Wasomi wa Tanzania wametoa mchango gani kwenye Taifa letu mpaka sasa?

Unategemea nini kutoka kwa mtu aliyekuwa akilazimishi akili kukariri usiku kucha kwa kuweka miguu kwenye beseni la maji baridi ili kesho akajibu mitihani? Nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 90 Reginald Mengi akiwa mwenyekiti wa baraza la mazingira alitembelea UDSM na kuwashangaa Maprof wakiendesha vimiradi vya kufuga kuku na ng'ombe watatu au wawili ili kupata lita tano au 10 za kuuza tena katika mazingira ya chuo!
 
Wewe unamawazo mazuri sana je ningetaka kujua na wewe kama msomi umechukuwa jukumu gani kuwaelimisha hao maprof ili wasikimbilie kwenye siasa, kwa hiyo unataka kuniambia kwenye siasa ni sehemu ya vilaza?, sasa ndio naanza kuamini kwa nini siasa zetu ni za kipuuzi kwa sababu vilaza wengi wamekimbilia huko, so maamuzi yao yanakuwa ya kipuuzi ndo maana maprof nao wanaamua kukimbilia huko kwani hawatendewi haki na hao vilaza, Nilikuwa COET siku moja naongea na Dr mmoja nilimsikitikia sana kwani mbali na heshima aliyonayo katika tasnia ya uhandisi alikuwa analalamika hajapewa mshahara wake mpaka trh 6 nafikiri ilikuwa january au february, so unataka kuniambia mtu huyu ataendelea na kazi yake ya kukaa UD,,,,,,?
 
mkuu maada yako nzuri sana ila imekosa ladha ya uchangiaji kwa sababu umekuwa too biased, UMELAUMU MNO kuliko kuuliza tatizo ni nini!

Jaribu kukaa chini na kujiuliza tatizo ni nini, chanzo chake, jinsi ya kutatua ukiwa ndani na nje ya box that is real an art of any great thinker

Be realistic!

1. Si kweli kuwa wasomi hawachangii chochote nchi hii, wasomi miaka yote wamefanya wanayoyeza katika mazingira magumu ya nchi hii ambayo, wengi bado wana mawazo ya kitumwa! kuwa kila chema kinatoka nje, na kila mtaalamu anatoka nje ,neither in private sector nor in government, sasa huyu mtu unataka aperform vipi? wakati nchi generally haija-invest kwenye reserach?

2. It is known beyond reasonable doubt that scientist are low paid, mchukue mtu aliyemaliza udaktari na uhandisi na compare to someone who have graduated in commerce courses.....!! life is not fair for scientist. Mtu anapoona kuwa kumbe siasa na biashara ndio highly paid watu WANAFUATA HELA MKUU hawafuati science. When you can not afford to pay school fees for you kids , when you are not sure about what you will eat now and after your retirement, then, issue that 'I am a professor is irrelevant''

3. Globalisation: was not supposed to be introduced to third world countries. because we are importing almost everything na nina amini unavaa na kutumia vitu ambavyo viko imported!!!!!!!! then, what is the position of local industries where our scientist would manifest their ability? what about tax, how government is helping local scientist? Globalisation have also killed countries like Canada, not aloneTanzania my dear. for instance in canada' malls you will see many if not all electronics stuffs are imported from china, vehicle are imported from japan etc. If big countries like Canada have been affected by globalisation wind inspite of their development, what will happen in countries like Tanzania, where, when globalisation were introducing, we where several decades far behind the developed world!!

4.Be realistic we are survivors! we need to place food on table and live! kuwa mtu alisoma udaktari na leo kakimbia is none of your business because in the first place you did not tell him to study engineering or he did not tell you he will study engineering!! Note that our system can not accomodate these scientists, our system loves to get money in easy way. Why dont you fit in the same system so that you may survive?

BTW siasa sio professional!!! kila mtu ni mwasiasa! sidhani kama kwa mtazamo wako accountant au lawayer wanatakiwa kuwa wanasiasa, kama ndivyo basi you will need to revisit your theory in division of labour

Man by nature is a political animal -Aristole
 
Kuna madokta wangapi Tanzania na kati ya hawa wangapi ni wanasiasa?vivyo hivyo kuhusu maprofesa.

Nakushauri ufanye utafiti kujua ni proportion ipi ya madokta na maprofesa wamejiingiza kwenye siasa.je kuna utofauti kati ya Tanzania na nchi nyingine?usisikilize maneno ya kijiweni ukakurupuka na kuleta wrong conclusion hapa jf.

Usisahau kuna wanasiasa wanaokuwa ma Dr mfano Mkuu wa kaya(JK) na mh lyatonga.

Halafu kuna wengine ni feki kama profesa majimarefu.

Swali: una uhakika(wa kisomi) na unachokisema?kwa sababu mimi naamini recently wafanyabiashara wamejiingiza kwa wingi kuliko hawa unaowataja.
 
Huyu mleta mada hii kakurupuka tu na ninahisi anawivu. Au mzee una kidiploma au ki degree cha kuunga unga nini?
Nchi yoyote kama Tz ambayo haina political will haiwezi kuendelea hata kama watu wasome vp.
Bado kuna huge gap between professionals na politicians nchi hii.
 
Pengine mtoa mada ni mchokozi wa aina fulani aliyekusudia kutufanya tufikirie hivi hapa Tz msomi aliyesoma kwa gharama kubwa tena pengine kwa kutumia kodi zetu au hata misaada ya wahisani anathaminiwa kiasi gani na ile taaluma yake inathaminika kiasi gani?Ukifungua macho unaona ukweli hauko hivyo-wanasiasa bila kujali viwango vyao vya elimu wanavuna zaidi kuliko wanataaluma hapa Tz! Kama tuna uchungu kweli na nchi yetu kwa nini tunaishia kuwalaumu hawa wachache wanaotafuta kujikimu na tunaacha kukosoa mfumo mzima unaowakuza wanasiasa hata wanapokuwa wanadanganya umma na kuendekeza usanii???
 
Hakuna tatizo kama hao wasomi wanajiingiza kwenye siasa. Shida ni pale wanapokuwa wanasiasa waongo na wasioaminika. Kumbukeni hata Obama ni Profesa wa Sheria!
 
wewe unamawazo mazuri sana je ningetaka kujua na wewe kama msomi umechukuwa jukumu gani kuwaelimisha hao maprof ili wasikimbilie kwenye siasa, kwa hiyo unataka kuniambia kwenye siasa ni sehemu ya vilaza?, sasa ndio naanza kuamini kwa nini siasa zetu ni za kipuuzi kwa sababu vilaza wengi wamekimbilia huko, so maamuzi yao yanakuwa ya kipuuzi ndo maana maprof nao wanaamua kukimbilia huko kwani hawatendewi haki na hao vilaza, Nilikuwa COET siku moja naongea na Dr mmoja nilimsikitikia sana kwani mbali na heshima aliyonayo katika tasnia ya uhandisi alikuwa analalamika hajapewa mshahara wake mpaka trh 6 nafikiri ilikuwa january au february, so unataka kuniambia mtu huyu ataendelea na kazi yake ya kukaa UD,,,,,,?

Ukiangalia nchi kama za Ulaya utagundua wanasiasa ni wanasiasa na wataalamu huwa hawajichanganyi kwani muda wote wako wakiumiza vichwa kufikiria jinsi ya kugundua kitu fulani. Linapokuja tatizo katika jamii huwa wana compete kutafuta solution na kila mmoja anapambana ili awe wa kwanza kuja na solution.
Sisi hapa TZ tatizo la umaskini tu limekuwa kama heredity gene ambayo itaendelea kuwepo katika mfumo wa jamii yetu na hakuna ufumbuzi wa kitaalam unaotolewa. Kwa bahati mbaya ukaanzisha project then coordinator akawa professor badala ya kutumia utaalam wake kuifanya hiyo kazi basi ataamua kuwa supervisor na kuajiri watu wenye elimu duni ili abakize hela akajengee ghorofa ya kuishi na guest house kama mradi. Katika hali kama hii tutegemee nini ?
 
Pengine mtoa mada ni mchokozi wa aina fulani aliyekusudia kutufanya tufikirie hivi hapa Tz msomi aliyesoma kwa gharama kubwa tena pengine kwa kutumia kodi zetu au hata misaada ya wahisani anathaminiwa kiasi gani na ile taaluma yake inathaminika kiasi gani?Ukifungua macho unaona ukweli hauko hivyo-wanasiasa bila kujali viwango vyao vya elimu wanavuna zaidi kuliko wanataaluma hapa Tz! Kama tuna uchungu kweli na nchi yetu kwa nini tunaishia kuwalaumu hawa wachache wanaotafuta kujikimu na tunaacha kukosoa mfumo mzima unaowakuza wanasiasa hata wanapokuwa wanadanganya umma na kuendekeza usanii???


Kuthaminiwa au kutothaminiwa kwa wasomi kunategemea sana na contribution yake kiutaalam katika jamii. tatizo ni pale tunapomaliza masomo yetu na kusubiri kupokea hata kabla ya kutoa chochote. Nafikiri wasomi watakapoanza kuonyesha walicho nacho na mchango wake kwa maendeleo ya taifa basi kuna uwezekano wa serikali kubadili mtazamo. Wasomi wengi wanasubiri favour za viongozi wa serikali ili wapate kacheo hata ka mkuu wa wilaya na hali hii imewafanya wawe wanafiki na kuingiwa na ugonjwa wa "ndio mzee" ili wasiwauzi wakuu wao. Tatizo kama la umeme lisingetakiwa liwe suala la kutafuta wawekezaji bali serikali ingeunda timu ya wataalamu wakae na kutafiti vyanzo mbadala. Once serikali ikifanya hivyo utakuta akili zote zinajitega kupata chochote na hapo gharama za vikao zikawa kubwa kuliko suluhisho au wakati mwingine suluhisho lisipatikane.

Tujiulize tunajisikiaje tunapokufa na utaalamu tuliosomea bila kuutumia hata kwa asilimia 10% au tuseme ni wrong choice ya fani kwa sababu tu ulipata ufadhilii au tulikariri na kushindwa kui-translate ile knowledge katika ulimwengu halisia?
 
huyu mleta mada hii kakurupuka tu na ninahisi anawivu. Au mzee una kidiploma au ki degree cha kuunga unga nini?
nchi yoyote kama tz ambayo haina political will haiwezi kuendelea hata kama watu wasome vp.
bado kuna huge gap between professionals na politicians nchi hii.

hapo kwenye red ndio penyewe haswaaaaaaaa!!! The issue is that dr na profs wanafanya kazi kubwa kuelimisha umma jinsi ya kufanya vitu viende kwa njia ya usahihi..shida inakuja ni kuwa wanafunzi wanapouliza kuwa sasa kwa nini mambo hayaendi unajikuta unabaki mdomo wazi.........na kuamua kuchukua hatua...........

Kagame na museveni waligundua kushinda kwenye vitabu hakuna maana wakaamua kuchukua hatua mara tui walipopata uelewa.........watanzania bado tuna damu ya kunguni!!!! Uoga mwiiiiiiiiiiiiiiiiingiiiiiiiiiiiiii kama kwamba tunaishi milele!!
 
Maprofesa na Madokta wa TZ kujiingiza ktk SIASA ni adhari za kukariri au kupenda rahisi?

Jamani, adhari ndiyo nini?
 
Wasomi wapo wengi na fani zao Ila ngoma ipo ktk kutaka kazi lazima aulizwe uzoefu wa kazi.Sasa uzoefu unatoka wapi ilhali ndio katoka shule juzijuzi tu.Upewaji wa ajira kwa wasomi wetu una vikwazo vingi mfano atakaesoma nje ya nchi na atakaesoma hapa Tanzania mkienda kuomba kazi lazima aliesoma nje atapewa nafasi ya kwanza(kipaumbele)Kupeana kazi kwa undugu nalo ni tatizo kubwa sbb haijalishi una vigezo vyote hupati kazi.
Rushwa za ngono kwa watoto wa kike,pamoja na rushwa za pesa kwa wanaume nalo hilo ni tatizo kubwa.Kifupi urasimu wa kupata kazi huwa ni mmbovu mno na hivyo hupelekea elimu yetu pia kushuka thamani.Sisi kwa sisi watanzania huwa tunajidharau na kuwapa wageni nafasi za mbele.Toothpic tunaagiza kutoka nje huu ni ulimbukeni wa ajabu sasa ndio unasema wasomi wasiingie ktk siasa?
 
Uanasiasa siyo taaluma, ni haki ya kila mtanzania (msomi au sio) kuamua kuingia katika siasa
 
Mkuu hapa umenikuna!!! Maisha yote ni siasa. tunadanganywa ili watuibie tu. tuwafuate huko huko siyo kufanya kama wao lakini.
 
Ukiangalia nchi kama za Ulaya utagundua wanasiasa ni wanasiasa na wataalamu huwa hawajichanganyi kwani muda wote wako wakiumiza vichwa kufikiria jinsi ya kugundua kitu fulani. Linapokuja tatizo katika jamii huwa wana compete kutafuta solution na kila mmoja anapambana ili awe wa kwanza kuja na solution.
Sisi hapa TZ tatizo la umaskini tu limekuwa kama heredity gene ambayo itaendelea kuwepo katika mfumo wa jamii yetu na hakuna ufumbuzi wa kitaalam unaotolewa. Kwa bahati mbaya ukaanzisha project then coordinator akawa professor badala ya kutumia utaalam wake kuifanya hiyo kazi basi ataamua kuwa supervisor na kuajiri watu wenye elimu duni ili abakize hela akajengee ghorofa ya kuishi na guest house kama mradi. Katika hali kama hii tutegemee nini ?

Kila raia ktk nchi yoyote duniani anayo haki yake kikatiba ktk kujiingiza kwenye ulingo wa kisiasa na kugombea nyadhifa aitakayo. It doesnt matter if that individual is a Dr, Prof. Scientist, Engineer, Investment baker etc
Labda cha msingi ni kujiuliza INTENTION ya huyo mgombeaji ni ipi? Kama intention ni kuingia ktk ulingo wa siasa ili kuwahudumia na kuwatetea wananchi so be it. Kama ni njaa tu basi hapo ndio tatizo linakuja.
Kwa mfano orodha ifuatayo ni ya wanasiasa ambao ni wasomi kupindukia lakini wako kwenye politics:
Bill Frist-the former senate majority leader (R)=Physician/ one of the top US cardiac surgeons
Randy Paul-senator from Kentucky (R)=Physician
Howard Dean-former governor/Dem party chairman-Physician
Tom Coburn- senator from Oklahoma (R)-physician
Joe Barton-Congressman from Texas (R)-Engineer
Jerry McNerney, Congressman form California, mathematics PhD
A list of Congressmen with science PhDs: Vernon Ehlers, Michigan, physics PhD; Rush Holt, New Jersey, physics PhD; John Olver, Massachusetts, chemistry PhD; Brian Baird, Washington, psychology PhD; and now Bill Foster, Illinois, physics PhD. Other scientists, engineers and mathematicians include: Ron Paul, Texas, biology BS, MD; Jerry McNerney, California, math PhD; Dan Lipinski, Illinois, mechanical engineering BS, engineering-economic systems MS; Nancy Boyda, Kansas, chemistry BS; Cliff Stearns, Florida, electrical engineering BS; Joe Barton, Texas, industrial engineering BS.

Kwa hiyo sio vibaya kwa wasomi kuingia ktk ulingo wa siasa, like I said before inategemea intention yao ni nini...Ulaji, Njaa, Ufisadi, ama Kuwatumikia wananchi na kutetea wanyonge?
 
Kama ndivyo hali ilivyo always tutakuwa wasindikizaji lakini wanyarwanda wanakuja kwa spidi nyuma yetu na tusipo change mindset watatupita tukiwa hatujasogea hata hatua moja.

Inaonekana wewe hujasoma vizuri. Unaongelea nchi zingine wasomi wake kutoa mchango wa elimu yao katika maendeleo ya taifa. Unasahau kwamba wanasiasa na viongozi wa nchi hizo wana amini kwamba bila wasomi hakuna maendeleo.

Ukija kwa wanasiasa na viongozi wa Tanzania tukimuondoa nyerere wana amini kwamba kukiwa na wasomi wengi siasa zao za wizi hazitakuwa na nafasi na hivyo hawatilii maanani kuthamini umuhimu wa kuwatumia wasomi kuendeleza nchi.

Umataja Rwanda, kumbe wewe hujui. Nenda pale Kigali Institute of Technology (KIST) uulize nani kaanzisha idara ya Materials Engineering kama siyo Mtanzania Prof. Bisanda ambaye alionekana hana lake hapa Tanzania alipotokea Botswana.

Nenda tena leo Rwanda uulize Prof. Mshana aliyetoka UDSM kama hayuko huko anafanya vitu vyake.

Tatizo la Tanzania ni CCM na wasomi wameona dawa pekee ni kuwafuata huko huko akina Lowasa ili wagawane kilicho baki.
 
Sasa kama proffesor anapata milioni 3 halafu mbunge millioni 12 unategemea nini kitatokea. Au Raisi anamzidi mshahara proffesor, kwa nini nulear physist asikubali kuwa makamu wa raisi. Nyie wanasiasa uchwara mmeharibu system:mod:
 
Kuthaminiwa au kutothaminiwa kwa wasomi kunategemea sana na contribution yake kiutaalam katika jamii. tatizo ni pale tunapomaliza masomo yetu na kusubiri kupokea hata kabla ya kutoa chochote. Nafikiri wasomi watakapoanza kuonyesha walicho nacho na mchango wake kwa maendeleo ya taifa basi kuna uwezekano wa serikali kubadili mtazamo. Wasomi wengi wanasubiri favour za viongozi wa serikali ili wapate kacheo hata ka mkuu wa wilaya na hali hii imewafanya wawe wanafiki na kuingiwa na ugonjwa wa "ndio mzee" ili wasiwauzi wakuu wao. Tatizo kama la umeme lisingetakiwa liwe suala la kutafuta wawekezaji bali serikali ingeunda timu ya wataalamu wakae na kutafiti vyanzo mbadala. Once serikali ikifanya hivyo utakuta akili zote zinajitega kupata chochote na hapo gharama za vikao zikawa kubwa kuliko suluhisho au wakati mwingine suluhisho lisipatikane.

Tujiulize tunajisikiaje tunapokufa na utaalamu tuliosomea bila kuutumia hata kwa asilimia 10% au tuseme ni wrong choice ya fani kwa sababu tu ulipata ufadhilii au tulikariri na kushindwa kui-translate ile knowledge katika ulimwengu halisia?

Wewe nadhani hujui unaongelea nini......nikupe swali rahisi. Daktari aliye graduate leo akatibu bure bila mshahara au aanzishe zahanati kwa shs. 500 au wewe unasemea mchango upi??

Kwanza wewe hujiulizi kwa nini hao maprof. wanaishia kuanzisha bar na guest houses? Hebu sema Mtaji wa kuwa na karakana ya Mechnical na mtaji wa kuanzisha bar upi ni mkubwa?? Nipe jibu ili nikujue vizuri.
 
Hellow. . .

Tanzania ni nchi ambayo inakua katika mambo mengi, be it positive or negative, we are moving some steps forward. Moja ya vitu ninavyovisikia

kila kukicha ni idadi kubwa ya ma-dokta na maprofessor. Kwa sasa my interest ipo kwa professors. Hivi tunaweza kupata mchango halisi wa

hawa watu katika Taifa? Wamefanya nini ambacho kwa hakika kinawastahilisha kuendelea kuitwa maprofessor? Na Je wanayo nafasi yeyote ya

kufanya chochote katika wakati kama huu ambapo almost kila kitu kinaonekana kinahitaji marekebisho?

Kwa Mfano Professor Issa Shivji aliongoza tume maalumu ya raisi mwaka 1992 iliyochambua kwa kina maswala ya ardhi Tanzania na kupelekea

Sera ya Ardhi ya taifa ya mwaka 1995 na kisha sheria mbili za Ardhi mwaka 1999! Hiyo ni katika upande mmoja. Tunamfahamu vyema kwa

maswala ya katiba.

Sasa hebu wenye data kamili watufahamishe hapa
Prof Mwalyosi
Prof Mwandosia
Prof Sarungi
Prof Palamagamba Kabudi
Prof Mkandala
Prof Makenya Maboko
Prof Mwakyusa
na wengine wengi tunaowafahamu. Thanks
 
Back
Top Bottom