Umasikini wa mtanzania unatokana kipato chake..ritz,
la kwanza nikukosoe, Tz kama nchi co maskini na hivyo haiwezi kuwa miongoni mwa nchi maskini duniani. Huu ni uongo uliotungiwa nyimbo za beti zinazoitwa utafiti kisha kuimbwa mara nyingi mpaka tumelazimishwa kuukubali kama ndiyo ukweli halisi.
Pili, siasa ikitamalaki na kudumu ktk kila hatamu, utaalamu hukosa kabisa nafasi. Matokeo yake jambo lolote la kitaalamu ili lipokelewe na kufanyiwa kazi lazima lipate kwanza kitu wao wanaita "political will"-utashi wa kisiasa. Ktk mfumo huu mtaalamu hawezi kuwa na mchango wa maana kwa jamii yake.
Tatizo la Tanzania si wasomi. Tatizo ni wanasiasa. Ukiangalia balaa zote zilizotukumba chanzo chake ni wanasiasa. Kuanzia IPTL, Net Solutions, Richmonduli, wasomi walitoa ushauri lakini wanasiasa wakaingilia kati. Na ukitofautiana na utashi wa wanasiasa unaundiwa zengwe, unahamishwa au kuachishwa kazi.Umasikini wa mtanzania unatokana kipato chake..
Hawa wasomi wamewasaidiaje hawa watanzania masikini ambao hawakwenda shule?
Ni kipi cha maana hawa wasomi wetu wa Tanzania wamelisadia taifa letu kutoka kwenye dimbwi la umasikini?
Kama kuna wasomi tunaomba mnijibu ni kipi mlichoifanyia taifa letu la Tanzania..
Nawakilisha...