaa ikabid imilikishwe kwa jeshi na muhusika akaingizwa kwenye jeshi muundaje alishafariki ila enzi za uhai wake alijutia Sana kutengeneza hii bunduki alijutaa Sana alifariki akiwa hana kitu kabisa hiii bunduki haikumnufaisha yeye
Alikua mwanajeshi mwenye cheo cha Luten akiitwa Armat K... kabla ya kuibuni alijeruhuwa vitani akiwa.kwenye kifaru
 
Back
Top Bottom