Wasomi wetu na mustakabli wa taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi wetu na mustakabli wa taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TANMO, Mar 24, 2010.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Wanajamii kuna habari nimeisoma kuhusu msimamo wa vyuo vikuu dhidi ya waraka waziri Maghembe kuwataka watumie vyeo vya mwenyekiti badala ya rais wa serikali ya wanafunzi na pia juu ya kufutwa kwa serikali za wanafunzi n.k

  Kauli yao waliyoitoa juu ya waraka huo ni ya kumtaka waziri aachane na mambo hayo vinginevyo watapambana naye na hata ikibidi wataendesha kampeni dhidi yake kwenye jimbo lake la uchaguzi.

  Hoja yangu siyo kujadili upande upi uko sahihi bali kutokana na msimamo wa wasomi hawa nimeshawishika kuamini kuwa tatizo la uongozi mbovu nchi yetu mara nyingine linasababishwa na ubinafsi tulionao watanzania hasa wasomi. Ni mara nyingi sana viongozi wetu wanatoa kauli au kufanya maamuzi ambayo hayana tija kwa jamii lakini sijawahi kusikia kauli ya hawa viongozi wa vyuo. Mpaka maslahi yao yanapoguswa ndiyo wanaibuka na kutaka kuishirikisha jamii.

  Nadhani ni wakati sasa kwa wasomi wetu nao angalau kutoa misimamo yao pale wanapoona mambo yanafanyika ndivyo sivyo serikalini. Hii itasaidia angalau kuamsha mori ya wazalendo wengine kwa manufaa ya jamii ya watanzania wote.

  Nawasilisha.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ndugu, Wasomi sio kwamba hawoni madudu ya sirikali yao i think UTAKUWA UNAKUMBUKA KAMA ULIKUWEPO KIPINDI CHA NYERERE WAKATI WASOMI WALIPOKUWA WANAANDAMANA HADI IKULU KAMA HAWAPENDEZEWI JAMBO, NYERERE ALILIONA HILI NDO SIRIKALI WAKAWEKA MSIMAMO KWAMBA SIASA VYUO VIKUU HAKUNA, JIULIZE KWANINI WAGOMBEA WA UBUNGE NA URAIS HAWENDI VYUONI KUPIGA KAMPANI?? KWANINI ZITTO ALIZUIWA WAKATI ANAENDA UDSM KUUTUBIA???
   
 3. M

  Major JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2010
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Unaposema wasomi wetu, nashindwa kuelewa. hivi ina maana Tanzania nayo ina wasomi, Tanzania ina wakariri maandishi na wala haina wasomi kwa taarifa yako.ingekuwa na wasomi basi ingekuwa ina soko kubwa la kuuza mali ghafi zake na fito vyake vya thamani fikiri ni nchi ya tatu duniani kwa kuzalisha dhahabu lakini hatuna soko la kuuza dhahabu, ni mpaka South africa watusaidie kuuza. Sasa hivi hata mbao zetu ni mpaka kenya watusaidie kuuza.Shangaa tangu tulipoanza kuzalisha ges yetu ya songa mpaka leo ni mika kumi inaenda sasa lakini bado tunaagiza ges nje wakati ya kwetu ni nyingi ambayo hatutakaa tuimalize kwa hata miaka 1000. Sasa hapa kuna wasomi au kuna matope? pls usinitie hasira
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nijuacho mimi wasomi wetu wengi ni wazuri na wanaweza kuleta mabadiliko makubwa tu, lakini system iliyopo haitaki mtu yoyote aliye above average na iko tayari kukumbatia wataalama mediocre ilimradi hawahoji, hawafikirii na watadumisha status quo

  ukiona kuna wasomi wako serikalini, ujue kabisa hao ni wale wa "ndio mzee" na wamesha-trade usomi wao kupata vyeo vya kisiasa, yaani ni kama wamedenouce usomi wao

  THINK ABOUT IT!
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  definition ya usomi Tanzania
  inafurahisha sana........
  sisi tumekuwa kama kisiwa hivi,tuna mambo yetu
  ni made in Tanzania only...........
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Mar 24, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Wewe uko kundi gani? la wasio wasomi?
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kuna mwenye CV ya Prof Maghembe?................nasema hivi kwa sababu nilihudhuria conference moja ughaibuni.............wakati huo akiwa Waziri wa Utalii..............nilibaki nikijiuliza maswali meeengi sana....................
   
 8. serengo

  serengo JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2014
  Joined: Jul 30, 2013
  Messages: 426
  Likes Received: 267
  Trophy Points: 80
  Wana JF nimekuwa nikijiuliza kila kukicha Tanzania wanaongelewa wasomi kila kukicha , nafasi zote za uongozi zimekuwa za wasomi , hebu tujiulize huu utitili wa wasomi tulio nao umeisaidia nini Tanzania? mbona nchi inaelekea kubaya tofauti na kipindi ambacho hatukuwa na wasomi wengi, tunawasomi hata kutengeneza SINDANO hawawezi kila kitu tunaagiza kutoka nje ya nchi, kazi yao kujidai wasomi na degree za kununua au elimu za kwenye MAKARATASI ndo maana wanakuwa na uelewa mdogo?leo hii kila msomi anataka awe kiongozi serikalini wanalenga kuiba tu hakuna cha maana, tungewatambua usomi wao kama wangeleta mabadiliko mfano kwenye elimu, afya , uchumi , wasomi wetu wamebaki kupiga kelele za kuongezewa posho ndo maana tunazalisha division 5, ni mda umefika tuwahoji wasomi wetu hizo PHD zao wameifanyia nini tanzania, kuna watu wanaelimu ya kawaida sana form iv hadi vi lakini wanauelewa kuliko mtu mwenye PHD, hivyo tukiendekeza maswala ua usomi nchi yetu itapoea, tua Ndo tumpe uongoziangalie uelewa wa mtu na ameifanyia nini nchi yetu.
   
Loading...