Wasomi wa juu wa UDSM kuitwa Wapumbavu na Mwanasiasa kuna athari gani katika Taasisi hiyo ya Elimu?

Funguka mkuu, nani kasema hivyo, wakati gani, akiwa anafanya nini...ongeza nyama kwenye post yako
 
Funguka mkuu, nani kasema hivyo, wakati gani, akiwa anafanya nini...ongeza nyama kwenye post yangu

Rais JPM akiwaambia hivyo Mawaziri wake wawili Kabudi na Mpango. Na taarifa hii ilitolewa kama Nukuu katika Mtandao wa Mwananchi Online siku ile ile alipokuwa na Kikao chake na Wafanyabiashara wa Tanzania. Ukiitafuta huko unaweza ukajihakikishia zaidi tafadhali.
 
Ukiacha kufanya ulichosomea inaungana na Walaghai na Wasanii, Wafitini na Wazandiki lazima utukanwe.

Chuo hakijadharaurika, wahusika ndio Mazombi.

Na hao waliowahi Kufundishwa nae / nao wanakaa vipi pembeni ya hili neno la Pumbavu?
 
Uncle wangu ni prof pale....i wakat nafuatilia kuchagua vyuo few years ago after form six, he told me usichague UD...sikumuelewa ikabd nimuulize kwann, akaniambia this institution is no longer......i said why ? He then told me...just do what i advice you! Sijajua aliona nini maana ni few years ago yan
 
Yawezekana labda Yeye hili neno Pumbavu aliwahi Kulisikia likitajwa kwa Wasomi wa hapo kabla ya Rais JPM Kulihitimisha rasmi ile Juzi pale Ikulu aliposema kuwa amewashawaambia Pumbavu akina Kabudi na Mpango ila wameamua Kunyamaza tu.
 
Lugha za kisalfasa ni ngumu asie na ufahamu kuelewa mpaka apewe mtaalam kumuelewesha. "Mimi ni nani hata nipewe nafasi hiyo" haimaanishi ni dhaifu ila shukrani kwa mola kuonekana kati ya wengi wenye sifa kama zako. Kuna muimbaji wa Injili anaimba " Umenitoa Matopeni...(Yesu) " Hakumaanisha alikuwa mchafu wa kulala kwenye madimbwi ya matope bali ni kujishusha mbale ya mola wake
 
Yawezekana labda Yeye hili neno Pumbavu aliwahi Kulisikia likitajwa kwa Wasomi wa hapo kabla ya Rais JPM Kulihitimisha rasmi ile Juzi pale Ikulu aliposema kuwa amewashawaambia Pumbavu akina Kabudi na Mpango ila wameamua Kunyamaza tu.
Kwakweli hakuwahi niambia ila hili la juzi limenitafakarisha sana yan
 
Kwani lini kiliheshimika?

Sikumbuki. Hivi kama hawa Wasomi na Wanazuoni akina Kabudi na Mpango wameitwa Wapumbavu na wanajulikana wanatoka na wamesomea pia hapo UDSM hii haiwezi kuwa na athari katika kuwapata Wanafunzi wapya hasa katika Msimu ujao wa Septemba? Kisaikolojia huoni kwamba hili neno litawaathiri hata Wasomi wa sasa waliopo hapo UDSM kwani neno Pumbavu linauma na linadharaulisha pia.
 
Sasa sio wapumbavu? Mfano Lipumba sio mpumbavu?

Kwahiyo Mkuu nikikutana na Watu waliosoma hapo UDSM nianze Kuwapuuza kama siyo Kuwadharau kwakuwa tayari Rais JPM ameshahitimisha kwa kuwaambia akina Kabudi na Mpango hilo neno alilowaita?
 
Pumbavu ni neno LA kawaida,kama ambavyo neno dhaifu linapotumika.
Bora mpumbavu kuliko mjinga.
 
Pumbavu ni neno LA kawaida,kama ambavyo neno dhaifu linapotumika.
Bora mpumbavu kuliko mjinga.

Masahihisho kidogo Kwako na kwa faida ya wengine ni kwamba Mjinga ni Mtu ambaye anafundishika na anarekebishika ila Mtu Mpumbavu kamwe hafundishiki na ataendelea kuwa Mpumbavu mpaka anaingia Kaburini. Hii maana ya haya maneno mawili nimeitoa kwa Wataalam wa Lugha ya Kiswahili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom