Wasomi waitabiria mabaya CCM

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Na Kizitto Noya
Mwananchi

BAADHI ya wahadhiri wa Sayansi ya Siasa na Jamii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wametabiri kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaelekea kufa, kwa kuwa dalili zimeanza kuonyesha kuwa chama hicho kimepoteza dira na mwelekeo.

Wakizungumza na Mwananchi jana kwa nyakati tofauti, wahadhiri hao walisema CCM inatakiwa kujitazama upya na kuondoa kiburi na usiri unaotawala ndani ya chama hicho kwa kuwa ndivyo vitakavyokimaliza.

Wamesema kwamba usiri katika chama hicho unasabishwa na watendaji wake kutopenda kuweka wazi utendaji wao wa kazi unaoathiri uwajibikaji wao kwa umma.

Profesa Gasper Munishi alisema usiri unaliojengeka ndani ya CCM umeanza kukipotezea dira chama hicho kwa kuwa baadhi ya watendaji wake wanautumia kujilimbikizia mali kwa njia isiyo halali.

Alisema usiri huo ambao umejengeka zaidi tangu kuvunjika kwa Azimio la Arusha katika serikali ya awamu ya pili, pia unawakumbatia viongozi wasio waadilifu na wasiowajibika kwa umma, jambo ambalo ni hatari kwa uhai wa chama na uchumi wa nchi.

Pamoja na mambo mengine, Azimio la Arusha ambalo ilibadilishwa na Azimio la Zanzibar, lilipiga marufuku viongozi wa chama na umma kujilimbikizia mali isiyolingana na kipato chao.

"CCM haitaki kuondokana na usiri iliourithi kutoka kwa wakoloni, matokeo yake mtu aliyepata pensheni ya Sh35 milioni ana miradi ya zaidi ya Sh800milioni baada ya kustaafu," alisema Munishi.

Alisema tofauti na usiri wa enzi za ukoloni ambao ulitumika kutengeneza matabaka na kurahisisha utawala, usiri ndani ya CCM hauna faida zaidi ya kuondoa uadilifu, uwazi, uwajibikaji na kuchochea rushwa katika chama.

Akizungumzia kuhusu mjadala wa tuhuma za ufisadi, Profesa Munishi alisema kuwa unatokana na usiri uliojengeka katika mikataba mbalimbali, ambapo serikali kupitia kikundi cha watalaam kinatengeneza sera na wabunge wanalazimishwa kuipitisha kwa kuwa hawakushirikishwa tokea mwanzo.

Profesa Munishi ambaye ni Mhadhiri wa Uchambuzi wa Sera katika chuo hicho, alisema kuwa kanuni zinasema kuwa ni kawaida kwa mpeleka hoja kutengeneza sera zinazolinda maslahi yake, hivyo hoja za Zitto Kabwe na Dk Willibrod Slaa zina mantiki kwa kuwa hawakushirikishwa katika kuandaa sera za mikataba hiyo.

"Kanuni inasema maslahi ya kwanza ya hoja, ni ya mpeleka hoja mwenyewe, Serikali ndio inayopeleka hoja bungeni kwa nini wabunge ambao sio waandaaji wa hoja hiyo wasihoji kwa maslahi ya wananchi wanaowawakilisha?" alihoji Munishi.

Alisema hoja za Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe na Mbunge wa Karatu, Dk Slaa kuhusu utata wa mikataba ya Benki Kuu (BoT) na mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, ni matokeo ya usiri huo na kwamba hoja hizo hazipaswi kuchukuliwa kisiasa kwa kuwa wabunge hao ni wawakilishi wa umma.

"CCM isibweteke na ushindi wa asilimia 80 ulioupata wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, inahitaji kujichunguza zaidi na kuondoa mapungufu yake ili kujinusuru," alisema.

Aliishauri serikali kuanza kuwashirikisha wabunge katika taratibu za uandaaji wa sera ili kuondoa uwezekano wa kutengeneza sera zinazolinda maslahi ya wachache.

Profesa mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini alisema matukio ya kushutumiana, tuhuma za ufisadi, kiburi, kuongezeka kwa kasi na vitendo vya rushwa na malumbano baina ya viongozi na waanzilishi wa Chama cha Mapinduzi ni ishara ya chama hicho kuelekea ukingoni.

Akinukuu kitabu cha 'Mwisho wa Utawala wa Chama Kimoja' kilichotungwa na Doroth Solinga, Mhadhiri huyo alisema historia inaonyesha kuwa chama kinachokaa madarakani kwa muda mrefu kama CCM kina tabia ya kulewa madaraka na dalili za mwisho wake ni kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi, rushwa, kutoaminiana miongoni mwa watandaji wake na malumbano ya mara kwa mara.

"Ndiyo kwanza nimeingia ofisini sijui niseme nini, lakini historia inaonyesha kuwa chama kilichokaa madarakani kwa muda mrefu kama CCM kinafikia mwisho kwa kasi ya vitendo vya rushwa na malumbano," alisema Profesa huyo.

Alisema aina hiyo ya mwisho wa utawala wa chama, ilijitokeza kwenye miaka ya hivi karibuni katika nchi za Mexico, Taiwan na Brazil ambako vyama vikongwe vilianza kupoteza dira kwa kukumbatia rushwa kisha kufilisika sera na kufa kabisa.

Alisema malumbano ya viongozi waandamizi wa CCM kuhusu tuhuma za ufisadi huku baadhi yao wakitaka waliotuhumiwa kuwajibika na wengine kuwatetea, hayana tofauti na yale yaliyotokea katika nchi hizo na kusababisha mwisho wa utawala wa vyama hivyo.

Profesa Ernest Mallya aliishauri CCM kujibu hoja za tuhuma za ufisadi zilizoelekezwa kwa baadhi ya wanachama wake kwa kuwatoa 'kafara' wahusika wakuu wa tuhuma hizo ili kujijengea imani kwa jamii.

Alisema CCM inatakiwa kuchukua hatua madhubuti kujirudishia imani yake kwa jamii kwa kuwafichua na kuwawajibisha wala rushwa ili jamii irudishe imani kwake na kuendelea kukiweka madarakani.

Alisema baadhi ya watendaji wa chama hicho waliotuhumiwa kwa ufisadi wameshindwa kuwajibika kutokana na ulafi, ukweli wa tuhuma, ukosefu wa elimu ya demokrasia na kulewa madaraka.

"Ninachoweza kusema ni kwamba wameshindwa kuwajibika ama kwa sababu ya njaa, kutaka kuharibu ushahidi wa tuhuma, ukosefu wa elimu ya demokrasia au kulewa madaraka,� alisema.

Alisema katika nchi zinazoendelea, viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanawajibika wenyewe kwa kujiondoa madarakani kupisha uchunguzi huru, ila hili haliwezi kufanyika nchini kutokana na kuoza kwa mfumo mzima wa maadili.

CCM inahitaji kuwatoa mhanga baadhi ya watendaji wake ili jamii ijue kuwa iko serious (makini) vinginevyo kwa kweli imeanza kupoteza imani kwa wananchi,"alisema.

Mhadhiri Msaidizi wa Sayansi ya Jamii, Mathew Agripinus, amesema hakuna sababu kwa viongozi waliotuhumiwa kwa ufisadi kushindwa kuwajibika zaidi ya ukosefu wa maadini ya uongozi na kulewa madaraka.

Alisema baadhi ya viongozi wa CCM wamelewa madaraka na kusahau wajibu wao kwa jamii jambo ambalo linawafanya waone kama madaraka ni haki yao na siyo dhamana.

Alisema uwajibikaji ni tofauti pekee kati ya kiongozi na mtawala na mtu mwenye madaraka asiyependa kuwajibika hafai kuiongoza jamii.

Alisema viongozi wanatakiwa kujitofautisha na watawala kwa kuwajibika kwa jamii iliyowaweka madarakani badala ya kujifungia maofisini na kufanya mambo wanayotaka wao

Kauli za viongozi hao zimekuja huku kukiwa na mjadala baina ya wana-CCM, baadhi yao wakitaka waliotuhumiwa kwa ufisadi kuwajibika kwa kujiuzulu kupisha uchunguzi huru na wengine kuwatetea viongozi hao.

Baadhi ya viongozi wanaotaka watendaji wa CCM waliotuhumiwa kwa ufisadi kuwajibika ni Kada mwanzilishi wa Chama hicho Joseph Butiku, Makamu Mwenyekiti wa CCM, John Malecela na Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) Dk Mohammed Gharib Bilal.

Wakati kauli hizi zikitolewa na makada hawa, kuna wengine ambao wamekuwa wakitetea watuhumiwa hawa kutojiuzulu. Makada hao ni Kingunge Ngombale Mwiru na Agrey Mwanri.

Hata hivyo, Waziri Mkuu, Edward Lowassa alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa uamuzi wa kuwajibika kwa tuhuma hizo upo kwa watuhumiwa wenyewe au Rais aliyewateua.
 
HAWA si ndio wale wa redet?
wafanye utafiti then utaona jinsi wanavyoweza kutoa majibu uwa JK bado anaongoza kwa kupendwa na kuongoza taifa vizuri sana .
 
Ama ukweli ukipenda chongo utaita kengeza! Angalia alama za nyakati kaka! Watanzania hawana kawaida ya kuzomea viongozi wao. Sasa hivi hili la kuzomea ni kama kazi maana watu wamevumilia wamechoka.
 
HAWA si ndio wale wa redet?
wafanye utafiti then utaona jinsi wanavyoweza kutoa majibu uwa JK bado anaongoza kwa kupendwa na kuongoza taifa vizuri sana .

HAWA NI WAAJIRIWA TU,ALIYESHIKA MPINI NI MKANDARA..TEGEMEA MAAMUZI YA MKANDARA TU..!
 
Ila hapo Nkandara naye nadhani kakaa kona sasa,

Bado anasondwa na uamuzi wake wa kumzuia Zitto asiungurume chuo kwa ajili ya kulinda ubest na Muungwana,

Sasa akiangalia vibaya akapika hizi data za REDET this time, anaweza jikuta chungu kimoja na kina Karamagi ( Mtazamo wangu lakini)
 
Chama Cha Madalali + Academy ya Wezi na wanyang'anyi.

Poleni ndugu zangu mnaopambana katika mazingira magumu kujiokoa huku mliowaajiri wakikomaa kukumalizeni mazima.
 
Na Kizitto Noya
Mwananchi

BAADHI ya wahadhiri wa Sayansi ya Siasa na Jamii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wametabiri kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaelekea kufa, kwa kuwa dalili zimeanza kuonyesha kuwa chama hicho kimepoteza dira na mwelekeo.

Wakizungumza na Mwananchi jana kwa nyakati tofauti, wahadhiri hao walisema CCM inatakiwa kujitazama upya na kuondoa kiburi na usiri unaotawala ndani ya chama hicho kwa kuwa ndivyo vitakavyokimaliza.

Wamesema kwamba usiri katika chama hicho unasabishwa na watendaji wake kutopenda kuweka wazi utendaji wao wa kazi unaoathiri uwajibikaji wao kwa umma.

Profesa Gasper Munishi alisema usiri unaliojengeka ndani ya CCM umeanza kukipotezea dira chama hicho kwa kuwa baadhi ya watendaji wake wanautumia kujilimbikizia mali kwa njia isiyo halali.

Alisema usiri huo ambao umejengeka zaidi tangu kuvunjika kwa Azimio la Arusha katika serikali ya awamu ya pili, pia unawakumbatia viongozi wasio waadilifu na wasiowajibika kwa umma, jambo ambalo ni hatari kwa uhai wa chama na uchumi wa nchi.

Pamoja na mambo mengine, Azimio la Arusha ambalo ilibadilishwa na Azimio la Zanzibar, lilipiga marufuku viongozi wa chama na umma kujilimbikizia mali isiyolingana na kipato chao.

"CCM haitaki kuondokana na usiri iliourithi kutoka kwa wakoloni, matokeo yake mtu aliyepata pensheni ya Sh35 milioni ana miradi ya zaidi ya Sh800milioni baada ya kustaafu," alisema Munishi.

Alisema tofauti na usiri wa enzi za ukoloni ambao ulitumika kutengeneza matabaka na kurahisisha utawala, usiri ndani ya CCM hauna faida zaidi ya kuondoa uadilifu, uwazi, uwajibikaji na kuchochea rushwa katika chama.

Akizungumzia kuhusu mjadala wa tuhuma za ufisadi, Profesa Munishi alisema kuwa unatokana na usiri uliojengeka katika mikataba mbalimbali, ambapo serikali kupitia kikundi cha watalaam kinatengeneza sera na wabunge wanalazimishwa kuipitisha kwa kuwa hawakushirikishwa tokea mwanzo.

Profesa Munishi ambaye ni Mhadhiri wa Uchambuzi wa Sera katika chuo hicho, alisema kuwa kanuni zinasema kuwa ni kawaida kwa mpeleka hoja kutengeneza sera zinazolinda maslahi yake, hivyo hoja za Zitto Kabwe na Dk Willibrod Slaa zina mantiki kwa kuwa hawakushirikishwa katika kuandaa sera za mikataba hiyo.

"Kanuni inasema maslahi ya kwanza ya hoja, ni ya mpeleka hoja mwenyewe, Serikali ndio inayopeleka hoja bungeni kwa nini wabunge ambao sio waandaaji wa hoja hiyo wasihoji kwa maslahi ya wananchi wanaowawakilisha?" alihoji Munishi.

Alisema hoja za Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe na Mbunge wa Karatu, Dk Slaa kuhusu utata wa mikataba ya Benki Kuu (BoT) na mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, ni matokeo ya usiri huo na kwamba hoja hizo hazipaswi kuchukuliwa kisiasa kwa kuwa wabunge hao ni wawakilishi wa umma.

"CCM isibweteke na ushindi wa asilimia 80 ulioupata wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, inahitaji kujichunguza zaidi na kuondoa mapungufu yake ili kujinusuru," alisema.

Aliishauri serikali kuanza kuwashirikisha wabunge katika taratibu za uandaaji wa sera ili kuondoa uwezekano wa kutengeneza sera zinazolinda maslahi ya wachache.

Profesa mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini alisema matukio ya kushutumiana, tuhuma za ufisadi, kiburi, kuongezeka kwa kasi na vitendo vya rushwa na malumbano baina ya viongozi na waanzilishi wa Chama cha Mapinduzi ni ishara ya chama hicho kuelekea ukingoni.

Akinukuu kitabu cha 'Mwisho wa Utawala wa Chama Kimoja' kilichotungwa na Doroth Solinga, Mhadhiri huyo alisema historia inaonyesha kuwa chama kinachokaa madarakani kwa muda mrefu kama CCM kina tabia ya kulewa madaraka na dalili za mwisho wake ni kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi, rushwa, kutoaminiana miongoni mwa watandaji wake na malumbano ya mara kwa mara.

"Ndiyo kwanza nimeingia ofisini sijui niseme nini, lakini historia inaonyesha kuwa chama kilichokaa madarakani kwa muda mrefu kama CCM kinafikia mwisho kwa kasi ya vitendo vya rushwa na malumbano," alisema Profesa huyo.

Alisema aina hiyo ya mwisho wa utawala wa chama, ilijitokeza kwenye miaka ya hivi karibuni katika nchi za Mexico, Taiwan na Brazil ambako vyama vikongwe vilianza kupoteza dira kwa kukumbatia rushwa kisha kufilisika sera na kufa kabisa.

Alisema malumbano ya viongozi waandamizi wa CCM kuhusu tuhuma za ufisadi huku baadhi yao wakitaka waliotuhumiwa kuwajibika na wengine kuwatetea, hayana tofauti na yale yaliyotokea katika nchi hizo na kusababisha mwisho wa utawala wa vyama hivyo.

Profesa Ernest Mallya aliishauri CCM kujibu hoja za tuhuma za ufisadi zilizoelekezwa kwa baadhi ya wanachama wake kwa kuwatoa 'kafara' wahusika wakuu wa tuhuma hizo ili kujijengea imani kwa jamii.

Alisema CCM inatakiwa kuchukua hatua madhubuti kujirudishia imani yake kwa jamii kwa kuwafichua na kuwawajibisha wala rushwa ili jamii irudishe imani kwake na kuendelea kukiweka madarakani.

Alisema baadhi ya watendaji wa chama hicho waliotuhumiwa kwa ufisadi wameshindwa kuwajibika kutokana na ulafi, ukweli wa tuhuma, ukosefu wa elimu ya demokrasia na kulewa madaraka.

"Ninachoweza kusema ni kwamba wameshindwa kuwajibika ama kwa sababu ya njaa, kutaka kuharibu ushahidi wa tuhuma, ukosefu wa elimu ya demokrasia au kulewa madaraka,� alisema.

Alisema katika nchi zinazoendelea, viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanawajibika wenyewe kwa kujiondoa madarakani kupisha uchunguzi huru, ila hili haliwezi kufanyika nchini kutokana na kuoza kwa mfumo mzima wa maadili.

CCM inahitaji kuwatoa mhanga baadhi ya watendaji wake ili jamii ijue kuwa iko serious (makini) vinginevyo kwa kweli imeanza kupoteza imani kwa wananchi,"alisema.

Mhadhiri Msaidizi wa Sayansi ya Jamii, Mathew Agripinus, amesema hakuna sababu kwa viongozi waliotuhumiwa kwa ufisadi kushindwa kuwajibika zaidi ya ukosefu wa maadini ya uongozi na kulewa madaraka.

Alisema baadhi ya viongozi wa CCM wamelewa madaraka na kusahau wajibu wao kwa jamii jambo ambalo linawafanya waone kama madaraka ni haki yao na siyo dhamana.

Alisema uwajibikaji ni tofauti pekee kati ya kiongozi na mtawala na mtu mwenye madaraka asiyependa kuwajibika hafai kuiongoza jamii.

Alisema viongozi wanatakiwa kujitofautisha na watawala kwa kuwajibika kwa jamii iliyowaweka madarakani badala ya kujifungia maofisini na kufanya mambo wanayotaka wao

Kauli za viongozi hao zimekuja huku kukiwa na mjadala baina ya wana-CCM, baadhi yao wakitaka waliotuhumiwa kwa ufisadi kuwajibika kwa kujiuzulu kupisha uchunguzi huru na wengine kuwatetea viongozi hao.

Baadhi ya viongozi wanaotaka watendaji wa CCM waliotuhumiwa kwa ufisadi kuwajibika ni Kada mwanzilishi wa Chama hicho Joseph Butiku, Makamu Mwenyekiti wa CCM, John Malecela na Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) Dk Mohammed Gharib Bilal.

Wakati kauli hizi zikitolewa na makada hawa, kuna wengine ambao wamekuwa wakitetea watuhumiwa hawa kutojiuzulu. Makada hao ni Kingunge Ngombale Mwiru na Agrey Mwanri.

Hata hivyo, Waziri Mkuu, Edward Lowassa alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa uamuzi wa kuwajibika kwa tuhuma hizo upo kwa watuhumiwa wenyewe au Rais aliyewateua.
Mbna uzi wa BAK umefukuliwa toka mwaka 2007 hadi leo tarehe 7 Sept 2023 kulikoni? Mwana JF mwandamizi #BAK yuko wapi?
 
Makampuni makubwa ya biashara, wakigundua au kuhisi wanaanza kupoteza wateja, hukaa chini na kufikiria chanzo cha wateja wao kupotea au kuwaacha na kufuata bidhaa hizohizo kwenye makampuni mengine (competitors).

Wakigundua tatizo lililosababisha wateja wao kuhama, hujirekebisha haraka na ikibidi kuanza kufanya "promotion" ya bidhaa zao. Hapo wateja wao hubaki (retain), na wale waliokimbia wanarudi, na kuvutia wateja wengine wapya. Baada ya muda mfupi kampuni inasimama tena kama zamani.

Nakumbuka miaka kadhaa huko nyuma kulikuwa na kampeni ya kujivua gamba. Ilisaidia sana, kwani wateja waliokata tamaa na kutaka kuhama walibaki, na wale waliohama, baadhi walirudi.

Kumbe nyoka akikomaa sana, hujivua gamba na kuonekana hajazeeka, na huanza na nguvu mpya na ari mpya. Akizeeka tena anajivua gamba tena. Kumbe nyoka ili kujiweka imara, mwenye afya na nguvu, hujivua gamba mara kwa mara (sio mara moja tu).
 
Ubaya ni kwamba habadiriki kuwa kipepeo akijivua gamba.

Anabaki kuwa nyoka tena anakua na ari mpya zaidi na nguvu mpya zaidi na hapo kazi lazima iendelee ilipoishia.
 
Hapa ndio mjiulize 2007 kiongozi alikuwa nani, na leo 2023 kiongozi ni nani, halafu muone jinsi hivyo vichwa panzi viwili vinavyofanana.
 
Sawa, habadiliki kuwa kipepeo, anabaki kuwa nyoka vilevile, lakini mkuu ujuwe kuna nyoka wa aina nyingi; kuna weusi, wa kahawia, wa njano, wa kijani, wa kijivu, nk. Baadhi ya hawa wako "very sensintive". Hawa nyoka wa kijani huwa waoga sana, hivyo wakimwona adui huchukua tahadhari haraka sana! Ndio maana ni nadra sana kumkuta nyoka wa kijani kauwawa. Aliyewahi kumkuta nyoka wa kijani kauwawa atuambie, na alimkuta katika mazingira gani yaliyosababisha kifo chake!
 
Back
Top Bottom