Wasomi wamshukia Jaji Mark Bomani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi wamshukia Jaji Mark Bomani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 17, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,409
  Likes Received: 414,712
  Trophy Points: 280
  Wasomi wamshukia Jaji Mark Bomani


  *Ni kwa kutetea malipo kwa kampuni ya Dowans
  *Wasema, kama hakurubuniwa, anazeeka vibaya


  Na John Daniel
  SIKU moja baada ya aliyewahi kuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mark Bomani, kudai kuwa malipo ya sh. bilioni 94 kwa
  Kampuni ya Dowans haikwepeki, wanazuoni nchini wamemshangaa Mzee huyo na kudai kuwa kama hakurubuniwa na wahusika wa kampuni hiyo basi anazeeka vibaya.

  Wakizungumza na Majira jana wanazuoni hao walisema hawakutarajia kauli kama hiyo kutolewa na Jaji Bomani kwa kuwa ni moja kati ya watu wenye heshima ambao wangeweza kuisaidia serikali badala ya kutoa kauli zenye utata.

  "Mimi nilifikiri kwamba Jaji Bomani angetoa ushauri kwa serikali kuwaeleza Watanzania nini kilichomo ndani ya kesi hiyo ya Dowans, hadi sasa wananchi hawajui ukweli kama Mkataba wa Richomnd ulikuwa halali au la, na kama haukuwa halali ndiyo hiyo ya Dowans au ni vitu viwili tofauti.

  "Lakini pia kuna kampuni iliyowakilisha TANESCO kwenye kesi hiyo, wananchi wanataka kujua kama kampuni hiyo ina uhusiano wowote na Richmond iliyofutwa au sivyo," alisema Profesa Mwesiga Baregu.

  Prof. Baregu ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha jijini Mwanza alilinganisha kauli ya Jaji Bomani na ile ya Mwanasheria Mkuu wa sasa, Jaji Frederick Werema ambayo pia ilipingwa vikali na Watanzania.

  Alisema suala la malipo ya Dowans linagusa maslahi ya umma, hivyo ni lazima serikali ichukue taadhari kubwa kabla ya kuitekeleza ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa kina kwa wananchi na si kuharakisha malipo kama inavyoshauriwa na Jaji Bomani.

  "Jaji Bomani angeshauri kwanza serikali kuwa wazi kwa wananchi kueleza nini kiini cha tatizo hilo, ni uzembe wa watendaji au udhaifu wa wanasheria kama inavyodaiwa, ieleze hatua zilizochukuliwa dhidi ya walioingiza taifa katika mkataba huo kabla ya kukubali malipo," alisisitiza Profsa Baregu.

  Alionya kuwa iwapo serikali itaendelea na mfumo wa kufunika mambo muhimu yanayohitaji maelezo ya kina ili kuondoa mawazo potofu, wananchi watafikia hatua mbaya ya kukosa imani na serikali na kujenga chuki kwa viongozi.

  Kwa upande wao wanafunzi wa mwaka wa tatu wa kitivo cha Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliozungumza na Majira kwa sharti la kutotajwa kwa ma hofu ya kushughulikiwa walisema wanadhani Jaji Bomani anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwa kauli yake ya jana.

  "Sisi wanafunzi wa sheria Chuo Kikuu cha Dar es saalam hatukutegemea mwanasheria wa miaka mingi kama Jaji Bomani aongelee suala la Dowans ambalo liko kwenye mchakato wa mahakama, lengo lake nini kama si kuifluence mahakama?" aliohiji mwanafunzi mmoja katika ujunbe wao walioituma Majira.

  "Ni aibu kuwa hata wazee kama Bomani wanarubuni na mafisadi kwa pesa na kuwasaliti wananchi masikini, amezeeka vibaya," iliongeza sehemu ya ujumbe huo.

  Walisema walitegemea Jaji Bomani kuisaidia serikali kutafuta njia ya kurejea upya uamuzi huo katika kipengele cha uhalali wa mkataba kati ya Richmond na serikali ambayo ndio iliyorithiwa na Dowans.Walisema iwapo mkataba wa Richmond haukuwa halali ni vipi ikirithiwa na Dowans inakuwa halali, na kuitaka serikali kutoa ufafanuzi wa kina juu ya suala hilo kwanza.Katika mazungumzo yake na gazeti hili jana, Jaji Bomani alitoa kauli ambayo haikutarajiwa na umma ya Watanzania kuitaka serikali kulipa Dowans kwa maelezo kuwa kutofanya hivyo kunaweza kuigarimu zaidi Taifa.

  Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam wiki hii, Jaji Bomani alisema ni vigumu Mahakama Kuu kutengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC Court) kama hakukuwa na kasoro zozote katika utoaji hukumu hiyo.

  "Kwa kesi za usuluhishi kama hii hukumu hii inaweza kutenguliwa tu kama hao wapatanishi hawakuwa na sifa za kuwa wapatanishi kitu ambacho hapa hakiwezi kutumiwa kwa kuwa katika suala hili, hawa walikubaliwa na pande zote," alisema Jaji Bomani na kuongeza;

  "Hukumu hii inaweza kutenguliwa tu kama ikidhihirika kwamba wamepewa rushwa kwa kutoa hukumu ya namna hiyo. Vinginevyo Mahakama Kuu haijihusishi na kuingilia kesi yenyewe.""Mimi kwa upande wangu kama nilivyokwisha kusema siku za nyuma jambo hili liishe ili mitambo hiyo itumike hapa nchini kuzalisha umeme tuondokane na hali ya mgawo na upungufu wa umeme na hilo ndilo jambo muhimu kwa uchumi wa nchi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,409
  Likes Received: 414,712
  Trophy Points: 280
  Huyu Babu pamoja ni mchovu lakini amekithiri ubinafsi.................baada ya yeye kushiba hataki nasi tushibe kila mahali anatupinga tu................Katiba mpya anasema tusiwe na pupa................sijui ni nani kamwambia tutakuwa na pupa.............................sasa hili la DOWANS ambalo linasigina sheria ya manunuzi hatuko naye...................................................where is he in this struggle?
   
 3. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Mzee wameshamnunua kina Rostam sio bure,tayari sio mwenzetu tena huyu
   
 4. T

  Tofty JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  It's amazing how someone's soul can be easily bought..........shame on u Judge!!!!
   
Loading...