Wasomi wa vyuo vikuu mmeelimika kweli?

Uta Uta

JF-Expert Member
Feb 2, 2016
3,739
8,736
Habari za asubuhi?

Kumekuwa na kujitapa kwa wasomi wetu wa vyuo vikuu kwamba wasomi ndio kila kitu na wengine wakijinasibu fani fulani ndio wenye akili zaidi kuliko wengine.

Nimebahatika kutembelea vyuo viwili ambavyo ni miongonu mwa vyuo maarifu sana hapa Tanzania. Jambo la kushangaza nilipoenda vyooni sikuamini macho yangu. Vyoo ni vichafu, maji yapo ila watu wamejisaidia bila hata kuflash, haja ndogo zinatiririka kama maji ya mvua, miswaki, vipande vya sabuni, machupa ya maji yametupwa ovyo chooni.

Washing area ndio usiseme watu wamepigwa mswaki na kuteama bila kumwaga maji. Sasa najiuliza wasomi ninyi ambao mnashindwa hata kuflash vyoo, dust bin zipo mnatupa taka ovyo, mnasoma nini huko chuoni?

Huo mda mnaoutumia kujidai humu mitandaoni kwa nini msiutumie kuflash vyoo? Je mnatufundisha nn sisi ambao tunawategemea ninyi wasomi wetu?. Naomba kuwasilisha, nimesema vyuo viwili tu ambapo nimekuta haya vingine sijafika
 
Habari za asbuhi? Kumekuwa na kujitapa kwa wasomi wetu wa vyuo vikuu kwamba wasomi ndio kila kitu na wengine wakijinasibu fani fulani ndio wenye akili zaidi kuliko wengine.
Nimebahatika kutembelea vyuo viwili ambavyo ni miongonu mwa vyuo maarifu sana hapa Tanzania. Jambo la kushangaza nilipoenda vyooni sikuamini macho yangu. Vyoo ni vichafu, maji yapo ila watu wamejisaidia bila hata kuflash, haja ndogo zinatiririka kama maji ya mvua, miswaki, vipande vya sabuni, machupa ya maji yametupwa ovyo chooni. Washing area ndio usiseme watu wamepigwa mswaki na kuteama bila kumwaga maji. Sasa najiuliza wasomi ninyi ambao mnashindwa hata kuflash vyoo, dust bin zipo mnatupa taka ovyo, mnasoma nini huko chuoni? Huo mda mnaoutumia kujidai humu mitandaoni kwa nini msiutumie kuflash vyoo? Je mnatufundisha nn sisi ambao tunawategemea ninyi wasomi wetu?. Naomba kuwasilisha, nimesema vyuo viwili tu ambapo nimekuta haya vingine sijafika
UDSM lazma ipo kwenye hiyo list ya viwili.. Kataa sasa
 
Usomi hauna uhusiano na ustaharabu, kuna watu hawajasoma kabisa lakini ni wastaharabu sana na wana nidhamu nzuri.
Pili mambo ya kutokuflash choo na uchafu kwa ujumla ni swala binafsi kuna watu hawajawahi kutumia vyoo vya kuflash tangu wazaliwe na wameviona chuoni sasa matumizi kwao ni tatizo lakini pia KUNA WATU NIWACHAFU KWA ASILI NA USTAHARABU HAWANA .
 
Nakubaliana wewe ustaarabu. Ila wale tusiojua si tuulize tu, kwani ni moja ya mafunzo, au mtu anaogopa kuonekana mshamba?
 
Udsm hapo haikosi, chuo kina balaa kile, watu wasafi kwa nje, ila usithubutu kupita katika halls na pale ATA, ATB kama walekea CASS na kule chini COET kama waenda Cafeteria ya Lecturers. Full of strange smells
 
Kwa kweli ukiwaona wasomi wamependeza barabarani huwezi amini. Mtu akikuletea picha ya choo cha chuo kikuu huwezi kubali
 
Udsm hapo haikosi, chuo kina balaa kile, watu wasafi kwa nje, ila usithubutu kupita katika halls na pale ATA, ATB kama walekea CASS na kule chini COET kama waenda Cafeteria ya Lecturers. Full of strange smells
Strange smells ha ha ha ha umenivunja mbavu, umenikumbusha mbali sana
 
Back
Top Bottom