Wasomi wa Tanzania na koti la zamani

Marisi schweini

Senior Member
Dec 3, 2018
130
374
Wasalaam wanajukwaa..!!

Leo naomba kuongelea tatizo kubwa la wasomi wa nchi hii kutokana na uzoefu wangu mdogo tu;

Wasomi wetu wengi wanaishi katika nadharia za ZAMANI zilizowasaidia wakafaulu mitihani na kufika hapo walipo. Kwa maana nyingine tunaweza kuwaita ni watu wenye nadharia na utaalam usiolingana na kuendana na wakati uliopo.

Mfano mtu ni mechanical engineer wakati anasoma machine zilizokuwepo ni za miaka ya 80(tusisahau ndizo zinazotumika kufundishia vyuoni kwetu) leo hii unapomwambia afanye kazi kwa kutumia mashine za kisasa ilhali hajawahi kuji update utaalam wake lazima aonekane mweupe kuliko hata fundi wa mtaani.

Vivyo hivyo kwa daktari aliyesoma miaka ya 2010 leo hii zaidi ya asilimia 80 ya dawa anazotumia sio alizosoma kwenye vitabu, surgical techniques pia zimebadilika. Kwa ufupi ni kwamba dunia imeshahama kutoka mbinu alizosoma kwa kasi kubwa. Je, wasomi wetu hawa wanajishughulisha kuji update utaalam wao? Jibu ni hapana hasa kwa wengi walipo serikalini anachoweza kufanya ni kwenda kuongeza elimu tu labda alikuwa na shahada ataongeza kuwa na shahada ya uzamili ili apandishwe cheo! Kusoma ili kupanua uelewa wake aweze kuwa na tija kulingana na mabadiliko yanayotokea kila siku kwake ni hapana!

Turudi kwa wachumi wetu sio ajabu kumkuta anaamini katika falsafa za uchumi wa kijamaa za Mwalimu, swali la kujiuliza ni je, mpaka leo hii dunia haijabadilika katika nyanja za uchumi? Siasa alizoziacha Nyerere zikitawala dunia ni sawa na leo? Kwanini wasomi wetu wasije na utafiti wa njia mpya za uchumi badala ya kuendeleza zilezile?

Kuna wasomi wanaamini azimio la arusha bado linaweza kufanya kazi zama hizi unabaki unajiuliza, je, mpaka leo hii ni mabadiliko mangapi duniani yametokea toka miaka hiyo mpak sasa kuanzia mazingira, teknolojia, uchumi mpaka nyanja za kijamii.? Je, hizi sio dalili za watu wetu wasiojishughulisha akili zao ziendane na mabadiliko yaliyopo?
 
Back
Top Bottom