Wasomi waamua kumuanika Makamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi waamua kumuanika Makamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Dec 7, 2009.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wasomi waamua kumuanika Makamba
  Thobias Mwanakatwe
  Mtandao wa Wasomi na Wataalam Mkoa wa Mbeya, umemshambulia Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na kumuonya kuacha kuingiza porojo na utani anapojibu hoja za msingi zinazowagusa Watanzania kwani anakiweka chama katika wakati mgumu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.
  Mtandao huo ulitoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa habari jana, kuelezea kauli ya Makamba aliyoitoa Ijumaa iliyopita alipoitisha mkutano kujibu mapigo dhidi ya taarifa zilizoripotiwa katika kongamano la Mwalimu Nyerere lililofanyika wiki iliyopita.
  Katika kongamano hilo, vyombo vya habari kadhaa viliripoti kwamba baadhi ya watu wanashauri kuwa Rais Jakaya Kikwete atoswe kwa vile anasita kufanya maamuzi magumu ndani ya chama hicho.
  Mwenyekiti wa mtandao huo, Prince Mwaihojo, alisema tatizo la Makamba ni kupenda kuingiza porojo na utani wakati wa kujibu hoja za msingi ambazo zinaelekezwa kwa chama na serikali hali ambayo imesababisha wananchi na viongozi kutokuwa na imani naye.
  Mwaihojo ambaye ni mwanachama wa CCM mwenye kadi namba 725928 aliyoikata mwaka 2000 katika tawi la CCM Ghana, jijini Mbeya, alisema Makamba ni mzigo kwa chama kutokana na kila mara kuingiza porojo na utani hata katika mambo ya msingi ambayo yanakuwa yanalalamikiwa na Watanzania.
  “Makamba ajibu hoja: hakuna Mtanzania asiyefahamu kuwa Rais Kikwete amekuwa mgumu katika kuchukua maamuzi dhidi ya wanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi, na hayo ndiyo malalamiko ya msingi aliyopaswa kuyajibu na siyo kuingiza porojo zake ambazo tumezizoea,” alisema Mwaihojo.
  Mwaihojo ambaye aligombea ubunge uchaguzi wa 2005 katika Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CCM na kuangushwa kwenye kura za maoni, alisema Makamba ni miongoni mwa viongozi ambao hawatambui dhamana na thamani ya nafasi walizonazo katika chama na umma na ndiyo maana hawana mtazamo mpana wa kujua kwa sasa Watanzania wanataka nini.
  “Makamba asiwe mropokaji awe anajenga hoja na kujua nini umma wa Watanzania unataka, anawaondoa watu kwenye hoja za msingi analeta vichekesho na porojo, hii ni dharau kwa wananchi na kuwafanya hawana akili,” alisema Mwaihojo.
  Mwenyekiti huyo alisema udhaifu wa kiutendaji unaoonyeshwa na Makamba, ndiyo umeanza kusababisha umaarufu wa CCM kuanza kuporomoka taratibu kadri siku zinavyoendelea ikilinganishwa na miaka ya nyuma hali ambayo kama chama hakitachukua tahadhari Uchaguzi Mkuu wa 2010 utakuwa mgumu kwa chama hicho.
  Alisema chama kinapaswa kujiuliza mara kadhaa “hivi kuendelea kuwa na kiongozi kama Makamba kitapiga hatua kimaendeleo au kitadidimia kwa sababu kuwa kiongozi ndani ya chama kikogwe kama CCM, lazima mtu awe makini anapojibu hoja na malalamiko yanayotolewa na Watanzania ambao ndio wanakiwezesha chama kiendelee kushika hatamu ya uongozi.
  Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa iliyopita, Makamba alidai tuhuma dhidi ya Rais Kikwete zinatolewa na watu wenye visasi, walioshindwa uchaguzi na ambao wanafadhiliwa na matajiri wale wale wanaoitwa mafisadi wa CCM.
  Makamba alidai tuhuma hizo zimejengwa katika misingi ya chuki kwani wengi wa makada wa chama hicho waliokuwa wakizungumza katika kongamano hilo, ama wao wenyewe au wagombea wao waliangushwa katika harakati zao za kisiasa huko nyuma.
   
 2. A

  AG Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 70
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 25
  Rooney ni maarufu kushinda Manchester United= Kikwete ni maarufu kushinda CCM
  Huo ndio ulinganisho anaomanisha Mgosi wa ndima
   
 3. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee aliishia darasa la ngapi? anadiriki kuwatukana wazee ni WEHU kwa kusema ukweli? ...... @@@@ .....
   
 4. M

  Mwanaume Senior Member

  #4
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  wamwache kikongwe wa watu Makamba. He is only good for nothing. Mwenzenu anatetea kitumbua chake tu, akamate pension yake ili apumzike na mafisadi muda si mrefu.
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Uzee unamsumbua huyo! Wamshauri akapumzike sasa
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tutakuwa tunarudia yale yale. Chama cha kishkaji kitazaa serikali ya kishkaji pia. Ukiangalia jinsi ilivyo rahisi kummwaga Makamba utashangaa kwanini bado yupo na anaboronga? Jibu mstari wa kwanza wa message hii.
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,009
  Trophy Points: 280
  Makamba kaja na hoja kitabu cha warumi kuwa mamlaka zote zimewekwa na Mungu hivyo ziheshimiwe. Asichoweza kupambanua makamba ni ikiwa hizo mamlaka zimewekwa na Mungu haina maana kwamba zimetakaswa. Hivyo kuna kazi binafsi ya hizo mamlaka kujitakasa zenyewe kwa kipimo cha haki ya Mungu la sivyo Mungu mwenyewe huzipindulia mbali na ni kwa kupitia WATU tena wale wale aliowatumia kuzisimika hizo mamlaka. Na Mungu amefanya hivyo mara nyingi na kujivunia hiyo kazi ya kuzing'oa kwamba ni UKOMBOZI!!
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Safi,

  Mzee makamba majuzi kule Dodoma mwakumbuka wabunge wa CCM walirushiana maneno na baaadae yeye aka sema Umri wa mwanadamu kuishi ni miaka 70 na yeye na miaka nadhani 71 kwahiyo ana miaka 4 iliyobani ya kuishi tumwache, sas hizo ndizo dalili za mwisho wa uhai wake mawazo kufilisika na kutoa kauli za ajabu.

  Siku ile hakujibu hoja na hakulinda hoja yake esp kuhusu matajiri kuwa na nguvu ndani ya CCM hatukutaka kusikia swala la matajiri wanachangia nini CCM au maskini wanachangia nini CCM, swala lilikuwa kwanini matajiri wananguvu,nafasi nyingi ndani ya CCM? kipindi cha Mwl.JKN matajiri walikuwepo ila hawakuwa na nguvu lakini walikichangia chama na hii ni kwa kuwa Mwl.JKN alikuwa na hoja ndani ya chama na chama kikawa na uadilifu na uongozi bora ingawa pia kulikuwepo na mapungufu kama tulivyo wote sie ni binadamu, ila hii CCM ya kipindihiki kwa kweli wamekosa Dila kabisa, Hawapendi kukosorewa sasa hawa ni viongozi gani wao ni Mungu au??

   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  "Ukiita Masikini utapata Kuku"....Yusufu Makamba!
   
 10. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Angekuwa amesoma asingeishia uluteni (Lt.) Natumaini std viii ya enzi hizo.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,204
  Trophy Points: 280
  Kwa maana nyingine CCM haihitaji kuku, hivyo badala ya kuwaita maskini ni bora iwaite matajiri waliotajirika kupitia ufisadi.
   
 12. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280

  Kwani uluteni unataka elimu gani?? Mkulu wa kaya mbona naye aliishia uluteni na Degree yake............??

  Mbona akina msuguli, Mayunga na wengine wengi walikuwa mageneral bila hata hayo madarasa??

  May be sema huku jeshini waligundua hana kipaji cha kuongoza kama mkulu wetu. Ila siasa za bongo ndiyo zinawafaa watu asio na sifa za kuongoza bali sifa za kupiga domo tu kama akina ...........!!! Wako wengi tu mpaka naona kuwataja wachache ni kuwaonenea tu!!!
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  hahahahaha,

  ngoja niende jukwaa la jokes nkapumdhike
   
 14. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwakalinga anayo point kusema:

  “Makamba asiwe mropokaji awe anajenga hoja na kujua nini umma wa Watanzania unataka, anawaondoa watu kwenye hoja za msingi analeta vichekesho na porojo, hii ni dharau kwa wananchi na kuwafanya hawana akili."

  Mzee Makamba anasahau kwamba Chama anachoongoza ni Chama cha Wananchi wenye akili timamu waliopiga kura na kutoa uongozi kwa viongozi walio madarakani hivi sasa na hatimaye yeye naye kuambulia cheo alichonacho.

  Yaliyozungumzwa kwenye Kongamano lile mengi ni yale ambayo yamekuwa yakizingumzwa na wananchi mitaani wakiwemo wanachama wenyewe wa CCM. Haiwezekani Wazee wazima na akili zao waende pale kuzungumza mambo yasiyo na maana kwa mustakabali wa Taifa. Naamini kabisa Mzee Makamba asingelikuwa kwenye nafasi aliyonayo, naye pia angelikerwa kama ambavyo Wazee wengine kama yeye wanavyokerwa na angelikuwa mstari wa mbele kuungana na Wazee wenzake kuelezea mapungufu yaliyopo yanavyohatarisha mustakabali wa Taifa letu.

  Pia Mzee Makamba amejaribu kukwepa ukweli kudai kwamba yaliyosemwa kwenye kongamano lile yamesemwa kutokana na visasi vya uchaguzi uliopita miaka 4 iliyopita. Hivi Wazee wa nchi yetu waache kusema pale wanapoona mambo yanakwenda kombo kwa kuwa tu walitumia haki yao ya kidemokrasia kugombea uongozi na kukosa? Mimi nadhani wenye visasi hapa ni viongozi kama Mzee Makamba ambao hawataki kuwasikiliza wazee wenzao kwa sababu tu waligombea uongozi mwaka 2005.

  Jambo la busara ambalo angeliweza kulifanya Mzee Makamba akiwa Katibu Mkuu wa Chama tawala ni kuchukua mawazo yaliyotolewa kwenye Kongamano lile na Wazee wa nchi hii na kuyapeleka kwenye vikao vya Chama ili yajadiliwe na yafanyiwe kazi kwa manufaa ya taifa zima. Kejeli hazisaidii kuondoa ukweli wa mambo.

  Kwa kuwa Mzee Makamba anapenda sana 'vibwagizo' basi bora akumbushwe kwamba kuna kibwagizo kimoja kinasema "Mficha ficha maradhi kifo kitamuumbua". Tusitakie nchi yetu ifike huko kwa viburi visivyokuwa na sababu! Pia mchezo wa akina Makamba wa kutupa madongo/mawe kwenye bwawa lililojaa sie akina vyura ni mauti yetu sote ndio maana wapo vyura waliojitolea kupiga kelele.
   
 15. Laface77

  Laface77 JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 1,301
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Mtu kama katibu mkuu wa chama tawala kuwaita viongozi wenzake wehu ni aibu kwa taifa na aliyempa dhamana hiyo.
   
 16. c

  chelsea Member

  #16
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umenena mkuu hapo juu
   
Loading...