Wasomi UDOM waandamana kumuunga mkono JK kuwa mgombea pekee CCM, akerwa na Zitto!

Akili ileile ya utegemezi..

Halafu hizo kompyuta zitawashwa na nyasi au udongo? Umeme wenyewe coverage iko less than 15 % na hakuna plans za kuongeza capacity.

Atasema chochote kile ili kuhakikisha anapata KULA, cha ajabu anakwepa kuzungumzia mafanikio yake ya ahadi alizozitoa katika kampeni ya 2005, au labda ana memory ndogo sana ambayo haiwezi kukumbuka ahadi zake alizozitoa mika mitano iliyopita.
 
"Kuna watu wanasema ninapokuwa ziarani nje naenda kutembea, hapana, nimekutana na wamiliki wa kampuni kubwa za teknolijia ya mawasiliano (IT), wataalam wao wameshakuja nchini kufanya utafiti ili kutuunganisha Tanzania na barabara ya mawasiliano ya IT duniani na itafika mahali watoto wetu watakuwa wanasoma kwa kutumia kompyuta tu, tena wakiwa mbali na mwalimu wao," alisema.
.

Duh sijui ni lini tutafikia hapo maana sasa hivi wanafunzi wapo darasani wamekaa sakafuni kwa kukosa madawati - sasa hatua ya kutoka hapa tulipo hadi kufikia Kujifunza kwa njia ya Computer (video conferencing) mwee!! sasa hii imezikdi kuwa kali.

Tufike mahala tuwe wakweli - linalowezekana kwa sasa lisemwe ambalo haliwezekani liachwe. navyojua mimi technologia ya video conferencing kumfikia mwanafunzi itachukua muda sababu ya resources hakuna.

Mikutano mingapi serikalini inafanywa kwa kutumia njia hii kwa sasa? kama serikali haina technologia hii je lini itamfikia mwanafunzi aliyeko kijijini? je umeme umefika katika level ya vijiji.
 
Masomo kwa Computer kwa Internet ipi iliyo na kasi Tanzania?


Kaka acha kama ilivyo - video conferencing unatakiwa uwe na bandwidth zaidi ya 1MB upstream na downstream dedicated kwa ajili ya kupitisha picha na sauti na hii lazima iwe ni infrastructure kwa nchi nzima (Networked from the central Hub) - sasa kwa mantiki hii duh.

Inawezekana kutumia backbone ya TTCL sababu wamefika hadi kwenye wilaya lakini kwa jinsi shirika lilivyo hoi, na hii project kwa usimamizi wa nani? I don't think so.

Kama itawezekana ipe miaka 100 toka sasa.

 
Kwa kauli zako na Lugha yako (kiingereza cha mtaani), ni dhahiri kwamba wewe siyo Nkunya tunayemfahamu. Si vizuri kutumia majina halisi ya mtu fulani wakati wewe siye. Maana unaweza kumharibia mtu sifa yake na kumgombanisha na watu wake wa karibu. Napendekeza moderator achunguze kwa makini uhalisia wa jina hili.

Ni kweli si busara kutumia majina ya watu hapa JF, hivi ameshindwa kutafuta jina lingine??

 
don't abide with J.K's porojo! jamaa ni bingwa wa porojo sijawahi kuona, halafu anazitamku mbele ya wanafunzi wa chuo kikuu (hivi wanavyuo wa siku hizi wapoje?).
Tatizo la wanafunzi wa leo hawafikirii kuhoji matatizo yanayolikumba taifa kama walivyokuwa wale wa miaka ya 80s na 90s wako bize kugombea bumu.
 
kwani kuna Nkunya mmoja hapa duniani, na kama mtu ametumia nick name ya nkunya what so special hadi moderator aombwe kutathmini JF user names za watu, sioni mantiki yoyote hapa.
 
Aaaah Chuki binafsi hizi. Jamani walioandamana ni wanafunzi wanachama wa CCM mlitaka waandamane kwa chama gani au ndio ukiwa CCM basi wewe ni Muislaam Ukimuunga mkono JK wewe ni Muislaam.. Heee hizi chuki binafsi za makanisani sijui zitaisha lini hali CCM wanazidi kutupiga bao.
Na amini maneno yangu kama mtaendelea na tabia hii JK atashinda vibaya sana, wananchi hawatafuata tena chama wala sera ila dini ya mgombea na hapo mtakwisha. CCM have it all! Ina Wabunge Wakristu karibu kila jimbo lenye Wakristu wengi na Waislaam sehemu za Waislaam wengi, vyama vingine havina hata wabunge wa kutosha majimbo yote..Kazi kwenu wana kristo!
Chuki binafsi haziwezi kuzaa matunda bali mtaumia roho zenu hadi siku mnatiwa kaburini...

Mkandara unapalilia very destructive seed....sijui kwanini ume jump kwenye dini!! OOh God forbid!
Mix with yours
 
JK kakubali kuwa UDOM ni ya Chadema. Wengine je? Kama UDOM ni ya Chadema Kwa maana ya wazo na msisitizo wa utekelezaji kwa nini JK anakataa? Si ni yeye aliyetuambia "AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO"? Kama hivyo si ni rahisi tu kukubali kuwa Chadema walimwambia na yeye akachanganya na za kwake?

Mpaka hapo sioni kama angekuwa amekosea, Lakini haya anayosema na kujibaraghuza ndipo anapokosea kiukweli kabisa.

Wote ambao tunafuatilia maswala ya kisiasa katika taifa hili akiwemo Mh KIngunge na hata Marehemu Mzee Kawawa tunakubaliana kimsingi kuwa wazo la UDOM ni la Chadema ila Limetekelezwa na Kikwete na Wala siyo CCM. Tatizo ni kwamba ametekeleza lakini siyo ambavyo Chadema walivyotaka litekelezwe. Chadema walichotaka kufanya ni kuufanya mkoa wa DODOMA uchumi wake ukuzwa kupitia sector ya elimu. Yaani wawekezaji wawe wengi zaidi kwa kupewa masharti nafuu katika sector ya elimu mkoani Dodoma.
 
Wadanganyika bwana, sasa mnashangaa nini wakati maprofesa karibu wote wanakimbilia CCM... au wanafunzi ndio wasomi zaidi?
 






Na Mwandishi wetu
14th June 2010







Kabwe%281%29.jpg

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe



Rais Jakaya Kikwete amemjibu Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto, Kabwe kuhusu ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), kwamba ilikuwa ni hatua ya kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ingawa hakumataja waziwazi, lakini maneno ya Rais yalionyesha wazi kwamba yalikuwa yakimlenga mbunge huyo.
“Kuna mtu alikuwa anadai kwamba ujenzi wa Udom si utekelezaji wa Ilani ya CCM, lakini ni kwamba tulikaa tukazungumza kuhusu kupanua vyuo vikuu (kwa mujibu wa ilani ya CCM) ndipo tukashauriana kwamba kijengwe chuo kikuu kimoja kikubwa Dodoma,” alisema.
Alisema baada ya kuafikiana, wakaamua kutoa jengo la Chimwaga lililokuwa la chama chao kwa ajili ya kufanyia mikutano kwa ajili ya chuo kikuu kinachotarajiwa kuwa kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki kitakapokamilika.
“Kwa hatua hiyo, sasa tunafanyia vikao vyetu kwenye magodauni kule Kizota,” alisema.
Rais alisema chuo hicho kimejengwa kwa pesa za Watanzania na si wafadhili.
Akichangia Bajeti ya Serikali kwa mwaka fedha 2010/11, mwishoni mwa wiki iliyopita, Zitto alisema kwamba ujenzi wa Udom ambao wabunge wa CCM wamekuwa wakijivunia hauko hata kwenye ilani ya uchaguzi ya chama chao.
Aidha alisema kwamba wazo la kubadilisha Chimwaga kuwa Chuo Kikuu lilitolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwaka 1992.
“Kama kuna mwana-CCM yeyote humu Bungeni basi asimame kisha atusomee ilani ya chama chake kama kuna ahadi ya kujenga Chuo Kikuu Dodoma. Ujenzi wa chuo hiki lilikuwa ni wazo la Chadema tangu mwaka 1992,” alisema Zitto.
Hatua hiyo ilimfanya Mbunge wa Ukerewe, Getrude Mongela kuomba muongozo wa Spika ambapo alisema kwamba ujenzi wa Udom, uko kwenye ilani ya chama chao katika kupengele cha elimu.



CHANZO: NIPASHE
 
Nemesis!
The good part of you ni kwamba Nkunya alishawahi kuwa UDSM, na sasa ni Executive Secretary of TCU.

Huyo tunamfahamu jina lake halisi ni Prof. Mayunga Habibu Hemedi Nkunya, maarufu kama H.H Nkunya, I don't know how can you make it M.M badala ya H.H, anyway ni katika kuelimishana.

Cha msingi ni kwamba jina la mtu sio namba za gari, namba za simu nk hata zisifanane. Hata namba zenyewe kama ni mitandao tofauti zinaweza kufanana vile vile with only different codes, kama zilivyo initials tofauti.
 
Mkandara unapalilia very destructive seed....sijui kwanini ume jump kwenye dini!! OOh God forbid!
Mix with yours
No brother hii issue imekuwa kubwa sana kwenu kwa sababu ya UDom tu hakuna kingine...Chuki binafsi huwa haina aibu. walioandamana ni wanafunzi wanachama wa CCM vyuo vyote vya Dodoma, why pick on UDom?
Changanya na akili yako mkuu!
 
Mkandara (Sijui kama ni Rwekaza)

Kwa suala la VC wa UDSM kuwa kibaraka wa CCM hilo halihusiani na waliyoyafanya wadogo zetu wa UDOM, point yangu ni kuwa,mbona wanakuwa so cheap!!!!juzi juzi walitaka kugoma kwa madai hawana boom,leo 1.2M wametoa wapi?

Zaidi ya hayo, naweza kwenda mbali zaid na kusema kuwa inawezekana hata hizo fedha hazijatoka mifukon mwao, wamepandikiziwa tu ili CCM watuoneshe kuwa wanaungwa mkono na jamii ya wasomi, off course huo ni mchezo mchafu, tumeona Wazee waliochoka kimaisha wa Igunga wakifanya vivyo hivyo, so hilo sio chaguo lao ila tu njaa zao ndo zinawafanya wadharauliwe na sisi wasomi wenzao ila mimi sio wa UDOM (Nilikuwa na qualifications nzuri sana)

Watanzania wote tupo cheap na ndio maana tunatawaliwa na mafisadi. Kama maprofesa na madokta wetu ambao ndio ungetegemea wawe na mawazo badala wamekimbilia kwenye siasa za kifisadi unategemea nini kwa hawa wanafunzi ambao hata pesa ya chakula wanaombaomba?

Tuna uhakika gani kama hawajapewa rushwa kuandamana na kumuunga mkono mgombea wa chama chao? Kwa ufupi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma (sina uhakika kama ni wasomi kweli) ni wawakilishi wa jamii yetu ya watanzania. Hivyo ndivyo tulivyo watanzania na ndio maana hatutaendelea kamwe chini ya utawala huu wa kifisadi.
 
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao ni wanachama wa CHADEMA, CUF na vyama vingine vya upinzani andamaneni kuunga mkono hotuba ya Zitto alooitoa Bungeni juzi wakati akitoa mchango wake kwenye hotuba ya bajeti ya serikali. Vinginevyo mtakuwa "mmekubaliana" na walichokifanya wenzenu wa CCM kwa kukaa kimya na kulalama humu.
 
mkuu nkunya hujui kuwa kikwete ni mlezi wa kile chuo? hujui kuwa yeye ndie aliyefanya juhudi za kukifikisha hapo? hujui kuwa yeye ndie anayetaka kupata umaarufu kupitia chuo hicho? hujui kuwa yeye ndie aliyesema huwa anashangazwa na mtazamo mzima wa majengo ya UDOM? kwamba akifika dodoma huwaamrisha watu wake wampitishe na helkopta juu ya majengo ya UDOM ili aangalie ufahari huo? kwa mantiki hiyo UDOM kwa sasa ndio chuo pekee chenye mandhari ya kuvutia hapa nchini. hii inawasababisia wale 'watoto' kuona fahari kuwa pale kwa kipindi hiki na kupewa upendeleo maalum dhidi ya vyuo vingine. hata UDSM sasa hivi haithaminiwi hivyo. sasa wale vijana wanalipa fadhila ya kuwa karibu na mkuu
 
Back
Top Bottom