Wasomi wetu wa Tanzania wamelisaidia vipi taifa letu kutoka kwenye umasikini?

Awadh Samuel Kiwelu

Senior Member
Oct 11, 2014
192
69
Wana JF.

Tanzania toka tupate uhuru wetu mwaka 1961 mpaka leo mwaka 2015 bado nchi yetu ipo kwenye kundi la nchi masikini tunaendelea kusaidiwa na wahisani mpaka leo.

Tanzania kuna jamii tofauti tofauti bahati nzuri toka tupate uhuru jamii yetu ya Kikristo tumejaa idara zote za serikali na mashirika ya umma.

Sisi Wakirsto tumejaa idara wizara zote kama watendaji wakubwa wa serikali haya yametokea baada ya sisi Wakirsto kuwa tumesoma zaidi ya jamii ya Waislam ambao wapo wachache serikali kutokana na kutokwenda shule, sasa hivi ndiyo tunaona wanapata nafasi kidogo serikalini.

Sisi kama Wakirsto ni wasomi hivi tumelisaidia vipi taifa letu kutoka kwenye dimbwi la umasikini kupambana na ufisadi.

Tukiangalia ufisadi unaoendelea sasa hivi Tanzania jamii yetu ya wasomi wa Kikristo ndiyo tunaongoza tuki refer Escrow, Bandari,Tanesco, Reli, TRA, Mradi wa Mabasi, TAKUKURU, kula pesa za miradi ya serikali.

Ndugu zanguni Wakirsto sisi ni wasomi usomi wetu umelisaidia taifa au usomi wetu tunautumia kulitafuna taifa kwa ufisadi.
 
ivi Tanzania kuna wasomi? Yaani kwenda shule na kudesa tayali unakuwa msomi? Watu wanazawadiwa titles, sijui graduate, sijui Dr, sijui Prof? Ulojo mtupu. Hao graduates, hao madocta, hao Maprof wa Tanzania wamevumbua nini? Wametengeneza nini cha maana kuweza kuisadia jamii yao?

🔱No any meaningful innovation or invention, or discovery, or manufacturing has reached by Tanzanians. Usomi unatoka wapi? Au pengine niulize technolojia yetu ni nini? Kutengeneza sindano ya mkono? Kutengeneza viberiti? Au kutengeneza meli?

Tanzania tuna wasomi bingwa wa kukariri, kudesa tu. Madaktari bingwa wa kukariri. Mainjinia bingwa wa kukariri. Wanasheria bingwa wa kukariri. Walimu bingwa wa kukariri... Wasomi wa design hii hujikuta wamesahau kila kitu walichosomea kadili muda unavyokwenda. Muulizeni Prof Kapuya kama bado anakumbuka nini. Muulizeni Dr Nchimbi, Muulizeni Prof Maghembe, Muulizeni kila msomi!

Wakati katika ulimwengu wa kwanza anayehesabika kuwa ni msomi ni yule anayevumbua technology mpya au kuboresha technology iliyokuwepo, mambo ni tofauti nchini Tanzania. Sisi Mwenye uwezo mkubwa wa kukariri ndiyo msomi. Damn!

Wasomi wetu ni wasomi mawazo tu. Watu wa talk talk talk, write write write anything, any rubbish from morning to evening! Nani anayekula maneno? Eti wasomi wetu ni akina Prof Bana, Prof Kitila, and their colleagues! Rubbish!
 
Katika serikali iliosheheni wasomi ni hii ya awamu ya tano. Rais jpm aliwaweka kwenye nafasi mbalimbali akiamini wasomi hawa watatumia usomi wao kulikwamua hili taifa kupiga hatua za kimaendeleo fasta fasta! Mambo yamekuwa kinyume chake!!!

Ni mara nyingi mh Rais amekuwa akisikika hewani kuwa WATENDAJI WAKE HUWA HAWAMWELEWI KUWA ANATAKA NINI, serikali iliyojaa PhD holders na maprofesa wameshindwa kujua nini wanatakiwa wafanye.

Binafsi nilishawahi kuwafuatlia(kipindi cha nyuma) hawa wasomi wetu juu ya msaada wao kwenye taifa hili na niliofanikiwa kuwauliza walinijibu kuwa shida haiko kwao (hao wasomi) kwani wao wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali na kuzipeleka serikalini kwa ajili ya implementation, ila kwenye implementation yake ndipo palipo na tatizo. Sasa kwenye awamu hii ya tano hao wasomi ndio wako huko kwenye hizo nafasi za ku-implement , lakini tatizo liko palepale!!!!!!!

Why this!
 
- Unataka hao wasomi wafanyeje wakati zee la vi-wonder linataka lifanye kila kitu, ukifanya tofauti.

- Aidha litakufokea hadharani mbele za watu au

- Litakutumbua
 
- Unataka hao wasomi wafanyeje wakati zee la vi-wonder linataka lifanye kila kitu, ukifanya tofauti.

- Aidha litakufokea hadharani mbele za watu au

- Litakutumbua
Kama hutaki kufokewa au unaogopa kutumbuliwa si uikatae post once unapoteuliwa?!!
 
kuna mtu mmoja ana mfano hai katika taasisi anayofanyia kazi. Anasema kipindi taasisi ilivyokuwa na wasomi wachache saaana,walifanya vizuri sana tena sana. kwanza walikuwa na mhasibu ambaye elimu yake ilikuw ndogo sana lakini walikuwa maslahi yao yote kuanzia overtime, pesa ya likizo ilikuwa inapatikana kwa wakati lkn sasa hivi,watu walioenda likizo mwaka juzi ndo wanalipwa pesa ya nauli mwezi huu. kwa hiyo wasomi janja janja nyingi sana kazi zero
 
Katika serikali iliosheheni wasomi ni hii ya awamu ya tano. Rais jpm aliwaweka kwenye nafasi mbalimbali akiamini wasomi hawa watatumia usomi wao kulikwamua hili taifa kupiga hatua za kimaendeleo fasta fasta! Mambo yamekuwa kinyume chake!!!

Ni mara nyingi mh Rais amekuwa akisikika hewani kuwa WATENDAJI WAKE HUWA HAWAMWELEWI KUWA ANATAKA NINI, serikali iliyojaa PhD holders na maprofesa wameshindwa kujua nini wanatakiwa wafanye.

Binafsi nilishawahi kuwafuatlia(kipindi cha nyuma) hawa wasomi wetu juu ya msaada wao kwenye taifa hili na niliofanikiwa kuwauliza walinijibu kuwa shida haiko kwao (hao wasomi) kwani wao wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali na kuzipeleka serikalini kwa ajili ya implementation, ila kwenye implementation yake ndipo palipo na tatizo. Sasa kwenye awamu hii ya tano hao wasomi ndio wako huko kwenye hizo nafasi za ku-implement , lakini tatizo liko palepale!!!!!!!

Why this!

Kulisaidia kivipi? Mbona wamelisaidia sana tu au wewe ulitakaje labda? Ulitaka TZ kuwa na matatizo 0?
 
tatizo usomi wetu umejikita kwenye vyeti zaidi,kufaulu mitihani,kupenda sifa, na kupata/kulinda kibarua so kifikra hatupo huru(uoga) wasomi wanapelekeshwa tu na wanasiasa thus y PhD holder wengi in tz wanakua liability kwa taifa
 
fafanua mkuu
Mfumo wetu wa Elimu kwa asilimia kubwa unawaandaa watu kuajiriwa na wala sio kujiajiri.

Jee, kuna wasomi wangapi wenye kiwango cha PhD( nimetolewa mf.) wamegundua au kufanya jambo lenye tija na ambalo tunaweza kujivunia kimataifa?
 
Waliolisaidia Taifa ni wale walioishia Darasa la saba na wale ambao hawakwenda shule.Hao wasomi ndio walioliangamiza ili Taifa.
 
Back
Top Bottom