kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
WASOMI wamesema kuwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete alistahili kupongezwa kwa kuanzisha mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Wasomi hao wametoa maoni hayo baada ya mwanaharakati, Jenerali Ulimwengu kusema juzi kuwa Kikwete anapaswa kushtakiwa kama viongozi wengine walioisababishia hasara Serikali. Wasomi wametafsiri maoni hayo ya Ulimwengu kuwa hayakuwa ya kichambuzi, bali ya kiunaharakati.
Akizungumza katika Tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam juzi, Ulimwengu alisema Kikwete anastahili kushtakiwa kwa kuwa fedha nyingi zimepotea wakati wa kuunda Katiba Mpya, ambayo haikupatikana.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana akizungumza na gazeti hili jana, alisema anamheshimu Ulimwengu kama mchambuzi wa kimtazamo, lakini katika suala hilo hakuwa sahihi.
“Ulimwengu ni kati ya watu kumi kwa mitazamo ya kimsimamo na wachambuzi wazuri lakini katika hili nadhani maoni yake yalikuwa ya kiuanaharakati zaidi na sio ya kichambuzi makini kama tulivyomzoea,” alisema Dk Bana.
Alisema mchakato wa Katiba, ulienda kwa mujibu wa sheria na Bunge ndiyo lenye dhamana ya kutunga sheria na siyo Rais huyo mstaafu, ambaye yeye alianzisha tu na kwamba Kikwete alifanya kila njia, kuhakikisha anawaridhisha watanzania kupata katiba.
Hata hivyo, alisema Watanzania wanatakiwa kumpongeza Kikwete kwa kuanzisha mchakato wa Katiba kuliko kuwa na mawazo kwamba anastahili kupelekwa mahakamani.
“Bunge lile la Katiba lilijadili na kufikia lilipofikia na katiba iko uwanjani, tunachosubiri ni kupiga kura ya maoni, Kikwete kosa lake nini? Mchakato ule ulikuwa wa Watanzania wote na siyo wa Kikwete,” alisema Dk Bana.
Aidha alisema Kikwete kama Rais wa wakati huo, alipoitisha Bunge la Katiba lilionekana ni jambo jema kwa Watanzania wote kwani ilikuwa ni kilio cha muda mrefu kupata Katiba Mpya, “sio vizuri kutanguliza maoni ya kiuana harakati katika midahalo ya aina hii,” alisema.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba la Kanisa Katoliki, Methodius Kilaini alisema mchakato wa kupata Katiba Mpya, hauhitaji haraka ni mchakato wa muda mrefu ambao unahitaji uvumilivu ; na hilo limejidhihirisha katika nchi mbalimbali zilizopitia jambo hilo.
“Katiba sio jambo ambalo unaanza tu na unapanga kumaliza ndani ya muda fulani, ina mchakato mrefu, jambo la msingi ni kuwa wavumilivu inaweza kuchukua hata hatua tisa kumi,” alisema Askofu Kilaini.
Alisema suala la katiba lilikuwa ni la nchi nzima na Serikali kwa ujumla, halikuwa la mtu mmoja ambaye ni Rais wa wakati huo Kikwete.
Alisema kwa maoni yake ni kitu cha kawaida utayarishaji wa Katiba mpya, kuchukua zaidi ya mihula kadhaa na wakati mwingine isifanikiwe.
“Tuangalie historia katika nchi nyingine wamefanyaje, tena tupongeze sisi hatuna mauaji wengine wameingia mpaka kwenye migogoro na mauaji lakini sisi tunaenda polepole,” alisema Askofu Kilaini.
Msomi mwingine ambaye hakutaka jina lake kuandikwa ambaye pia alishiriki katika Bunge la Katiba, alisema mchakato wa kupatikana Katiba mpya haukuwa wa Kikwete ni wa nchi nzima ambao ulihusisha wadau wengi.
Alisema Kikwete alifanya kazi yake ipasavyo, hivyo haoni sababu ya kusema kwamba Rais wa wakati huo anastahili kushtakiwa badala yake angepongezwa.
“Kwanza tungempongeza kwa kutumia rasilimali za ndani pekee kwa sababu hakuna mchakato kama huu ambao ungeendeshwa bila rasilimali, na tulizotumia hazikuwa za kutoka nje,” alisema.
Aidha alisema katika watu ambao walishiriki kuchelewesha mchakato wa Katiba mpya ni pamoja na wajumbe kutoka vyama vya siasa, ambao walijali zaidi maslahi ya vyama vyao.
Habari Leo