Wasomi wa Tanzania wametoa mchango gani kwenye Taifa letu mpaka sasa?

Mongoni mwa maswali ambayo wanataaluma waliyojiuliza jana katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru ni suala la kujihoji ni upi hasa mchango wa wanataaluma.

Kulingana na Profesa Shivji Mara tu baada ya uhuru wakoloni hawakutuachia Taifa ila walituachia Nchi ambayo ni eneo la kijiografia.

Katika ujenzi wa Taifa hayati Baba wa Taifa alifanikiwa kupitia siasa ya ujamaa kuanzisha Taifa la Tanzania.

Swali lakujiuliza ni upi hasa mchango wa wanazuoni limetamalaki sana leo ambapo Mzee Butiku naye alihoji law msisitizo mkubwa sana ni upi mchango wa wanataaluma?

Leo tunatambua wanataaluma ndiyo wanaosimamia na kuongoza sehemu mbalimbali ambazo kuzorota kwake au kuendelea kwake kwa kweli inatokana na wanataaluma hao.

Ufisadi na ubadhirifu tiliouona Nchini umefanywa na wanataaluma ambao kwa kweli ndiyo wanaosimamia na kuongoza sehemu mbalimbali.

Je jamii inawachukuliaje wanataaluma?Ikiwa gharama za elimu mathalani ukiangalia miundombinu ya chuo cha Dar es Salaam ukiangalia utabaini kwa kweli ni kubwa lakini jamii hairidhishwi na return.
 
Return ipo Mkuu.

Wasomi wanajitahidi kulihudumia taifa lao l. Tatizoni Wanasiasa ambao wanafanya upuuzi kwenye ishu sirius zinazohusu taaluma.

Wasomi kwa nafasi yao wamejitahidi sana kulijenga taifa hili.

Kuna barabara zilizojengwa na wakandarasi ambao ni wasomi. Kuna Majengo marefu kwa mafupi katika majiji makubwa yaliyojengwa na Wahandisi. Kuna madaraja kila kona ya nchi.

Kuna Waalimu kila kona wanaohakikisha watoto wanaondoa ujinga kichwani. Kuna Madaktari ambao siku hizi wamekuwa wengi. Huduma za Afya zimeboreshwa angalau kidogo japo bado kuna changamoto.

Kuna mabenki na wataalamu wa fedha kila miji mkubwa. Kuna Wanasheria wanaotusaidia mambo ya sheria.

Wataalamuna wamejitahidi sana japo Wanasiasa wanazingua.
 
Kwamba return imeptkn wapi zaidi km si wanataaluma. Stupid question .watu wanapenda kucriticise wasomi na inasense 7bu watz tuna ushabiki wa kipimbi
 
Jokajeusi,

Swali gumu jibu rahisi, mchango wa wanataaluma wetu katika miaka 58 ya Uhuru. Jibu rahisi magorofa yanajengwa na madaraja yanajengwa. Material view.

Katika kutoa mlingalisho wa haki, kwa wanataaluma wetu ni bora tutumie mizania zote mbili, absolutely and relatively ili kuchangia katika mada kusudiwa.

Absolutely, wanataaluma wetu wamechangia kwa kwenye maendeleo ya nchi, tulikuwa na vyuo vichache sasa vimeongeza sana tu, wasomi wameongezeka, uchumi una kuwa kwa kasi nzuri tu. In short quantitatively yes wamechangia kama thinking tanks ya maendeleo ya taifa na nchi kwa ujumla.

Relatively, qualitatively na chelea kusema viwango vimeenda chini sana. Ubora wa elimu ni umeshuka, mazingira ya kutolea elimu, yameshuka weledi wa kazi umeshuka. Maendeleo linganishi bila ya kutafuta visingizio scapegoats, ukilinganisha na majirani zetu Kenya; Japo uwepo wa rasilimali , Tanzania ina rasilimali asilia mara mbili na zaidi ya Kenya.

Umeme sasa hivi kenya wanazalisha 2400MW, wakati Tanzania only 1540MW, Budget ya Tanzania ni 31 Trillion wakati ya Kenya ni 61 Trillion kwa fedha ya Tanzania. Unaweza ukalinganisha ukubwa wa uchumi, nakisi ya biashara yetu na vinginevyo vingi.

Wanataaluma wetu wakati wa kujitathimini ni bora wawe wazalendo zaidi ya kufikia zaidi ya wao binafsi na familia zao.
 
Hawa wasomi wetu kila kukicha wanajitapa na kijisifia na wengine wapo humu JF kuwa ni wasomi..

Sisi watanzania tunatatizo la kujivunia mambo yasiyo na tija "unajua mimi ni nani?" Mwambafication hata kama kichwani hakuna kitu, kadhalika tunajivuna hata kama hatuna cha ku deliver sana sana show off badala ya kuacha matokeo ya judge umuhimu wa mtu husika.
 
hii mada ni nyeti sana,inafaa kujadiliwa kwa kina na haowasomi ili sisi tulioishia darasa la pili b tusome comments tu,lakini cha ajabu hao wasomi kama kina le profesa mwaluko aidani anamsifu le stone kwa kumtoa jalalani,sasa tutegemee nini kama hao ndo maprofesa,
 
hii mada ni nyeti sana,inafaa kujadiliwa kwa kina na haowasomi ili sisi tulioishia darasa la pili b tusome comments tu,lakini cha ajabu hao wasomi kama kina le profesa mwaluko aidani anamsifu le stone kwa kumtoa jalalani,sasa tutegemee nini kama hao ndo maprofesa,
Kipindi tunasheherekea uhuru uliochangiwa na wanataaluma tuna mengi sana ya kuangalia na ninaomba ninapotumia neno wanataaluma nieleweke kuwa namaanisha hata Watemi wetu na wazee wa jadi kule kijijini ni wanataaluma
 
"The professional of the too long, we remain a young nation" Barrack Obama
 
Mfumo unawabeba zaidi wanasiasa kuliko wasomi wataalamu. Utaona daktari anatamani kuwa mbunge na labda awe waziri.

Mfumo hautoi nafasi kwa wataalamu wabunifu kutambulika na mchango wao kutumika katika jamii.
Nimekutana na wataalamu wawili kutoka ughaibuni nyakati tofauti walisema, Tanzania wapo wataalamu wajuzi wa fani mbalimbali, lakini tatizo, hawatambuliki, wametawanyika kama wamefichwa vile.

Inabidi ufanye jitihada kuwapata. Na ukiwapata unashangaa kumbe wapo.

Kwahiyo, wasomi na wataalamu wapo lakini sasa mfumo wa kisiasa siyo rafiki. Ni mfumo wa kulinda maslahi ya kisiasa kwanza kwa gharama zozote.

Wasomi wenye mawazo mapana kwa jamii kwa ujumla wanasita kujidhihirisha au kutoa mawazo yanayo gongana na watawala.

Wasomi wengi huamua kuchagua kanuni ya ungana na aliyekuzidi nguvu upate mkate wako.
 
Back
Top Bottom