Wasomi wataka uwazi wa matumizi vyama vya siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi wataka uwazi wa matumizi vyama vya siasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 17, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,203
  Trophy Points: 280
  Wasomi wataka uwazi wa matumizi vyama vya siasa

  Mwandishi Wetu
  Daily News; Thursday,October 16, 2008 @21:00

  Wadai kuna matumizi mabaya, CAG ayakague

  WASOMI na wanasheria wamesema kuna matumizi mabaya ya fedha ndani ya vyama vya siasa na wamependekeza matumizi yote ya vyama vyote yawekwe wazi, ikiwa ni pamoja na kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Wakichangia katika kongamano la siku mbili kuhusu rushwa katika siasa na suala la kugharimia shughuli za siasa lililoanza Dar es Salaam jana, wametaka matajiri wa ndani ya nchi na wa nje ya nchi ambao wanavifadhili vyama mbalimbali waanikwe hadharani kabla ya uchaguzi ili kujua kiasi cha fedha kinachotumiwa na vyama vya siasa.

  Wa kwanza kuchokoa mjadala huo alikuwa Jaji Joseph Warioba ambaye katika mada yake alisema licha ya wabunge kuwa wakali kuhoji fedha za serikali, lakini viongozi hao hawajui na wala hawazungumzii kwa ukali kuhusu mapato na matumizi ndani ya vyama vyao.

  “Wanazungumzia mambo ya fedha ndani ya vyama vyao pale tu wanapogombana wao kwa wao,” alisema Jaji Warioba na kuongeza kuwa uwazi katika mambo ya mapato na matumizi ya fedha za umma za aina yoyote ni jambo la msingi katika nchi ya demokrasia.

  Jaji Warioba alisema matumizi mabaya ya fedha ndani ya vyama yamefikia hali ambayo rushwa ndani ya siasa ni kama inakubalika, kwani viongozi wanatumia rushwa na wananchi wanategemea hivyo na wanangojea takrima. Jaji Mkuu Augustino Ramadhan katika mada yake alisema matumizi mabaya ya fedha ndani ya vyama ni aina moja ya rushwa.


  Alifafanua kuwa lugha za mambo ya chama yanazungumzwa kwenye halmashauri kuu sio kwenye Bunge yanatoa fursa ya vyama kutumia vibaya fedha za ruzuku.

  “Huu ni mwanzo wa matumizi mabaya ya fedha katika chama na yanasababisha uwepo rushwa ndani ya chama,” alisema Jaji Ramadhan katika mada yake iliyosomwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa Ferdinand Wambali.

  Jaji huyo alipendekeza ili kuwepo na nidhamu katika matumizi ya fedha za ruzuku ni lazima zikaguliwe na CAG, kwa maelezo kuwa ndio njia pekee ya kudhibiti rushwa ndani ya vyama vya siasa.


  Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Jaji Amir Manento, alisema kwa kuwa imedhihirika kuna wabunge wanaingia madarakani kwa kutoa rushwa, ni vyema Katiba ya Nchi ibadilishwe kumpa fursa Rais kuteua mawaziri kutoka miongoni mwa wananchi ambao sio wabunge.

  “Hawa rais atakaowateua ambao sio wabunge watakuwa hawajaathirika na rushwa hizi ndani ya uchaguzi, hivyo watakuwa waadilifu na wataweza kukemea rushwa,” alisema Jaji Manento.

  Jaji pia alipendekeza matajiri ambao wanavifadhili vya siasa watangazwe na vyama vyenyewe kabla ya uchaguzi na kiasi cha fedha wanachotoa. Alisema kitendo cha wafadhili hao kutoa fedha kisiri vinachangia matumizi makubwa ya fedha ambayo hayana udhibiti.

  “Hawa watangazwe mapema tuwajue na kiasi cha fedha wanazotoa…kwa nini wanaogopa kutangazwa kama wafadhili kwa nia njema? Alihoji.


  Lakini Jaji Warioba anaonya kuwa kwa chama kutegemea misaada ya wahisani ni hatari kwani kila mfadhili anakuwa na malengo yake hivyo akapendekeza vyama viweze kupewa ruzuku kutoka kwenye fedha ya nchi.

  Jaji Warioba pia alishauri sheria ya ufadhili katika vyama vya siasa iwe wazi ili wafadhili wa nje na ndani wanaotoa fedha wawe wanajulikana, lakini pia wawe na kiwango maalumu na sio ilivyo kwa sasa ambayo ni siri ya chama.

  Kongamano hilo la rushwa katika siasa lilifunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, ambaye alisema lengo lake ni kutathmini utaratibu na sheria za uchaguzi ambao unafaa katika kuendeleza demokrasia ya vyama vingi.

  Kongamano hilo linawashirikisha wabunge, viongozi wa vyama vya siasa, majaji, wanasheria na limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya msajili wa vyama vya siasa na taasisi za kudhibiti na kuzuia rushwa.
   
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kongamano, warsha, semina, kozi, ziara, matembezi, seminar, fursa, mijadala, mikakati, mikutano, vijiwe, malengo, sera, kampeni, ilani, workshop, training, mafunzo na kadhalika, ni nani anayepima positive or negative effects zake ili tuendelee kuzipangia pesa au la?

  Tired; unaalikwa, mnazungumza, mnalipwa posho. Ni dhambi kama mkiulizwa yale mliotoa mwaka jana mnataka kuona matunda yake badala ya kila siku kuitwa tu nakurudia rudia?
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi Muungwana si aliahidi wakati anaingia madarakani kulishughulikia hili? nalo anahitaji muda gani kulikamilisha?
   
Loading...