Wasomi wetu wamekuwa mwiba kwetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi wetu wamekuwa mwiba kwetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by spencer, Feb 14, 2012.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,
  Nina jambo la kusema linaniumiza kichwa kwa baadhi ya wasomi tuliowaamini na kuwapa dhamana ya uwakilishi.

  Wanajitahidi kutumia usomi na utaalamu wao kuumiza vichwa ili mikataba yote mibovu inafungamanishwa wasihojiwe huku wakijua inaumiza hata watanzania ambao watazaliwa baada 2050.

  Wenzetu wasomi wao wanatumia utaalamu kujenga taifa baada ya miaka 50 ijayo

  Wanahakikisha miradi yote yenye mazabe inaanza na kukamilika na kukabidhiwa na kukubaliwa hata kama iko chini ya kiwango kipindi wao wakiwa madarakani.
  Miradi yote ya kudumu wenzetu inakuwa ya muda mrefu, kila kiongozi anakuja kukamilisha phase yake

  Wanahakikisha wamefungua accounts ktk mabenki ya ulaya ili tusiwachungulie, Kisha pesa hizo hizo zinatumika kukopesha nchi yetu kwa riba kubwa.
  Matajiri wote wanafungua accounts ktk mabenki ya kwao na kuwekeza ndani ya nchi yao

  Wako tayari kuliweka Taifa rehani kwa kucheza na Nishati (Mafuta na Umeme) huku wakijua wazi ukipandisha bei ya kimojawapo au vyote basi kila kitu kinapanda bei, wao hawajali ili mradi wameahidiwa Suti mpya na kupelekwa ktk mahotel yaliyo na viwanja vya kutua helkopta ghorofani.
  Wenzetu hawako tayari kuumiza wananchi Umeme na mafuta ni kipaumbele cha kwanza ili kushusha gharama ya maisha na gharama ya bidhaa zalishwa. Wanahakikisha exports zao zinafidia nafuu inayotolewa kwa wananchi wao

  Wawekezaji wageni wanapewa kipaumbele cha misamaha ya kodi huku wakiruhusiwa kubadili majina ya mahotel,makampuni yao ili kukwepa kodi
  Wazawa wana kipaumbele cha kipekee na kupata misamaha ili miradi yao ifanikiwe.

  Makampuni ya kigeni (mfano Madini) kupewa umiliki 100% kwa zaidi ya miaka 90 huku taifa likiambulia 3% ya faida. Kigezo kinachotumika ni kuwa Tanzania haina mtaji ili kuwa na Share ktk hizo kampuni
  Wenzetu wao wanasema kilichoko chini ya ardhi ndiyo Share tena 50%, mgeni njoo na mitambo pamoja technolojia yako lakini tunagawana 50/50


  Yako mengi yanayonikera kwa hawa mbwa mwitu wanaojifanya kondoo. Kwa kiasi kikubwa mabaya haya yote yanafungamanishwa na Siasa chini ya CCM ambazo kwa sasa badala ya kulinda maslahi ya mfanyakazi na mkulima, Sera yao yao inalinda wezi na matapeli

  Hivi tuwafanye nini hawa?
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kinachotusumbua si usomi bali ufisadi uliokithiri.
  Kama unafikiri usomi ni atizo jaribu ujinga!
   
 3. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Kumbuka ni baadhi si wote.
  Lakini nadhani Uroho pia ni tatizo we unasemaje?
   
 4. K

  Kizotaka JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wasomi wa kibongo wanamikogo kitu cha kwanza, selfish na wakikutana na limfumo lilo kijambazi kama la serikali yetu ndo wanatokomea humo, wanadharau yani m2 kuwa na digrii anaona wengine wote vilaza, akipata kikazi ndo loo, hashikiki! we angalia ni wasomi wangapi wameanzisha vikundi na kuchukua mikopo na kuanzisha miradi inayotoa ajira? hakuna.! ni akina mama na malayman(ambao ndo wenye akili) wengine wa kitaa, wasomi ubinafsi na mikogo! Wanategemea vyeti na sio akili zao tena,ni kuuza vyeti kutafuta kazi mwanzo mwisho, wamekuwa brain washed, everything is planned. I was born Intelligent but education ruin me ,:Cry:
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,599
  Likes Received: 3,892
  Trophy Points: 280
  FYI

  Msomi (graduate) wengi wanaweza kuwa wenyeviti wazuri sana wa vikao vya harusi na vipaimara! wengi wao ni wakusanyaji wazuri wa michango ya Upatu....

  Nchi inajengwa na wasio wasomi.....!!

  Nionyeshe msomi mmoja nchi hii,nitakuonyesha wasio wasomi watatu bora zaidi yake!
   
Loading...