Wasomi wa Tanzania kwanini mko hivi au ni siasa?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
Kwa kipindi kirefu nimekuwa mfatiliaji wa midahalo mbalimbali ya wasomi katika nchi yetu ili angalau nipate LA kujifunza .

Ila nilichogundua wasomi wetu wana TABIA zifuatazo ambazo zinanifanya niwatilie shaka .

1.wasomi wengi wakiwa hawana ajira au wamekosa jambo LA kufanya huwa wanalalamika na kuikosoa serikali lakini ikitokea serikali imewapa shavuu au ajira basi hutowaSikia tena hoja zao na malalamiko kwa serikali. ..

2.kuna wasomi wengine ni mabigwa wa kulalamika kuhusu issue za ajira na kuikosoa serikali kuhusu ajira lakini ikitokea msomi huyo huyo amepata nafasi ya kufanya kazi hupenda kuwahamisha vijana wajiajili

3.kuna wasomi ambao wakiwa katika madaraka hupenda kuhamasisha vijana wajiajiri lakini ikifika kipindi cha uchaguzi ikitokea wamekosa nafasi za madaraka au ubunge wako tayali kuhama chama kuutafuta madaraka hata kwa chama kingine au kwenda mahakamanii.

Ni mengi ya kuongea haya ongeezeni na nyinyi ndugu zangu
 
Back
Top Bottom