Wasomi waonya chuo kikuu cha Dar-es-Salaam kutumiwa kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi waonya chuo kikuu cha Dar-es-Salaam kutumiwa kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmwaisoba, Oct 26, 2012.

 1. m

  mmwaisoba JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 434
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika hitimisho la miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo kikuu wasomi mbalimbali amesifu mchango wa chuo hicho katika masuala mbalimbali yanchi lakini wameonesha kutilia shaka baadhi ya wasomi wenzao ambao wamekuwa wakitaka kukichafua chuo hicho kwa kukiweka katika ushabiki wa siasa badala ya kuwa kioo cha kuongoza maendeleo ki falsafa.

  Wameshangazwa na mtindo wa baadhi ya viongozi waandamizi wa jumuiya ya wanataaluma UDASA kutumia nyadhifa zao katika vyama vya siasa kuleta makongamano yenye ajenda ya kupigia debe vyama vyao.

  Baadhi ya wanataaluma hao wamebainishwa kuwa ni wastaafu na hawapo tena chuo kikuu lakini wamekuwa wakitumia historia ya kuwahi kuwa chuoni hapo kuleta makongamano yenye mtazamo wa upande mmoja. Pia walitilia shaka matumizi ya baadhi ya vyombo vya habari.

  Chuo kikuu kina Television yake Mlimani TV, LAKINI BAADHI YA WANATAALUMA WAMEKUWA WAKIITA VYOMBO VYA HABARI AMBAVYO NI VYA BINAFSI NA KURUSHA LIVE MAKONGAMANO HAYO BILA KUWEKA BAYANA NANI WANAFADHILI MATANGAZO HAYO.

  WALIWEKA MSIMAMO BAADA YA KUHOJI IWEJE KWENYE MAADHIMISHO YA CHUO KIKUU MBONA HIVYO VYOMBO VYA HABARI HAIVIKURUSHWA SHEREHE ZA MIAKA HAMSINI YA CHUO KIKUU? LABDA KUTAKUWA NA MAJIBU KWENYE HII FORUM
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hao wasomi wanaolalama kuhusu hili ni wanafiki. Wangegomea kwanza kwa Prof. Mkandara (Kada wa CCM) kutumia wadhifa wake kutekeleza majukumu ya chama na kudhoofisha upinzani. Tunajua hawa wanalalamika wapinzani, na wameshaamua kumuondoa Dr.Kitila Mkumbo kwenye uongozi wa UDASA kipindi kijacho. Hizi ni zuga zuga tu, target yao ni Dr. Kitila. Kama wangeanza kwa kulalamika UD kutumiwa na CCM tungewaelewa.

  Inashangaza kuona wasomi hawa (kupitia umoja wao wa wanataaluma) waliopinga Mh. Rais Dr. Jakaya Kikwete kupewa Honorarium Doctor-ship na Chuo kikuu cha Dar-Es-salaam, lakini uongozi wa chuo kupitia kada aliyepewa chuo na JK mwenyewe (Prof.Mukandara) walifanikisha hilo.

  Tunapenda kuwaeleza tu, image ya UD imeharibika sana kimtazamo katika jamii ya wasomi wanaotegemea kuwa wasomi watoe dira makini bila kuegemea upande mmoja. Tunajua wasomi wanatishiwa kutekeleza majukumu yao sahihi kwa kutopewa mikataba baada ya umri wa kustaafu kufika, kwa sababu tu za kisiasa hata kama wanahitajika. Tena na wale waliopo kwenye mkataba ndiyo wamekuwa waoga sana na kutokuwapa tena mwanga wanajamii, kisa ni kuogopa mikataba yao kusitishwa. Mfano mzuri ni Prof. Baregu Mwesiga, sababu tu yupo kwenye Upinzani basi waliamua kusitisha mkataba wake.

  Nchi hii unathaminika pale tu unapokuwa mtwana wao, na pindi ukitaka kutenda haki na ikaonekana ni kinyume cha watawala hawa wa sasa basi wewe ni adui namba moja. Tunaimani hali hii itakwisha, na hasa pale wasomi wetu watakapoacha kuwa waoga na kutekeleza majukumu yao kikamilifu, basi Tanzania yenye dira sahihi itapatikana upesi.
   
 3. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  aiseee babaangu kweli wajinga waliwao mlimani tv inashika kinindini ilala na temeke unataka watu wa mikuani wasipate tarifaa????
   
 4. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,298
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Naomba hawa wanaoitwa wasomi wanaolaumu kutumia ITV na kuhoji mfadhili ni nani watajwe kwa majina halafu nitarui baadaye kukata data kuanzia enzi za marehemu Prof. Chachage. Wamtoe Dr. Mkumbo UDASA ili wampe Dr. BANA?
   
 5. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu huyo bana ndio mnafki tena ni gamba kubwa pale udsm,,ni bora wampe prof chaliga, prof kimambo au prof mutahaba
   
 6. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  muwasilishaji naomba ufafanuzi manake umenitatiza!
  hv kongamano mlilozungumzia ni siku ile ya kumbukumbu ya kifo cha nyerere?
  hv maada iliyokuwa ikitolewa pale ilihusiana na kukitangaza chama chochote cha siasa?
  kina nape, mtatiro ni viongozi wa siasa mbona wasizungumzie ya vyama vyao badala yake hata nape alipopewa nafasi alisapoti lile lililokuwa likizungumziwa?
  mara ngapi tumeshuhudia makada wa ccm wakienda chuo kikuu cha Dodoma ?
  vipi hv akina Dr. Bana na Prof Rwekaza Mukandala wao mara ngapi tunawasikia wakiongea mambo ya CCM pale?
  Vyombo vya habari vina haki na wajibu wa kutoa taarifa kwa watu.. na watu wana haki na wajibu wa kupata habari..
  hv walitakiwa wakaripoti kwa mkandala juu ya utendaji wao na mahali watakapopata wadhamini?
  hv mlimani Tv walizuiliwa kurusha kipindi kile hewani? Hata kama kile kipindi kingedhaminiwa na chama chochote cha siasa kuna sheria yoyote inayokataza?
   
 7. C

  Concrete JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mleta mada embu funguka zaidi tuelewe hiyo hoja, kwa mfano
  1/Ni akina nani hao wasomi?
  2/Wapi wamesema hayo maneno?
  3/Lini wamesema?
   
 8. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,298
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Wanaompinga Dr. Mkumbo ni vijana wa Prof. Mkundala na wanaCCM wa waziwazi ndoo maana nimemtaja huyo Dr. Bana. Prof. Kimambo Isalia? Huyu ni mzee sana atadhidisha busara, Chaligha yupo tume ya uchaguzi kwahiyo anaeleweka kuwa tayari kazibwa mdomo. Prof. Mutahaba nimemskia siku moja tu sijamfahamu msimamo wake ila sidhani kama anaweza mnyoshea kidole Prof. Mkandala si homeboy wake
   
 9. m

  mdunya JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wanafiki! Hawana tofauti na Dr. Ramadhan Dau wa NSSF
   
 10. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Elimu imekufa mlimani na haijauwawa na siasa. Vyuo vyote duniani ndio mambo muhimu hufanyika pamoja na siasa, anaglieni USA kila wakifanya debate, mikutano ya kampeni, wageni wa kisiasa wakija wakitaka kuhojiwa mfano Raisi wa Iran wote huenda vyoni kukutana na watu wenye akili zinazochemka. Sasa chuo chetu cha dar kinakufa sio kwa sababu ya siasa la hasha, ubora wa elimu unaporomoka kwa sababu ya waalimu kukosa lishe bora. Naomba neno lishe bora mtumie elimu kulipambanua.
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Uwezi tenganisha usomi na siasa hasa kwa nchi yetu inayopitia kwenye kipindi cha mabadiliko. Tatizo lao wametumwa na magamba kuleta umbea, hapo wanamsema Dr Mkumbo, baada ya lile kongamano la wiki mbili zilizopita lililorushwa live na ITV.
   
 12. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mtu anaelengwa ni Dr Mkumbo,mbona Bansen Bana na Mkandala wapo pale kwa fadhila za kisiasa kwa kazi 'nzuri' ya marehem REDET? KWANZA Bana cku izi akihojiwa na media atoe maoni ya kisiasa bora hata maoni ya mtoto wa kaka yangu aliyepo darasa la 4.
   
 13. i

  ibange JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Labda yanaweza kuwa maoni ya msomi Uchwara Dr (Sic) Bana, ila hakuna msomi wa kawaida atasema maneno ya kipuuzi hivyo
   
 14. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Huku ndiko kufikiri kwa vijana wa kizazi cha dot com. Nadhani kama upo chuo kila kitu una ki google unacopy na ku paste kwenye assignment zako. ndio maana huwezi ku reason!
   
 15. Monyiaichi

  Monyiaichi JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 1,825
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Hivi dr bana anaonaje jinsi hadhi yake inavyoshuka kwa ushabiki wake kwa chama tawala? Interlectuals wanategemewa zaidi katika michango ya mageuzi ya kiuchumi, kisiasa na kielimu. Kushabikia ulaji kidogo inaleta utata kwenye uwezo wa mhusika. Kwa sababu kwa sasa hivi sio kwamba ni siri, nchi yetu iko vibaya kiuchumi, kisiasa na kielimu, tukiachana na propaganda za siasa kwamba uchumi umepanda. Tunajuaga hizo report zinakuwa za ku-cook zaidi. Ina maana na usomi wote mtu anajidhihirisha kuhofia tumbo?
   
 16. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wana REDET akina profesa Mukandala kapewa VC wa udsm,,na Profesa Berdetta kiliani ni mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na mawasiliano.Ni kweli kabisa siasa inatafuna udsm.
   
 17. L

  Lamusumo JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na dr bana anapewa ukuu wa idara.
   
 18. 2hery

  2hery JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,551
  Likes Received: 2,063
  Trophy Points: 280
  Noana sasa wanaojiita wasomi wameanza kufikiri kwa kutumia ile nyenzo muhimu ya masaburi.mbona hawajifunzi mambo mazuri kutoka kwa wenzetu midahalo inayohusu mustakabali wa nchi wanataka ifanyiwe nyumbani kwa Prof mkandala.??
   
 19. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  aiseeee babaangu ulicho sema ni kweli kabisa prof mtahaba wanakaa mtaa mmoja na mkandala aka mzee wa ps 220 na mkandala ndio mwasisisi wa hali mpya kasi mpya na nguvu zaidi,, basi 2mpe dr ngware wa ds au au prof mbonile wa ge ikishindikana rwaitama
   
 20. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Wasomi? Wasomi gani hao wanaoweza kuwa na busara kidogo kiasi hicho. Heshima gani ya chuo itakayosahau mambo ya nyakati. Hizi ni enzi za vyama vingi. Hizi ni enzi ya vyama kongwe kufa. na hizi ni enzi za kila mtu kuwa na akili yake.

  Nadhani kuna watu wanashindana na Mkandara kujikomba. Kila wakati wanataka waonekane wanaipenda CCM. Uchafu mtupu!
   
Loading...