Wasomi UDOM waandamana kumuunga mkono JK kuwa mgombea pekee CCM, akerwa na Zitto! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi UDOM waandamana kumuunga mkono JK kuwa mgombea pekee CCM, akerwa na Zitto!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by nsami, Jun 13, 2010.

 1. n

  nsami Senior Member

  #1
  Jun 13, 2010
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyo Dodoma (wanachama wa CCM) leo wamefanya maandamano ya kumunga mkono Mkwere kama mgombea pekee wa urais kwa tiketi ya CCM. Huu ni ujinga na kukuosa kujitambua, inawezekanaje kwa msomi wa Chuo kiku tena anaetegemewa kuleta mapinduzi ya kidemokrasia ktk nchi iliyosinzia kidemokrasia?

  Je ni mkwere huyu huyu anayehubiriwa kuwa anakubalika 75%, anasifiwa kuwa maarufu kuliko chama chenyewe hadi kulewa sifa na kuchagua kura? Je sio huyo ndie aliyesema hataki kura za wafanyakazi? Ni nani anayeogopwa ndani ya chama kuwa akichukua fomu atamuangusha mkwere? Kama 75% ameipata kwa uhalali hii inareflect kuwa anapendwa hata ndani ya chama pia, sasa inakuwaje?

  Huu ni ukandamizaji wa demokrasia unaopaswa kupingwa na wana CCM wenyewe, sio tusubiri akina Slaa na Zito kuja kutuhubiria hilo. Mapinduzi halisi ni yale yanayoanzia ndani ya chama. Wapi zimedumu fikra za mwasisi wa Chama? Ni waliko wazee wa CCM kukemea hilo?

  If we cana not change the system why not change ourselves? Changes are never just happen, but they are caused to happen. We are the one to bring them changes!
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa kauli zako na Lugha yako (kiingereza cha mtaani), ni dhahiri kwamba wewe siyo Nkunya tunayemfahamu.

  Si vizuri kutumia majina halisi ya mtu fulani wakati wewe siye. Maana unaweza kumharibia mtu sifa yake na kumgombanisha na watu wake wa karibu. Napendekeza moderator achunguze kwa makini uhalisia wa jina hili.

  Lakini kwa upande wa hoja yako ya wasomi kumuunga mkono Kikwete, napenda kuungana na wewe kwamba wasomi walipaswa kuwa ndiyo chachu ya mabadiliko. Maana wakulima kule vijijini, pamoja na shida zote wanazopata, wakiona wasomi wamemuunga mkono Kikwete, hawatakuwa na lingine tena.

  Lakini pia ni jambo zuri kutambua kwamba hawa ni wanaCCM, hawana lingine la kufanya zaidi ya hilo la kuunga mkono kinafiki. Ukikaa nao mmoja mmoja utakuta wanalalamika, lakini wakiwa katika chama wanalazimika kufanya hayo wanayoyafanya. Ni haki na wajibu wao.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wacha ujinga wewe, hivi ni wapi mleta thread amejinadi kuwa ni mtu fulani? kwa jina au kwa cheo?
   
 4. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #4
  Jun 13, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Nimesikitishwa sana na kitendo cha Kaka/Dada/Watoto ze/wetu kwa kitendo chao cha kuwa so easy and looser to such an extent ya ku allow politicians wetu wawatumie,inasikitisha sana, ni juzi tu walitaka kugoma kwa madai ya kucheleweshewa boom--meal allowance,leo wanatoa 1.2M kwa mtu ambaye serikjali yake imeeendelea kuwafanya maisha yao vyuon yawe magumu mno.

  I think UDOM ipo for political credits,ila inasikitisha sana kuona wasomi wetu ndo wanakuwa majuha number one,any way,kuna mtu alisema vilaza wanaokosa chance UDSM hufanya UDOM ndo kimbilio lao,nilikuwaga siamin,..ila kwa hili...ninin kitanizuia nisiamin hivyo...
   
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ......&^&%&^%&^((&^%#$^&**())_(*(&^%#$@# !!!! :angry::angry::angry:Na hawa ndio tunategemea wawe na mawazo mapya na vipaumbele vipya? Wanamchangia mtu ambaye anaongoza serikali ambayo kila siku imekuwa inawafanyia vituko??? Wanamchangia mtu huku wazazi wao wanalala njaa??Sasa nimeamini. Aliyeturoga ameishakufa bila kumrithisha mtu uganga wake!
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Bramo,
  Usiwe mwepesi kutoa maamuzi wakati hufahamu chanzo cha haya. Mbona huko UDSM huyo Mukandara ni kibaraka wa chama na watu hawasemi kitu?..Wewe mwenyewe unaweza kuwa umechangia chama au taasisi ambayo mimi siamini kabisa kama unafanya vizuri..Kumbuka tu kuna wana CCM vyuoni iwe chuo kikuu Dar,DOm au Nyegezi. Their choice haihusiani kabisa na matakwa yako.
   
 7. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kesho tu hapo wataanza kuandamana mikopo...ndo hapo huwa wananivunja mbavu..
   
 8. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mi naona hawa ni wale wenye high capacity creming na siyo high capacity understanding, they also know nothing about the next coming 24 hrs in their life, sasa hao ndiyo wanaitwa wa vyuo, kwa mtindo huo utakuta Tz nzima ina wanavyuo ambao ni wasomi na watakao kuwa productive kwa taifa 20% ya wanavyuo waote nchini 80% inayobaki ni pre mafisadinism
   
 9. K

  Kifuna JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 426
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kazi kubwa ya msomi ni kutekenya bongo, kuwaza mambo ambayo watu awengine wa kawaida hawayawazi. wanachambua hoja na kuitathimini wanaiacha wazi ili watu wengine wasioenda shule waweze kujua mbichi na mbivu.

  Sasa kama msomi unaunga mkono mgombea awe pekee hiyo si kazi yako!!! acha wenye kazi hiyo waifanye. na kazi hiyo ya kuwashangilia viongozi wa siasa ndio inayowafanya maprofesa na madokta kujazana mjengoni na kuacha taaluma zao ambazo serikali imewasomesha ili wakasomeshe wanetu wao wanang'ang'ania kuunga mkono hoja kwa tiketi ya chama hata kama hawazikubali.

  Kwa hiyo wasomi nyie msingi mnaouweka si msingi mwema acheni tabia hii si kazi yenu.
   
 10. consigliori

  consigliori JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hiyo ndo demokrasia yenyewe mkuu, haitatokea eti wasomi wote wawe ktk vyama vya upinzani. Ila ni kweli kwa jinsi CCM wanavyoiendesha nchi hii, tungetegemea wasomi wanaouona uozo huu wawe mbele ktk kuleta mabadiliko, lakini ndo hivyo tena, kwenye msafara wa mamba na kenge wamo.
   
 11. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Hao ni wasomi wetu, njaa kali kama nini.

  Nalaani kitendo hicho kibaya cha kudalilisha jamii ya wasomi duniani. Wanaganga njaa, CCM ni Mungu wao.

  Wanasahau JK mwaka 2006 aliwaahidi kuwa hakuna mtoto wa maskini wa kitanzania atakaye kosa elimu sababu tu hana pesa. kilichotokea wengi tunajua, walifukuzwa kama wahuni.

  Hii bangi ndani ya wanavyuo itaisha lini? Wasomi wa Kitz nani kawaloga hata kutaka kumtubisha shetani sala ya toba ? Kushabikia CCM kwa mabaya yake yote ni upofu wa hali ya juu. Ni wendawazimu.
   
 12. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,840
  Likes Received: 1,095
  Trophy Points: 280
  Nadhani hukufanya sahihi kutumia maneno makali kiasi hiki.

  Jamaa anayo hoja ya msingi, juu ya jina la mwanaJF mwenzetu. M.M. Nkunya siku alipojiunga wengi tulisisimka na binafsi niliamua kumuuliza kama ni M.M.Nkunya tunayemjua (huenda wewe humjui ila alikuwa Chief Academic Officer wa UDSM kwa muda mrefu, baada ya hapo (mpaka sasa nadhani) ni CEO wa Tanzania Commission of Universities. Kutokana na madaraka yake huyu ni mtu muhimu ktk jamii. Jamaa kaona lugha iliyotumika haiwezi kutumiwa na Prof. M.M.Nkunya.

  Nami naonelea kuwa si vema kutumia jina la mtu mwingine (kama unatumia nick name). Itakuwa si vema mtu akijitokeza jamvini kujiita J.K. Kikwete au M.L. Luhanga au I.H. Lipumba nk. Haya ni mawazo na mapendekezo binafsi, wala hakuna haja ya kuitana wajinga.
   
 13. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wakimaliza hapo, si muda mrefu wanaanza kuandamana kwaajili ya boom, ni kama kipindi kile wanafunzi wa udsm wanasukuma gari ya kikwete kwenye kampeni pale mlimani...na mwaka huu watasukuma gari lazima..
   
 14. M

  Malila JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kwa bongo yote yanatokea/yanawezekana.
   
 15. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #15
  Jun 13, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Wametoa na 1.2M kabisa ya boom lao.
   
 16. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hili tukio la wasomi wa chuo kikuu kuandamana kwa ajili ya kikwete ni dhihirisho la hali duni ya kiwango cha elimu Tanzania, uwezo mdogo wa kufikiria wa wanafunzi na mategemeo finyu waliyo nayo juu ya maisha. Kama sii hivyo basi ubongo wangu una matatizo
   
 17. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #17
  Jun 13, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Mkandara (Sijui kama ni Rwekaza)

  Kwa suala la VC wa UDSM kuwa kibaraka wa CCM hilo halihusiani na waliyoyafanya wadogo zetu wa UDOM, point yangu ni kuwa,mbona wanakuwa so cheap!!!!juzi juzi walitaka kugoma kwa madai hawana boom,leo 1.2M wametoa wapi?

  Zaidi ya hayo, naweza kwenda mbali zaid na kusema kuwa inawezekana hata hizo fedha hazijatoka mifukon mwao, wamepandikiziwa tu ili CCM watuoneshe kuwa wanaungwa mkono na jamii ya wasomi, off course huo ni mchezo mchafu, tumeona Wazee waliochoka kimaisha wa Igunga wakifanya vivyo hivyo, so hilo sio chaguo lao ila tu njaa zao ndo zinawafanya wadharauliwe na sisi wasomi wenzao ila mimi sio wa UDOM (Nilikuwa na qualifications nzuri sana)
   
 18. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  YAANI AMEWAKAMUA tena watoto bumu lilelile alilowakopesha?
   
 19. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  pathetic..........
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
Loading...