Wasomi vyuo vikuu Dodoma watoa tamko kuunga mkono tamko la Jumuiya ya Wanazuoni

Sep 30, 2014
95
47
UMOJA WA WANAZUONI WA VYUO VIKUU DODOMA KUUNGA MKONO KAULI YA JUMUIYA YA WANAZUONI VIJANA TANZANIA ILITOLEWA JANA MJINI DAR ES SALAAM.

UTANGULIZI.


SISI ni mkusanyiko wa wanazuoni wanaosoma vyuo vikuu mbalimbali mkoani Dodoma, tumejitokeza kuzungumza na nyinyi waandishi wa habari kuhusiana na mambo mbalimbali yanayofanyika nchini ikiwemo suala zima la AKAUNTI YA TEGETA ESCROW.

Pia, tumejitokeza kuunga mkono kauli ya Jumuiya yetu ya vijana wanazuoni juu ya tamko lao walilolitoa kwenye vyombo mbalimbali vya habari jana na kupewa nafasi kubwa kwenye vyombo hivyo ikiwemo magazeti na radio. Tunashukuru sana kwa hilo ndugu waandishi.

AKAUNTI YA ESCROW

Kabla hatujazungumza tunapenda kuwaasa hasa wanasiasa jambo lolote ukiwa hauna uhakika nalo, usipende kulizungumzia mbele ya umma kwa kuwa mwanasiasa ni mtu makini na mwenye uelewa mpana wa mambo.

Tumekaa kwa muda mrefu tukisoma taarifa mbalimbali kwenye magazeti na kwenye mitandao kuhusiana na suala la akaunti ya ESCROW ili kujua ukweli wa suala hilo, ambalo kwa kiasi kikubwa linazidi kupotoshwa.

Tunafurahi sana kupata nafasi hiyo ya kuzungumza na nyinyi waandishi wa habari kwa kuwa ni watu muhimu na mtaweza kuhabarisha umma juu ya usahihi wa taarifa

kuhusiana na sakata hilo, baada ya kufanya utafiti wa kutosha na kuelewa mambo mengi.

Sisi wanazuoni tunawajibu mkubwa wa kuitetea nchi na kuisemea pale tunapoona kuna jambo baya limefanyika, kwa kuwa uelevu wetu umetokana na kupata elimu bora iliyotokana na kodi za watanzania wenzetu na hatupo tayari kuona mambo yakienda mrama.

Tukiwa kama wasomi vijana, tuna wajibu kwa taifa letu kulipigania ili kuhakikisha kuna usawa kwa kuwa Tanzania ni taifa huru na linahitaji kuwepo kwa wanasiasa huru na wenye maono ya kuifikisha nchi pahala salama kwa kuwa uwezo na maadili yao ni muhimu.

Pia, tunapaswa kuhakikisha nchi yetu inaendeshwa kwa kufuata misingi imara ya ukweli, uwazi, uwajibikaji na kuzingatia uhuru wa haki kwa kila mtu na watanzania waelewe kuwa kujiuzuru sio ushujaa au uzalendo. Jiulize wote waliojiuzuru ni wazalendo wa kweli wa nchi yetu?.

Wabunge wametufedhehesha, wametunyong’onyesha na wameonyesha ni jinsi gani wameshindwa kuwa wakweli kwenye kusimamia sheria na uhuru wa haki wa kila mtu(natural justice) kwa kutengeneza tuhuma na kisha kumtaka Rais Jakaya Kikwete awawajibishe watu hao.

Sote sie tunakumbuka kwamba hivi karibuni Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilitoa taarifa ya uchunguzi wake wa akaunti ya TEGETA ESCROW kwa serikali na kwa bunge na ripoti hiyo iliweza kuvuja kwenye mitandao mbalimbali

Kuvuja huko kulitusaidia sie kupata taarifa za ripoti hiyo na kuzisoma kwa umakini, ueledi na ufanisi mkubwa na kugundua kinachozungumzwa sasa ni mchezo wa kisiasa unaochezwa na wabunge wakishirikiana na wafanyabiashara mbalimbali.

Ripoti iliarifu juu ya hadidu za rejea 11 ilizopewa, pamoja na kutaja ofisi mbalimbali zilizoanza kuomba kufanyiwa uchunguzi kabla ya Ofisi ya Bunge, ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini.

Jitihada za ofisi hizo, zilisaidia kupatikana kwa taarifa bora na yenye mantiki kwa jamii na ndio maana katika uchunguzi wake, CAG hakusema kuwa ESCROW ni fedha za umma au la, pia alisema kuwa uchunguzi wake haukumtia hatiani mtu au kikundi chochote cha watu kilichohusika katika sakata hilo. Je tujiulize yale yanayozungumzwa kwenye mitandao na uamuzi wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) imepata wapi?.

Tunatambua kilichofanywa na PAC kugeuza ripoti ya CAG na kuitengeneza ripoti yao isiyojaa uzalendo wa hali ju ni kumharibia jitihada za Rais Jakaya Kikwete kuonekana ni kiongozi anayeongoza serikali ya kifisadi wakati sio kweli. Rais Kikwete amefanya mambo mengi makubwa kwa nchi hii na tutamkumbuka kwa ukarimu wake aliokuwa nao licha ya kuwepo kwa upuuzi, uzandiki unaoendeshwa na watu hasa wabunge huku yeye mwenyewe akiwa anacheka na kutoa ushahidi wa kila jambo kwenye vyombo vya habari.

Katika ripoti ya CAG pamoja na viambatanisho vyake

vyote, tumesoma na kuvirudia na hakuna iliyosema kwamba Waziri mkuu amelisababishia hasara Taifa au mawaziri wengine nao wameshiriki kuliletea hasara taifa huku wabunge wenyewe wakiwa wanafanya shughuli za kitaifa kishabiki, kichuki, kimaslahi binafsi bila kuzingatia ukweli na misingi ya Utawala bora.

Ndugu zangu, kwenye Ripoti ya CAG kumesema wazi kwamba, serikali imefanya jitihada stahili kuhakikisha taratibu zinafuatwa ili kujiondoa kwenye madhara yanayoweza kutoke baada ya pesa kufuatwa.
Ripoti ya CAG haijamtia hatiani mtu yeyote je kinachozungumzwa na PAC ni sahihi? Au mapendekezo yao kwa Rais yamezingatia utawala bora?.

Haya ni maswali ambayo PAC inapaswa kuyajibu ili umma wa watanzania na sisi wasomi tuelewe kuliko kukaa juu juu na kuimba wimbo wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ajiuzuru, au Katibu wake, Eliakim Maswi ajiuzuru au hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema naye ajiuzuru. Je kujiuzuru kwao ndio suluhisho la matatizo au ndio uzalendo?.

Tunashindwa kuelewa misingi ya kamati ya PAC ya kutaka kuwajibishwa kwa watu hao bila ya kuwa na hatia yeyote ikiwa taasisi ya ukaguzi inasema hakuna kosa lililofanyika, Je PAC wamepata wapi makosa?.

MAPENDEKEZO NA MSIMAMO WETU.


Kwa kuwa Bunge wao wamepeleka maombi yao haramu kwa Rais, nasisi tunapeleka mapendekezo yetu kwa Rais na kumsihi afanye yafuatayo

1. Kwa kuwa Swala zima la ESCROW limegubikwa na siasa, maslahi binafsi, chuki, wivu na kukomeshana, hivyo tunamuomba Rais asitekeleze azimio hata moja mpaka kwanza umma utakapoelezwa ukweli halisi wa mbivu na mbichi na kila lililo nyuma ya pazia kuhusiana na sakata hili
2. Tunamuomba Rais aunde chombo huru, ili swala hili lichunguzwe na kufanyiwa maamuzi huru pamoja na kuviagiza vyombo vyake vya ulinzi na usalama viwachunguze wabunge hawa kwa kukubali kutumiwa, kuhongwa na kununuliwa ili kutuondolea watetezi wetu wa Rasilimali.

Mungu ibariki Tanzania.
Imesomwa na
Josephat Joachim
0768-911840
………………………………………………………
Katibu Mtendaji wa Umoja wa wanazuoni wa Vyuo Vikuu Dodoma.

3.jpg

2.jpg


1.jpeg
 

Attachments

  • 1.jpeg
    1.jpeg
    360.6 KB · Views: 3,036
  • 3.jpeg
    3.jpeg
    521.9 KB · Views: 2,880
Hao wasomi ndio waliokipitisha ccm serikali za mitaa huko Dodoma bila kupingwa.
 
Hao wasomi wamechelewa sana. Marekani ameshasema. Kikwete hana namna!
hahahaha!!! hapo hamna wasomi kabisa. hivi hii tanzania wasomi wanaona siasa tu? jiulize, wasomi walishawahi kutoa tamko kuhusu mauaji ya albino? uharibifu wa mazingira? kuporomoka kwa shilingi ya tanzania? kutokuendelea kwa viwanda? kufeli kwa wanafunzi? mauaji ya tembo? utoroshwaji wa twiga? utoroshwaji wa madini? ajali za barabarani? na mengine kem-kem nsoyajua. wasomi wa tz njaa tu!

i stand to be corrected (kama kuna nlosema hapo na walitoa matamko nisahihishwe)
 
Dodoma University and Company LTD in Dodoma sio vyuo ni vyuo vya sawa na shule za kata. You can not have brain from UDOM and the like
 
Reginald Mengi alitaka kutuharibia nchi yetu

Mkuu, kwani mtu anapojitolea kueleza ukweli sharti alipwe na mtu?

Ni mjinga tu dunia hii ambae atakubaliana na PAC.
hivi hii tanzania wasomi wanaona siasa tu? jiulize, wasomi walishawahi kutoa tamko kuhusu mauaji ya albino? uharibifu wa mazingira? kuporomoka kwa shilingi ya tanzania? kutokuendelea kwa viwanda? kufeli kwa wanafunzi? mauaji ya tembo? utoroshwaji wa twiga? utoroshwaji wa madini? ajali za barabarani? na mengine kem-kem nsoyajua. wasomi wa tz njaa tu!

i stand to be corrected (kama kuna nlosema hapo na walitoa matamko nisahihishwe)
 
Nafikiri mawazo yenu kama mnavyojipambanua kuwa ni wasomi yana mapungufu makubwa sana!
Pengine mkiwa hapohapo Dodoma muwe mnapata nafasi kwanza kutembelea bunge nakuelewa totauti ya ufanyaji au utendaji kazi wa serikali na bunge.
Pengine wazo lenu lawezekana ni nzuri kwa fikra zenu, ila ukweli ni kwamba ripoti ya bunge imepelekwa serikalini kwa ajili ya utekelezaji hivyo basi mheshimiwa sana atatekeleza na kupeleka mrejesho kwa bunge pia.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Back
Top Bottom