Wasomi watanzania: Wakili Lissu mfano wa mchumia tumbo na aibu kwa Chama Cha Mawakili

Mugisher

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
411
360
Wasomi watanzania wamezidi kuonyesha jinsi gani si watu wenyemisimamo bali ni wachumia tumbo. Nikimuangalia Lissu (kama mfano) ambaye alikuwana misimamo imara dhidi ya dhuluma na ufisaditangu wakati ule akifanya kazi za uwakili kwa weledi mkubwa. Lissu kesi zakezote (kama si nyingi) alikuwa akiwatetea wanyonge.

Ingawa watu hawajui hili,pamoja na uzuri wake, Lissu alikuwa hashindi sana kesi, kwa maana nyingine,hakuwa na rekodi nzuri ya kushinda kesi. Alipokuwa mwanasiasa Lissu aliendeleana msimamo wake dhabiti dhidi ya ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma. Wazunguwanasema alikuwa CONSISTENT siku zote. Mara ghafla Lowasa amekuja, sijui ninini Lissu kimemtokea.

Kama mtu ninayemjua binasfi, kati ya watu niliotegemea wangepingahili au kwa manufaa ya chama angekaa kimya au kujiondoa kwa heshima, Lissualikuwa mmoja wapo. Lakini kwa bahati mbaya, yeye hakufanya hivo.

Naheshimumaamuzi yake, lakini swali langu ni maamuzi haya ya kigeugeu, yakubadilikabalidilika yanaleta sura gani kwa wasomi wetu? Namchukulia Lissu kama mfano wawasomi wetu ambao hawana misimamo, hasa kwenye mambo ya msingi.

Kamamwanasiasas msomo hujiwakilishi wewe tu, unawakilisha familia yako, tabakalako, jimbo lako, kabila lako, profession yako n.k. Sasa huyu wakili msomi amejalitumbo lake na AHADI ZA KUWA WAZIRI WA SHERIA. Ndiyooo.. Lissu anategemea iwapoLowassa atashinda (MWENYEZI MUNGU TUEPUSHE NA HILI) basi yeye atakuwa waziri washeria. Je mtu unaweza kuwa mbinafsi kiasi kichi?

Lissu kwa ujumbe huu, nataka nikuambie umeibaka professionyako na ni aibu kwa TLS. Wewe ni mtu mbabaishaji, hueleweki, kigeugeu na zaidi yayote huaaminiki tena. Silaha kubwa ya wakili yoyote ukiacha elimu yake, nilazima awe mtu anayeaminika. Sasa kwa haya aliyofanya Lissu anaaminika tena?
 
Kamtaja mhusika mkuu wa Richmond sasa kwa nini unamtukana?Tanzania MAFISADI ndiyo wanaoishi kwa amani hasa ukiwa CCM.Jamani mwaka huu CCM ikae pembeni tu UKAWA wasafishe uchafu ambao Kikwete anasema Magufuli akishinda atalala usingizi.Mzee anaamini demokrasia ila haamini Chama kingine this is a shame
 
Kazi Ya Wakili Ni Nini? Ata Common Sense Hauna,story Ndefu Akili Huna. Wakili Anatetea Alipo Kama Mhusika,je Aache Kumtetea Lowasa?
 
JK kamuomba ataje na yeye kataja sasa kosa lake ni nini!?
Mwanzoni alimhusisha EL lakini baada ya yeye mwenyewe kuonana na kamati kuu ya cdm (na Dr. Slaa akiwepo) na kuwaeleza uhusika wake kwenye Richmond na kutoka live kwenye media akisema uhusika wake ilikuwa ni maelekezo kutoka juu, ulitaka wafanyeje!?
Wewe nakufananisha na Litanzania lingine limoja ambalo nimeona linalalamika na kuilani TANSCO eti kwa nini miaka yote huduma zao ni mbovu lakini likisisitiza kuwa #hapakazitu!
 
Kazi Ya Wakili Ni Nini? Ata Common Sense Hauna,story Ndefu Akili Huna. Wakili Anatetea Alipo Kama Mhusika,je Aache Kumtetea Lowasa?
Hujui unachoongea ROBERT MTINDA. Nani kakwambia Lissu ni wakili wa Lowassa? Tangia lini na mahakama gani? Acha kutumia uharo kufikiria.
 
JK kamuomba ataje na yeye kataja sasa kosa lake ni nini!?
Mwanzoni alimhusisha EL lakini baada ya yeye mwenyewe kuonana na kamati kuu ya cdm (na Dr. Slaa akiwepo) na kuwaeleza uhusika wake kwenye Richmond na kutoka live kwenye media akisema uhusika wake ilikuwa ni maelekezo kutoka juu, ulitaka wafanyeje!?
Wewe nakufananisha na Litanzania lingine limoja ambalo nimeona linalalamika na kuilani TANSCO eti kwa nini miaka yote huduma zao ni mbovu lakini likisisitiza kuwa #hapakazitu!
Soma tena nilichoandika. Mimi siongei mambo ya Richmond- ndio tatizo lenu mnasoma lakini hamchambui. Mimi nimeongelea misimamo yake na kile anachoamini. Penda kwa kiasi.
 
JK kamuomba ataje na yeye kataja sasa kosa lake ni nini!?
Mwanzoni alimhusisha EL lakini baada ya yeye mwenyewe kuonana na kamati kuu ya cdm (na Dr. Slaa akiwepo) na kuwaeleza uhusika wake kwenye Richmond na kutoka live kwenye media akisema uhusika wake ilikuwa ni maelekezo kutoka juu, ulitaka wafanyeje!?
Wewe nakufananisha na Litanzania lingine limoja ambalo nimeona linalalamika na kuilani TANSCO eti kwa nini miaka yote huduma zao ni mbovu lakini likisisitiza kuwa #hapakazitu!

Wewe ki.l.aza umelishwa sumu mbaya sana.
 
Msimamo wake kamtaja muhusika kwan ni tatizo kasema ukwel na ushahidi upo lissu hoyeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Bila shaka uzi huu umeanzishwa na mtu aliyeweka kambi CHOONI

Ukitaka usiumize kichwa sana, usilifikirie hili jambo kisiasa.

Fikiri kwa ufupi tu kwamba LISSU NI WAKILI.
Itakusaidia usipoteze muda kuwaza sana.

Ila kwa upande mwingine wa KISIASA ni kwamba, alichosema Lissu kilikuwa ni jibu kwa JK.

Mbona rahisi sana kuchanganua hapo mkuu!
 
Kila mtu ni mchambuzi wa mambo magumu, hata yale tusiyokuwa na utaalamu nayo! Mugisher eembu njoo hapa nisaidie maana ya wasomi kama ulivyowatumia kwenye 'insha yako'
 
Last edited by a moderator:
Hivi nyie ndiyo wanapropaganda wa CCM? Mbona hamfanyi kazi yenu ipasavyo?

Tafadhari kuweni serious, or else......
 
Hujui unachoongea ROBERT MTINDA. Nani kakwambia Lissu ni wakili wa Lowassa? Tangia lini na mahakama gani? Acha kutumia uharo kufikiria.

Umeuliza ...mahakama gani?...

Sio lazima uwe mahakamani ili kuweza kuwa na wakili wako.

Taasisi zinakuwa na mawakili, watu binafsi wanakuwa na mawakili.

Ivi kwanza unajua kwamba ni haki yako kuwa na wakili?
 
Mugisher

Ulishawahi kuona kesi isiyoruhusiwa wakili kuisimamia? wakili anatetea uadilifu wa mtu au anashughuliakia mambo ya kisheria katika kesi inayomhusu mteja ili aweze kutoa shauri?

Wewe mleta mada weka ushahidi wako hapa kumhusu Lowasa ili tuanze kuuchambua kama kulungana na ushahidi ana kosa au laa.

Halafu pia usimwangalie Lowasa tu na kuacha kuangalia mamia kama sii maelfu ya mafisadi yaliyobaki ndani ya ccm na bado eti yanafikiri kuondoka kwa Lowasa ndiko kuliko yatakasa.
.
 
Last edited by a moderator:
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom