Wasomi wa Tanzania sio wabunifu wanakariri makaratasi

Robinhomtoto

JF-Expert Member
May 17, 2017
238
250
Nimefanya utafiti kidogo Juu ya utendaji wa Wasomi wa kitanzania.Walio wengi wanaamini alichojifunza Chuoni ndio atakachokifanyia Kazi. Ukweli uliopo sio., matokeo yake wasomi hao wamekuwa wanafanya Kazi Kwa mazoea.

Kwa mfano pale Magogoni kuna Jengo la abiria like Jengo lina miaka zaidi ya 30 wenye mamlaka nalo Kwa elimu zao wameridhika liendelee kuwa vile.Msomi mbunifu angebuni mabadiliko makubwa ya kuliboresha Jengo lile Kwa linaingiza mapato.

Angeliinua paa, angeweka viti vizuri ili abiria waliolipa nauli wakae Kwa raha, angeweka hats Madirisha Na viyoyozi ili hata Vivuko vikichelewa Kwa kuwa abiria kakaa Kwa raha hata ona kero, wangeboresha milango ya kutokea ili abiria wasitoke kama Ng' ombe Na kukanyagana lakini yote hayo Wasomi wetu wameshindwa kubuni.

Jengo la Azam la abiria ambao biashara inafanana Na hiyo ya hapo magogoni in la kisasa.Hebu wasomi wetu kuweni wabunifu sio kukariri makaratasi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom