Wasomi walioeneza propaganda za mabeberu. Je, Ubeberu umekwisha?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kuna wasomi walitumia miaka mitano kuwatukana na kuwadhalilisha watu wenye upeo mpana na waliotuzidi maendeleo kwa kuwaita mabeberu. Wasomi hawa walifika wakati wanatuaminisha hata mtanzania mzalendo anayewaza sahihi kuhusu nchi hii anatumiwa na mabeberu.

Kauli mbiu ya mabeberu iliwajaa watu wazima na waliokombolewa kwa elimu nzuri huku wakujua fika kwamba wanachokifanya siyo kile wanachokiamini.

Nikifuatilia kuanzia tarehe 17/03/2021 neno mabeberu alitumiki Tena, hotuba bungeni na michango ya kamati na wabunge mbalimbali haina kitu kinaitwa mabeberu. Tujiulize waliotuaminisha tupo kwenye Vita na mabeberu wameishia wapi? Kwanini walituadaa na kunyamazisha watu kupitia dhana ya ubeberu?

Huko wapi uzalendo wao? Je baada yakulivuruga Taifa wanapewa adhabu gani? Je, wanaofanya mikutano na Mawaziri na hata Mhe. Rais tuendelee kuwaita mabeberu?
 
Niliwahi kusema hili mara nyingi humu. JPM alikuwa kama cult leader. Bila kujali kama ni kweli au la, aliaminisha watu kuwa “tunajenga kwa fedha zetu za ndani”, “tuko kwenye vita vya kiuchumi”, “nchi yetu ni tajiri” na “mabeberu”. Hizo zote zikikuwa ni dhana tu kwa sababu deni la taifa lilikuwa mara dufu, adui wa uchumi hakutajwa, utajiri haupimwi kabla rasilimali hazijawa converted na hata mabeberu hawakutajwa (huenda ni IMF, WB na nchi za kibepari).

Maneno hayo hayatumiwi tena toka mwezi March. Ndio kusema vita tumeshinda, mabeberu hawako tena, tumerudi kwenye umasikini??

Propaganda ni kitu kibaya sana!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom