MWITONGO MAARIFA
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 276
- 1,428
Nikifuatilia mswada wa mafao kwa watumishi naona hakuna Mbunge wa CCM, hakuna mtumishi wa umma Wala mwanasiasa kutoka chama tawala anayeona mapungufu ya sheria ile na kanuni zake, ila viongozi wa vyama vya upinzani, wanaharakati na viongozi wengine waliopo nje ya serikali na chama tawala wanaona mapungufu lukuki.
Je Kati ya wasomi ndani ya serikali na nje ya serikali na chama tawala ni nani anayewaza sawasawa kuhusu sheria hiyo?
Sheria ya makosa ya mtandao pia inatetewa na serikali na chama tawala na watumishi wa umma lakini asasi za kirai,wanaharakati na vyama vya upinzani wanaona kasoro lukuki. Je wasomi wapi wapo sahihi Kati ya makundi haya mawili?mbona wamesoma vyuo sawa na wote wakafaulu?
Sheria ya takwimu, CCM na watumishi wa umma walisema ni mzuri na inatija kwa taifa lakini wanaharakati na wanasiasa wa upinzani wakaukataa na baadaye wazungu wakaingilia Kati. Wazungu waliposema serikali ikawasikia kidogo lakini tofauti ya hoja ya wazungu na wanaharakati wazawa ilikuwa ni KIINGEREZA kilichopambwa na misaada.Je na hapo napo wasomi waliona makengeza?
Mswada wa vyama vya siasa hivyohivyo, kwanini wasomi wanagawanyika kwenye hoja ambazo zipo wazi? Unafiki huu unaletwa na Nini? Kati ya makundi haya mawili ya wasomi lipi linainyonya nchi? Kindi lipi limejaa wasomi wasio wazalendo na wabinafsi?
Moja jumlisha moja ni mbili lakini upo wakati inakuwa tatu na jibu hilo linasimamiwa na Dolla na kupigiwa makofi na watunga sheria